ifa96
JF-Expert Member
- Jul 25, 2014
- 435
- 222
Wakuu,
Mkuu wa kaya leo yupo Kilombero Mahenge,kesho atakuwa Ifakara kuzindua ujenzi wa daraja la mto Kilombero.
Mishemishe zilzokuwepo hapa sio mchezo, mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya mkurugenzi makada wanapitapita NAWAONA MAAFISA USALAMA KAMA 10.
Ninachojiuliza je, hizi pilka za polisi wilaya zote na mkoa pamoja na msafara wa magari yasiyopungua 50 fedha za wafuja jasho ndio zinatumika?
========
Rais azindua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Kilombero
Mkuu wa kaya leo yupo Kilombero Mahenge,kesho atakuwa Ifakara kuzindua ujenzi wa daraja la mto Kilombero.
Mishemishe zilzokuwepo hapa sio mchezo, mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya mkurugenzi makada wanapitapita NAWAONA MAAFISA USALAMA KAMA 10.
Ninachojiuliza je, hizi pilka za polisi wilaya zote na mkoa pamoja na msafara wa magari yasiyopungua 50 fedha za wafuja jasho ndio zinatumika?
========
Rais azindua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Kilombero
Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.PICHA NA IKULU
Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri akifuatiwa na Mama Salma Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu madawati mapya ya shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani wa Morogoro Agosti 20, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani Morogoro
KABLA YA UZINDUZI