CHADEMA Waache "ushamba"

CHADEMA Waache "ushamba"

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
500
Reaction score
488
Chadema ya Tundu Lissu na John Heche wamekuwa na utamaduni mbaya sana hasa kuhusu VIFO.Kwanza wamekuwa VINARA wa kushangilia VIFO vyote vya Wanaccm na Viongozi wa Serikali "Utamduni" ambao hatukuwahi kuwa nao wakati wa Uongozi wa Mzee Freeman Mbowe.

Lakini pia wamekuja na utamaduni mpya tena kwamba kila KIFO cha Mwanachadema lawama zimekuwa zinakwenda kwa Serikali lakini hauwezi kusikia VIFO vya VIONGOZI na Wanaccm kwamba lawama wanatupiwa Chadema.

Wakati huu wa kifo cha Dereva wa Makamu Mwenyekiti,John Heche kimetokea,kumekuwepo na juhudi kubwa za kutaka kuiaminisha jamii kwamba kifo cha Suez Maradufu sio kifo cha kawaida.

Wakati Jeshi la Polisi wakifanya Uchunguzi wa kitabibu kujua chanzo cha kifo hicho,Chadema wakaibuka na HOJA kuwa wanataka mtu wao ashiriki kwenye Uchunguzi wa kidaktari.
Serikali IKAKUBALI.

Soma Pia: Dereva wa John Heche akutwa amefariki chumbani Kigoma

PAMOJA NA HAYO KUNA MAMBO YA MSINGI YA KUJIULIZA HAPA.

Inasemekana Dereva huyo wa Ndugu John Heche amekuwa na msongo wa mawazo wa muda mrefu sana kutokana na kutokupata STAHIKI zake toka kwa John Heche na Chama.

Uthibitisho wa hilo ni nyumba ya wageni ambayo alikutwa Marehemu Suez Maradufu amefariki,ilikuwa ya kiwango cha chini sana na hauwezi kutegemea kuwa Dereva ya mtu kama John Heche angeweza "kujiegesha" hapo.

Kwanza ni sehemu isiyo salama kiafya na hata kiulinzi kwani Nyumba hiyo ilikuwa haina hata UKUTA wa Fensi.Nyumba hiyo inakadiliwa kitoza malazi kati ya Tsh 10,000 -12,000 wakati John Heche alikuwa amelala nyumba ya kati ya Tshs 100,000 -150,000.

Ishu ya pili ya kujiuliza ni kwamba,kama kweli Dereva wa Heche KAUWAWA,swali la kawaida ni kwamba hivi,nani anaweza kuwa "TARGET" kati ya Dereva wake au John Heche mwenyewe?Yaani Serikali iangaike na Dereva ambaye labda hata kwenye KIKAO cha ndani cha Chadema cha Kigoma HAKUINGIA,HANA taarifa yoyote ya maana zaidi ya kuwa na taarifa za gari na mafuta🤣🤣

Huyu mtu(Marehemu) wakati wa upekuzi wa POLISI kakutwa na vidonge ndani ya Chumba cha kulala, ISHU ambayo Naibu Katibu Mkuu,Amani Golongwa hajataka kuongelea kabisa.

Kuna uwezekano labda Dereva huyu alikuwa ANAUMWA kabla ya kwenda kulala,lakini zipo taarifa kuwa Marehemu Suez alikutwa na vidonge vya kuongeza nguvu za kiume pia.

Pamoja na kwamba Katika Uchunguzi wa kidaktari MTU wa Chadema alishiriki lakini mpaka sasa hajasema au kukiri uwepo wa hujuma katika KIFO hicho.

Ufike wakati tukubali tu kuwa kifo kaumbiwa Mwanadamu na siku ikifika imefika.Wananchi wapuuzeni hawa jamaa(Chadema).
 
Kwamba chumba alicholala dereva kilikuwa duni/cha bei ya chini.
SWALI:Je,hivyo vyumba vya bei ya chini kwenye hiyo "nyumba",wamekufa wangapi kabla na hata baada ya dereva tajwa kwa huo uduni?
SWALI:Ulitaka target awe John Heche?Umewahi kufuatilia mbinu chafu za wauaji kwa kupenda kuua walio karibu na target,wapendwa au ndugu zao?Unaelewa sababu?Kwanza huwa ni kumtisha mlengwa mkuu,kumpa onyo ili abadilike kadiri watakavyo/liquidations.
Pili,unajua kwa nini dereva wa Lissu alisakwa mno kabla hajaenda Ubelgiji?Nia kuu ni ku-mframe/kumsingizia mauaji target wao mkuu.Kwa hiyo acha uzwazwa wako ukishashiba mayai ya kuchemsha na mahindi ya kuchoma.
 
Back
Top Bottom