​hahahaaaa!!ulivyoshadadia duuuh!!ngoja Mushi arudi. Aendelee kusubiri tu.ngoja nimpe RIP mapema hakuna kitu kinauma kama kumegewa mke na ukajua.
ngoja Mushi arudi
Napenda kutofautiana na washauri wote wa hapo juu!
Mambo ya kuripoti polisi wakati unajijua ushagonga mke wa mtu na mwenye mali ana ushahidi ni kukuza tatizo x 100000...unaweza ukamshinda mdai wako kwa mambo ya kipolisi, lakini kimtaamtaa ishu itakuwa na moto wa gesi, na akufuatilia kama vile anatrack nyayo za simba.
Binafsi ninachoona chaweza kufanyika kikasaidia ni jamaa awe mpole.
Ajikubalie moyoni kwamba ametenda hilo kosa na hawezi kujificha popote...U can run but you cant hide.!
Akishajikubali kuwa amekosa asisubiri jamaa arudi, aulizie huyo mhandisi yuko mkoa gani, na amfuate kiumeni hukohuko mkoa, afanye mbinu yoyote akutanishwe nae na aongee kwa maana ya kuomba Msamaha na kumsihi jamaa yaishe!
Zaidi ya hapo binafsi sioni njia yenye usalama!...
Ushauri wa eti ahame nyumba au akimbilie mkoa mwingine ndiyo kumrahisishia mhandisi kumnyofoa jamaa bandama kwa kutumia vijana au wazee wa kazi!
Mwambie jamaa afuate ushauri huu, hapa bana hakuna kujifanya mjanja, mke wa mtu ni kifo na asipofanya hivi nilivoshauri atarajie BIG RESULTS NOW.
Nawasilisha.
Kuna jamaa yangu amepata janga,
Amepigiwa simu na baba mwene nyumba wake akamtaarifu kwamba amepata taarifa zenye ushahidi kwamba yeye huyo mshkaji wangu anatembea na mke wake, na akirudi lazima amtoe maini . Huyo jamaa mwenye nyumba ni contractor kwa sasa yupo safarini.
Jamaa kweli amekiri alikuwa anatoka na huyo mama kwa muda kabla hata hajaoa. Jamaa anasema huyo mama ndiye aliyejilengesha kwake, jamaa kwa tamaa na kushindwa uzalendo akamkubali, Mama mwenyewe hata sio mzuri sana anamiaka kama 30 na amezaa na huyo mume wake watoto 2.
Jamaa yangu ameshaishi kwa huyo mama zaidi ya miaka 2 amerenew juzijuzi tu mkataba wake wa mwaka wa 3.
Huyo mama ni mke mdogo wa huyo mkandarasi ambaye amemjengea nyumba ya ukweli maeneo ya kihonda huku moro ambayo ina servant quarter kubwa kwa nyuma ambayo ndio amepangishiwa mshakji wangu.
Huyo mkandarasi anasafiri sana na ana mke mkubwa mwingine pia hivyo mara nyingi haji hapo kwa huyo bi mdogo, ila anamgharamia kila kitu na amempatia harrier ya kutembelea,
Kuna kipindi huyo jamaa yangu kabla hajanunua gari yake nilikuwa namuona na hiyo harrier ya huyo mama alikuwa anakuja nayo hata job na kushinda nayo kama yake ,huyo bi mdogo ni mama wa nyumbani hiyo gari haitumii sana, wala hapendi kuendesha, huyo mshkaji wangu alikuwa pia kama dreva wa huyo mama,mida ya jioni akitoka job au siku nyingine akiwa off alikuwa anampeleka huyo bi mdogo sokoni na saloon,
Mshakji ndio ameoa hivi karibuni miezi kama 3 imepita amemuoa aliyekuwa mchumba wake na anaujauzito wa miezi 7.
Huyo mke wa mshkaji naye amepata hizo taarifa na amekasirika sana amemwambia mshkaji ampe nauli arudi kwao songea.
Jamaa ni mtumishi ameajiriwa kwenye idara ya serikali.
Huyo jamaa yangu ameghafirika sana hajui jamaa anaushaidi gani na atarudi lini, na ana hofu ya maisha yake, ana mpango wa kukimbia ahame mkoa kwa kuogopa, huyo bi mdogo naye kamchunia sijui naye kapigwa mkwara na mume wake.
Tumemshauri atulie amuombe mke wake msamaha na atafute nyumba nyingine wahame hapo kwenye hiyo nyumba haraka na ikiwezekana aende kuripoti polisi. Akikimbia anaweza kufukuzwa kazi.
Ushauri wa ziada kwa huyu ndugu yetu manake anaogopa sana.
Lazima kuna sehemu amekosea ,ila hilo sio kubwa kulitatua ,na yeye ashushe mkwala na atafute mguu wa kuku atembee nao ,ila asikubali kabisa kabisa akatae kwa nguvu zake zote .
mkuu Mwiba habari ya siku ulipotelea wapi ndugu yangu, karibu tena
naunga mkonpo hoja inawezekana jamaa anamtisha tu hana ushahidi, madam hajawafumania live, basi ahame hapo ijapokuwa ni tuhuma, aripoti polisi kama ana ushahisi wa vitisho...baas...kwanza jamaa sio mke wake, ni ka nyumba kadogo tu, namshauri asome ile the Guide yetu
na huyu babu asprin leo anachezewa wapp hayo masharubu mbona simuon on board??mkuu Mwiba habari ya siku ulipotelea wapi ndugu yangu, karibu tena
naunga mkonpo hoja inawezekana jamaa anamtisha tu hana ushahidi, madam hajawafumania live, basi ahame hapo ijapokuwa ni tuhuma, aripoti polisi kama ana ushahisi wa vitisho...baas...kwanza jamaa sio mke wake, ni ka nyumba kadogo tu, namshauri asome ile the Guide yetu
duuu, hi ni noma,ingemkuta ka hii , sijui ingekuwaje.Aangalie isijemkuta kama hii
![]()
sio mimi rafikiHapo kwenye red andika ..NIMEPATA JANGA...
Wote washenzy tu sioni innocent party kwenye hii case
mke wa jamaa ni innocent