Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

Watakuja watu kubeza hayo mafanikio. Mimi huwa nnawaambia wachanganye awamu zote waone kama Kikwete hajafanya zaidi ya wote.

HAWA NDO UITWA BENDERA FUATA UPEPO, MLIMSIFIA FISADI MKAPA, SASA MNAMSIFIA JK, BADAE UTAMUONA ANAMSIFIA CHENGE, HUNA LOLOTE BWE..GE Wee
 
Dada yangu. Hbari za leo. Mzee Mwinyi ana msemo mzuri ila sijui kama na yeye kautoa kwa mtu mwingine "Kila zama na kitabu chake" Hatuwezi kuangalia mafaniko ya Kikwete kwa kulinganisha na awamu zilizopita and that how to think beyond time and space. Lakini tukiangalia kwa kulinganisha na awamu zilizopita tunaweza tukajikuta Kikwete si lolote wala chochote maana unaweza ukakuta plans na financial resources ziliandaliwa na serikali zilizopita na hapo tukaanza ubishi wa kati ya kuku na mayai ni kipi kilianza? Tuangalie mafanikio ya Kikwete na tuyapime kutegemea na resources tulizojaliwa na kuona je kuna urari? Kama kuna kasoro kwenye hizi projects either architected or implemented by him tuseme na tutakuwa tumemtendea haki maana anaweza kurekebisha kabla ya kuondoka na kuweza kuiacha positive legacy. Lakini tukimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kuwa kila alilolifanya halina mawaa kesho akishatoka tutaanza kumwanika wakati haya mapungufu yalikuwepo na yeye alikuwa na uwezo wa kuyarekebisha. Mfano ni hili la katiba mpya na mapungufu. Yapo na mengi katika uadaaji wake na utekelezaji wake ambapo CCM wamelazimisha vitu ambavyo wenyewe wamekuwa na wanaendelea kuvilalamikia na ukiwauliza wanasema bunge la katiba lilikuwa mradi wa kula hela. Yaani nchi inawekwa rehani kwa maslahi ya chama kimoja sijui kwa faida ya kudumu au isyo ya kudumu. Kuna kashfa zilizojitokeza katika kipindi cha awamu na zimemalizwa kishabiki na kulindana kiasi kwamba taifa limejiandalia bomu litakalokuja kulipuka baadae. Nchi haina dira na maadili ya kitaifa(hili sio tatizo lake peke yake) na hili kidogo rasimu ya Warioba ilijaribu kulipatia ufumbuzi ingawa sio wa kimalaika lakini wajumbe walionyesha uzalendo mkubwa ilikuwa ni kuongezea uzito na kuzifanya kuwa sehemu ya katiba. Hayo ni kwa ufupi. Mbali na mafanikio yake lakini bado ana mapungufu tena mengi ambayo anaweza kuyatatua baadhi au kumwekea misingi chanya ajaye ili apate pa kuanzia

Hata mwaka wa biashara kimafanikio unafananishwa na uliopita. Itakuwa nchi?

Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
 
Mafanikio ya kushindwa kuwalinda albino na tembo? Au mafanikio ya kuiacha nchi na madeni mazito? Au mafanikio ya kuuza gesi ya Mtwara kwa Wachina ili Riz 1 asinyongwe? Au mafanikio ya kujenga lijumba la kifahari Msoga kwa hela za walipa kodi?

Wewe kinakushinda nini kuwalinda, au wewe si Mtanzania? unangoja kila kitu ufanyiwe? wewe kilema?
 
Mtoa mada nakuunga mkono Kwa kuuona baadhi ya mafanikio aliyoyafanya Jk japo yapo mengi uloyaacha kutokana na mda wako kuwa finyu. Lakini unaamin kuwa watanzania wote tunaona na mwenyemacho aambiwi tazama. Nakubaliana na we we kweli mkubwa ni jalala
 
Nakubaliana kuwa JK amefanikiwa ktk mengi nakubaliana na JK kuwa kuna watu wamejipanga kuchafua utawala wake kwa gharama yoyote ile... ILA ... watu wake wa karibu Lukuvi, Pinda, Membe, Sitta ndo wanaomharibia ...vatican inamikono mirefu hope analitambua hilo...
 
Yaani na wewe Mungu akuongezee, umeandika ukweli wa kiwango cha juu sana. Viva Kikwete Viva.
 
Mtoa mada nakuunga mkono Kwa kuuona baadhi ya mafanikio aliyoyafanya Jk japo yapo mengi uloyaacha kutokana na mda wako kuwa finyu. Lakini unaamin kuwa watanzania wote tunaona na mwenyemacho aambiwi tazama. Nakubaliana na we we kweli mkubwa ni jalala

Hata Yesu masihi alikataliwa kwao pamoja na wema wote aliosafanyia mayahudi!. Kikwete anakataliwa kwa mema yake na kwa uzalendo wake, hakika tutamkumbuka!. Na hakika he is the African shining star of the moment!
 
Yaani na wewe Mungu akuongezee, umeandika ukweli wa kiwango cha juu sana. Viva Kikwete Viva.

Hakuna cha maana alichofanya. uchumi umeshuka. maisha magumu. gharama za vyakula juu. ubadhirifu sana. escrow. ufisadi. yani shiidaaaa
 
Umesahau pia mafanikio katika mauaji ya albino, mauaji ya tembo wetu kutoka 55,000 hadi 13,000, kushamiri kwa madawa ya kulevya, rushwa na ufisadi uliokubuhu kama escrow na richmond, utekaji na uteswaji wa wanaodai haki zao kama kina Dr. Ulimboka.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hata mwaka wa biashara kimafanikio unafananishwa na uliopita. Itakuwa nchi?

Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?

Hatuko katika mwaka wa biashara hapa maana ulitaka twende kwenye trends hapo ndipo utakapokuta unayetaka kumsifia ni bure maana kwenye fiscal development amekuwa failure
 
Back
Top Bottom