Jamaa aliyetaka kutapeliwa akashtuka akamtapeli mtapeli

Wadau tuwekane hapa wazi kwa sisi ambao tumewahi shtukia matapeli.

Mwaka juzi kuna jamaa mmoja ilitokea tulikutana bar. Alikuja meza yangu akakaa tukaongea ongea na kuwa friends.alinambia yeye ni mgeni dar anakuwa sana arusha.

Anafanya biashara ya madini so akija huwa anafikia hotel...katika maongezi tukafahamiana sana.alilipia mpaka beers zangu.nlimkatalia sana akaomba alipe sababu amefurahi kupata rafiki mwema.

Nikajiwazia nikasema tu moyoni hiiiii "yaani mimi ni mwema?"

Basi akanipa ni biznez kadi yake tukaagana tena akimwita dereva aje pia anifahamu.akiwa dar huwa anakuwa na dereva wake.

Tukawa friends after some weeks nlimkaribisha hadi home.alipapenda sana home.siku amekuja alinunua zawadi kwa watoto na wife.almost alitumia kama 200,000+

Jamaa alikuwa mpole sana anaongea kwa upole and very smart. Anapiga sana suit alikuwa akija anatumia uber au prado moja kali sana na dereva wake.

Alinambia anajenga mbezi beach alinunua kiwanja milion 150. So ujenzi unaendelea weekend moja akaniomba akanioneshe hiyo nyumba maana akiwa nje ya nchi anakosa mtu wa kumwangalizia.

Alinipeleka mbezi beach nikakuta mafundi wapo wamechangamka wakimwita mzee na kumweleza mahitaji.fundi akasema wapewe milion 8 kuna vitu vya kununua.akaomba account ya bank ya fundi akasema ataenda mtumia jumatatu.ila kwa siku hiyo akamtumia tsh mil 1 ya matumizi tu wagawane weekend.

Jamaa alikuwa fresh sana.alianza kunipa stories za biashara ya madini.akitaka niweke mtaji hata wa mil 30 ngepata mil 45 ndani ya week tu.akinishauri niende naye arusha tukanunue dhahabu then anapoenda South Afrika twende sote akanioneshe wateja.

Hapo akili ilianza ku alert.jamaa alikuwa busy na simu kuongea na wateja sometimes aliweka tu loud speaker.nlianza kushtuka kuwa jamaa yupo fast sana kunishawish.wife nikimsimulia ananambia kazi niache hata siku hiyo nikapige pesa.

Nikawa namwambia si rahisi kiivyo asubiri nifanye utafiti kwanza. Weekend moja nikapita mbezi nikakumbuka mjengo wa jamaa.kupita ile sehemu hakuna mafundi.

Nikauliza kwa vijana jirani kuwa ile nyumba nliitamani nikitaka kupata ramani yake mwenyewe yu wapi.wakanambia mwenye nayo alifungwa kwa madawa ya kulevya toka mwaka 2016. Na haijawahi guswa tena.

Nliwadodosa sana jamaa wakasema imeachwa hivyo tu ila kuna siku jamaa mmoja alikuja wakaja na mafundi wakapotea tena.

Nliporudi home nikawasiliana na jamaa.nikamuuliza ujenzi unaendeleaje.akasema safi kabisa mafundi toka siku ile wanapiga kazi mchana na usiku na jana tu alikuwa nao.anataka iishe ndani ya miezi 3. Ahamie dar.coz ana nyumba dar na south afrika.

Kesho yake nikapita tena ile sehemu.nikakuta kimya hakuna fundi hata mmoja.

Nikamuuliza tena vipi speed ya mafundi wake nataka nami nije niwatumie.akasema wapo vizuri leo tu kawapelekea vifaa vya mil 10. Hapo ndo nikashtuka zaidi.jamaa alikuwa mwongo.

After two days nikaonana naye town.nlimwambia anisaidie 50,000 ya haraka ntampatia nikifika ofisini nmesahau biz cards zangu zote aliniazima. Nlipofika ofisini nilimwambia nmempiga picha nmetuma kwa jamaa yangu polisi akatafute mtu mwingine wa kumtapeli.

Kuanzia muda huo hakupatikana tena.sijui alihamia wapi.ila niseme jamaa alikuwa vizuri.anaongea kiingereza vizuri.anajua nchi nyingi duniani.

Jamaa alikuwa amejipanga vizuri sana.alinikosa kosa sababu mimi kwenye issues za pesa huwa nachunguza sana.mzito kuamua ghafla.

Siamini katika deals ambazo zinaleta pesa kirahisi rahisi sana.ambazo hesabu zke hazimake sense.

Walinishinswa forever living,wakanishindwa gnld,wakanishindwa wazee wa goodmorning all time. Sipatikani katika kutapeliwa.

Tupeane shuhuda mbalimbali za kutapeli na kutapeliwa.mimi nlimtapeli jamaa 50,000. Na kumuingiza hasara kwa zawad ambazo alileta kwa wife na watoto wangu.

Ntaleta kisa kingine cha bi dada mmoja ambaye alitaka kunitapeli kupitia mapenzi.
Ungejichnganya kidogo tu ukaamua tuseme kukubali kwenda naye SA, angeweza hata kukua!
 
Hilo halina shida.nlishamchimba biti kali sana na hata hawezi kuwaza rudi home. Actually matapeli ni waoga kuwa violent. Wao hutumia akili.wakiona umeshtuka wanaanza mbele kutafuta victim mwingine.

Hilo halina shida nlishamwambia nmekabidhi kila kitu chake kwa ndugu yangu polisi.likitokea lolote atatafutwa.

Mtu akiwa na nia ya kujua unapoishi ni rahisi sana. We mwenyewe fikiria.madereva wangapi wa bajaji,bodaboda wamewahi kukufikisha kwako? Wangapi wamewahi kukufuatilia unapoishi wakafika bila wewe kujua?

Kosa kubwa ulilofanya ni kumuonyesha nyumbani kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa wanabadilisha madini. Anakuachia fake anaondoka nayo real.so mkifika huko anakupotea wakati huo wewe una madini huna waswasi sana.ukienda kutaka uza au pima ndo unagundua ni fake yeye alichukua yale original.

Ungejichnganya kidogo tu ukaamua tuseme kukubali kwenda naye SA, angeweza hata kukua!
 
Aisee unawajua mataperi au unawasikia wakiwa washakutarget na kukuona una mpunga shukuruni hapa mshapata trick mpya ila ukiingia kingi hutoki
simlaumu jamaa matapeli huwa hawamtapeli mtu kiboya huwa wanakufatilia pengne hata miezi 2 hata mitatu kukupeleleza kiasi wakikuibukia washajua udhaifu wako na hutumia udhaifu huo kufanikisha jambo lao au tuseme tamaa km jamaa alivyobainisha hapo kutoka katika kitabu na tamaa ya pesa ya haraka ndo huponza
mfano mm nilitapeliwa kiboya tuu mpk leo najiona fala sana kuhaminishwa niliachiwa ESCUDO kipindi hicho zinatamba siku 3 na funguo nikapewa kuja kupata akili dadeki nishaingizwa chaka
hao wajomba wakuitwa mataperi omba usikutane nao

jambo zuri taperi ni kuwa 90% ya mataperi hawadhuru mtu mwili na mioyo hiyo hawana na hawawezi ndo mana akaamua kuwa taperi 7bu huwa smart kichwani na wengine wamepiga shure vizuri tu na magentleman haswa na km ukimkuta mdada ni PISI ya maana huwezi mkuta taperi muhunimuhuni mvuta bangi au mwenye muonekano wa kilevi 7bu utamtilia shaka tu
na taperi akipiga tukio au akishtukiwa anahana hilo eneo au mkoa hata miaka miwiri

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna jamaa yangu kipindi fulani cha miaka ya 90 mwishoni, aliamua kwenda Kagera, akaenda akakaa kwa jamaa fulani halafu akawa anavaa Lubega nyeusi, miguuni amejipaka masizi meusi, akijidai kuwa ni mgonjwa halafu huyo jamaa yake akawa anigiza kuwa ndiyo mganga wa kienyeji. Watu kuona hivyo wakawa wanamiminika kwa wingi nyumbani hapo, kwa ajili ya kupata tiba ya miguu na mambo mengine, huku yeye akiwashuhudia kuwa alifika akiwa ana hali mbaya lakini mganga amemsaidia sana kuimarisha afya yake. Walipiga hela ndefu halafu baadaye akapotea. Baadhi ya wagonjwa walikuja kustuka baadaye, kuja kuonana naye walipomuuliza, akawaambia kuwa hata yeye alienda pale kupata tiba kama wao walivyokuwa wakifanya kwa hiyo yeye hakuwa tapeli isipokuwa yule mganga, kwa hiyo akawa anawaelekeza waende wakamuulize mganga wao aliyekuwa akiwatibu.

Kesi nyingine tena akawa yuko anasafiri kwa Baiskeli iliyokuwa imechoka sana, alikuwa anaeleka Magu. Kukaribia Magu akawa amekamatwa kwa kutokuwa amekata kodi ya Baiskeli, kipindi hicho baiskeli zilikuwa zinakatiwa kodi kwa mwwaka. Wakamataji wakamlazimisha aidha akate kodi pamoja na kutoa faini, au aiache Baiskeli akatafute hela halafu akipata, arudi aje achukue Baiskeli. Jamaa kuona hivyo akaona ni dili kama la "900 itapendeza", akawaachia Baiskeli na hawakuandikishana. Akatembea kwa mguu mpaka Magu mjini. Kufika mjini akaenda kwenye duka la rafiki yake, akaomba kuandikiwa risiti ya Baiskeli mpya aina ya Phoenix, halafu tarehe za risiti zikarudishwa nyuma miezi kadhaa. Kesho yake akawarudia watoza ushuru, akawapa hela yao ya faini, akalipia na kodi ya Baiskeli, halafu akawaomba sasa wamrudishie Baiskeli yake. Walivyoileta Baiskeli ile ile aliyokuwa amewaachia jana yake, akaikataa, akasema kuwa yeye Baiskeli yake ilikuwa ni mpya aina ya Phoenix, akawaonyesha na risiti akidai kuwa ameinunua siku siyo nyingi na ndiyo maana hata risiti yake huwa anatembea nayo siku zote. Kilichotokea baada ya mvurugano huo, ilibidi wahusika wakanunue Baiskeli mpya aina ya Phoenix, wakamkabidhi akaondoka na Baiskeli mpya, akawaachia mkweche.

Hata hivyo huyu ni tapeli perce na utapeli wake haufanani na ule wa kwako
 
Ulimtapeli ndio, hupotezi pesa kirahisi ndio ila still kumpeleka stranger kwa familia yako na kuruhusu awahudumie sijui awape zawadi you are still dumb.

Bora ungetapeliwa maana pesa inatafutwa. MUNGU aepushie mbali ila Ukisikia mkeo kaviziwa kafanyiwa mambo ya ajabu ujue ww ndo ulifanya utambulisho.

Protect your family mkuu, take risk za aina zote ila si familia.
By the way, mm naona jamaa alikurahisishia sana kumgundua baada ya kukupeleka sight.
Tatizo kubwa la huyo tapeli ni speed ya kufanya deal.
 
Umempeleka nyumbani hapo tayari amesha kutapeli zaidi ya hiyo 50k yako na vijizawadi ulivyo mtapeli, yaani familia yako itakuja kupigwa ambush moja matata hadi uchanganikiwe, tembo hasahau njia yake
tapeli hapo akanyagi teena, nina wajua sana hao watu. sio watu wa kutumia nguvu na kabla jamaa hajamkaribishwa nyumbani kwake huyo tapeli tayari alikua anapajua kitambo.
 
V
Wadau tuwekane hapa wazi kwa sisi ambao tumewahi shtukia matapeli.

Mwaka juzi kuna jamaa mmoja ilitokea tulikutana bar. Alikuja meza yangu akakaa tukaongea ongea na kuwa friends.alinambia yeye ni mgeni dar anakuwa sana arusha.

Anafanya biashara ya madini so akija huwa anafikia hotel...katika maongezi tukafahamiana sana.alilipia mpaka beers zangu.nlimkatalia sana akaomba alipe sababu amefurahi kupata rafiki mwema.

Nikajiwazia nikasema tu moyoni hiiiii "yaani mimi ni mwema?"

Basi akanipa ni biznez kadi yake tukaagana tena akimwita dereva aje pia anifahamu.akiwa dar huwa anakuwa na dereva wake.

Tukawa friends after some weeks nlimkaribisha hadi home.alipapenda sana home.siku amekuja alinunua zawadi kwa watoto na wife.almost alitumia kama 200,000+

Jamaa alikuwa mpole sana anaongea kwa upole and very smart. Anapiga sana suit alikuwa akija anatumia uber au prado moja kali sana na dereva wake.

Alinambia anajenga mbezi beach alinunua kiwanja milion 150. So ujenzi unaendelea weekend moja akaniomba akanioneshe hiyo nyumba maana akiwa nje ya nchi anakosa mtu wa kumwangalizia.

Alinipeleka mbezi beach nikakuta mafundi wapo wamechangamka wakimwita mzee na kumweleza mahitaji.fundi akasema wapewe milion 8 kuna vitu vya kununua.akaomba account ya bank ya fundi akasema ataenda mtumia jumatatu.ila kwa siku hiyo akamtumia tsh mil 1 ya matumizi tu wagawane weekend.

Jamaa alikuwa fresh sana.alianza kunipa stories za biashara ya madini.akitaka niweke mtaji hata wa mil 30 ngepata mil 45 ndani ya week tu.akinishauri niende naye arusha tukanunue dhahabu then anapoenda South Afrika twende sote akanioneshe wateja.

Hapo akili ilianza ku alert.jamaa alikuwa busy na simu kuongea na wateja sometimes aliweka tu loud speaker.nlianza kushtuka kuwa jamaa yupo fast sana kunishawish.wife nikimsimulia ananambia kazi niache hata siku hiyo nikapige pesa.

Nikawa namwambia si rahisi kiivyo asubiri nifanye utafiti kwanza. Weekend moja nikapita mbezi nikakumbuka mjengo wa jamaa.kupita ile sehemu hakuna mafundi.

Nikauliza kwa vijana jirani kuwa ile nyumba nliitamani nikitaka kupata ramani yake mwenyewe yu wapi.wakanambia mwenye nayo alifungwa kwa madawa ya kulevya toka mwaka 2016. Na haijawahi guswa tena.

Nliwadodosa sana jamaa wakasema imeachwa hivyo tu ila kuna siku jamaa mmoja alikuja wakaja na mafundi wakapotea tena.

Nliporudi home nikawasiliana na jamaa.nikamuuliza ujenzi unaendeleaje.akasema safi kabisa mafundi toka siku ile wanapiga kazi mchana na usiku na jana tu alikuwa nao.anataka iishe ndani ya miezi 3. Ahamie dar.coz ana nyumba dar na south afrika.

Kesho yake nikapita tena ile sehemu.nikakuta kimya hakuna fundi hata mmoja.

Nikamuuliza tena vipi speed ya mafundi wake nataka nami nije niwatumie.akasema wapo vizuri leo tu kawapelekea vifaa vya mil 10. Hapo ndo nikashtuka zaidi.jamaa alikuwa mwongo.

After two days nikaonana naye town.nlimwambia anisaidie 50,000 ya haraka ntampatia nikifika ofisini nmesahau biz cards zangu zote aliniazima. Nlipofika ofisini nilimwambia nmempiga picha nmetuma kwa jamaa yangu polisi akatafute mtu mwingine wa kumtapeli.

Kuanzia muda huo hakupatikana tena.sijui alihamia wapi.ila niseme jamaa alikuwa vizuri.anaongea kiingereza vizuri.anajua nchi nyingi duniani.

Jamaa alikuwa amejipanga vizuri sana.alinikosa kosa sababu mimi kwenye issues za pesa huwa nachunguza sana.mzito kuamua ghafla.

Siamini katika deals ambazo zinaleta pesa kirahisi rahisi sana.ambazo hesabu zke hazimake sense.

Walinishinswa forever living,wakanishindwa gnld,wakanishindwa wazee wa goodmorning all time. Sipatikani katika kutapeliwa.

Tupeane shuhuda mbalimbali za kutapeli na kutapeliwa.mimi nlimtapeli jamaa 50,000. Na kumuingiza hasara kwa zawad ambazo alileta kwa wife na watoto wangu.

Ntaleta kisa kingine cha bi dada mmoja ambaye alitaka kunitapeli kupitia mapenzi.
"Very smart fellow"
 
Kuna jamaa yangu kipindi fulani cha miaka ya 90 mwishoni, aliamua kwenda Kagera, akaenda akakaa kwa jamaa fulani halafu akawa anavaa Lubega nyeusi, miguuni amejipaka masizi meusi, akijidai kuwa ni mgonjwa halafu huyo jamaa yake akawa anigiza kuwa ndiyo mganga wa kienyeji. Watu kuona hivyo wakawa wanamiminika kwa wingi nyumbani hapo, kwa ajili ya kupata tiba ya miguu na mambo mengine, huku yeye akiwashuhudia kuwa alifika akiwa ana hali mbaya lakini mganga amemsaidia sana kuimarisha afya yake. Walipiga hela ndefu halafu baadaye akapotea. Baadhi ya wagonjwa walikuja kustuka baadaye, kuja kuonana naye walipomuuliza, akawaambia kuwa hata yeye alienda pale kupata tiba kama wao walivyokuwa wakifanya kwa hiyo yeye hakuwa tapeli isipokuwa yule mganga, kwa hiyo akawa anawaelekeza waende wakamuulize mganga wao aliyekuwa akiwatibu.

Kesi nyingine tena akawa yuko anasafiri kwa Baiskeli iliyokuwa imechoka sana, alikuwa anaeleka Magu. Kukaribia Magu akawa amekamatwa kwa kutokuwa amekata kodi ya Baiskeli, kipindi hicho baiskeli zilikuwa zinakatiwa kodi kwa mwwaka. Wakamataji wakamlazimisha aidha akate kodi pamoja na kutoa faini, au aiache Baiskeli akatafute hela halafu akipata, arudi aje achukue Baiskeli. Jamaa kuona hivyo akaona ni dili kama la "900 itapendeza", akawaachia Baiskeli na hawakuandikishana. Akatembea kwa mguu mpaka Magu mjini. Kufika mjini akaenda kwenye duka la rafiki yake, akaomba kuandikiwa risiti ya Baiskeli mpya aina ya Phoenix, halafu tarehe za risiti zikarudishwa nyuma miezi kadhaa. Kesho yake akawarudia watoza ushuru, akawapa hela yao ya faini, akalipia na kodi ya Baiskeli, halafu akawaomba sasa wamrudishie Baiskeli yake. Walivyoileta Baiskeli ile ile aliyokuwa amewaachia jana yake, akaikataa, akasema kuwa yeye Baiskeli yake ilikuwa ni mpya aina ya Phoenix, akawaonyesha na risiti akidai kuwa ameinunua siku siyo nyingi na ndiyo maana hata risiti yake huwa anatembea nayo siku zote. Kilichotokea baada ya mvurugano huo, ilibidi wahusika wakanunue Baiskeli mpya aina ya Phoenix, wakamkabidhi akaondoka na Baiskeli mpya, akawaachia mkweche.

Hata hivyo huyu ni tapeli perce na utapeli wake haufanani na ule wa kwako
Nimejifunza somo kubwa sana hapa
 
Tupeane shuhuda mbalimbali za kutapeli na kutapeliwa.mimi nlimtapeli jamaa 50,000. Na kumuingiza hasara kwa zawad ambazo alileta kwa wife na watoto wangu.

Mkuu, hapo kwenye Zawadi kwa Jamaa kwa Wife, kuwa Makini, asijekuwa aliondoka na Namba ya simu ya Shem.
Na umemsifia Jamaa kuwa ni Laghai na tapeli, hebu angalia katika Muktadha huo pia....
 
Nimejifunza somo kubwa sana hapa
Siri nyingine kubwa kwenye haya mambo, mara nyingi the advantaged huwa hawako samart kama the disadvantaged. Nadhani ni kwa sababu wanakuwa wanajua kuwa sheria iko upande wao, na wanakuwa hawana shaka na mtu. Kwa hiyo inapotokea the disadvantaged akawa na courage ya kufanya kitu cha kuwaumiza the advantaged, uwezekano wa kufanikiwa huwa ni mkubwa sana
 
Back
Top Bottom