Jakaya Kikwete ndani ya Ifakara

Jakaya Kikwete ndani ya Ifakara

mkuu ndio mara ya kwanza kuona msafara wa kiongozi mkuu wa nchi?? ama ulitaka aje kwa baiskeli ili uje na thread nyingine ya kumkashifu, au asiwe na ulinzi ili upate nafasi ya kurusha mawe kwa manati yako kwa chuki zako binafsi kwa mamlaka ya nchi, pole kijana, wewe ni wa kuogopwa sana
msamehe bure mkuu,kijana njaa kali,kazi hamna,frustration kibao.
 
Kaka tukutane hapa Malale maendeleo baadae tutafakari ujio wa raisi huku kwetu kama una faida yoyote ya msingi

Poa mkuu kwa sasa tupo mwendo mdundo 2najadil ujio wa huyu vasco dagama
 
Mkuu Elungata we na wewe gamba nn? Mbona unamtetea sana huyu vasco dagama?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu SAUTI YAKO upande wa barabara ya ifa to mlimba ujenz wa kiwango cha lam ushaanza kuhusu umeme mkuu vijj vya udagaj chita ikule pamoja na mngeta viko kwenye mpango wa
kupokea umeme wa kutoka kians

mkuu acha utani mimi nipo maeneo ya huku chita lakini hakuna dalili yoyote ya lami wala kiwango cha kokoto
 
Last edited by a moderator:
Hivi unajua Rais hatumii punda?
Mkubwa, Jakaya hatembelei Punda, anakwenda kwa kutumia ndege. Lakini jana alikuwa Dodoma kwenye kikao cha CC na aliruka kutoka Dodoma saa 12 jioni kuelekea Dar. Mi niko Dodoma na nilishuhudia hili ninalolisema. Haya hata kama ndege ingeweza kutua Morogoro, uwanja huo hauna taa na muda alioruka huku lazima huko angefika usiku. Tazama uzi wako umeurusha saa ngapi ndio utoe mapovu humu jamvini
 
likamilike wapi! tayari bil18 zimeshatambaa na kazi iliyofanyika ni kusogeza crane tu!

Hotuba yake mi hata cjaielewa mkuu naona hana jipya zaid ya kutoka pov t
 
likamilike wapi! tayari bil18 zimeshatambaa na kazi iliyofanyika ni kusogeza crane tu!

wacha bana na zile tetesi za kandarasi mchina kujinyonga kwa kuharibu kazi ni za kweli?
 
Wakuu naona vasco dagam ashaondoka,vilaza wake watapumua sasa manake tangu juz wanakesha
 
mkuu acha utani mimi nipo maeneo ya huku chita lakini hakuna dalili yoyote ya lami wala kiwango cha kokoto

Kauli yake aliyo itoa leo akiwa Kibaoni, amesema barabara ya Ifakara - Mlimba itajengwa kwa kiwango cha lami kuanzia Ifakara mpaka Mungeta, na sehemu itakayo baki itajengwa kwa kiwango cha Kokoto na itapitika mwaka mzima. Sasa kama ni kweli au porojo mimi sijui, ila kwa ujenzi unao endelea kuanzia Lumemo, mpaka Idete ninaona makaravati yananyanyuliwa juu sana jambo linalo tia matumaini Chita tuombe tu barabara iwe inapitika muda wote.
 
​
Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.​
PICHA NA IKULU ​
​

Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.

​
​
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais)​
​

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)


​
​

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri akifuatiwa na Mama Salma Kikwete


​
​
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
​

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro


​
​

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu madawati mapya ya shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani wa Morogoro Agosti 20, 2014


​
​

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani Morogoro


KABLA YA UZINDUZI
UJENZI+WA+DARAJA+LA+MUDA+MTO+KILOMBERO..JPG
DARAJA+LA+MUDA+KILOMBERO..JPG

03++Kilombero+River.jpg

​
 
Big up, JK.

Kwa kweli watu walipata shida sana maana ikishafika saa 1 huwezi kwenda wilaya nyingine...

Kwa hili na mambo mengi JK utakumbukwa saaaaaana.
 
hongera. sana mh: jk tulianza na mungu tutamaliza mungu. wene wivuuuu .......
 
Hongera CCM mmetekeleza ahadi zenu kwa hilo sifa ziwaendee wote hususan Mhe. Rais wetu mpendwa
 
Back
Top Bottom