Jaji Warioba Kujiuzulu?

Jaji Warioba Kujiuzulu?

Status
Not open for further replies.
Kama ni Kweli basi Huyo mzee mjanja sana, atakuwa amenusa tetesi kuwa Kikwete amesha saini mswaada uliopitishwa na Bunge.

Warioba ameshavuna 'mpunga' wa kutosha na muda wa tume kuendelea kufanyakazi uko ukingoni kwa kuwa sheria ya bunge iliyopiitishwa inaondoa uwepo wa tume baada ya bunge la katiba kuanza.
Warioba anatafuta heshima tu kwa sasa...
 
Mkuu, huyu B. G. TANGAWI anastahili ban ya mwezi nzima kwa kutuletea habari za uzushi

Lizaboni, mbona una haraka? wan-ban kwa lipi? tulia taarifa tutakuletea hapa hapa usiwe na wasi wasi bwana, mimi sio CHadema wala CCm ndo maana nipo huru, Press ipo na nitakujulisha!
 
ngoja tuone, manake najua magamba ni wagumu sana kuachia ngazi, ila huyo mzee anaonekana kama vile sio gamba, tabia zake na za magamba kama tofauti
 
ikiwa hii tarifa siyo ya kweli sijui mkuu tukueleweje ni hivi juzi tu kunamtu alizusha kuwa baadhi ya wajumbe wanataka kujiudhuru lakini warioba akaja kukataa.
 
Pole mzee wangu bora maana CCM kupitia Bulembo wamekusema vibaya

Na MAJOR DOMO wake naye alishapayuka hapa JF!

W. J. Malecela27th September 2013 06:44
#1 ​
JF Senior Expert Member
verified.png
Array


Join Date : 15th March 2009
Posts : 5,078
Rep Power : 6130
Likes Received2248
Likes Given1858​


[h=2]
icon1.png
Ni Wakati Muafaka Now kwa Tume ya Katiba Kuondoka!!;- They Should Go Now!![/h]
- Nimeshitushwa sana na vitisho kutoka kwa Tume ya Katiba kwamba eti watajiuzulu iwapo matakwa yao ya kututengenezea Katiba mpya hayatakubaliwa, well;- nilisema toka siku ya kwanza Tume hiyo ilipotoa the so called "Rasimu ya Katiba Mpya" kwamba ilitakiwa siku ile ile wote waondoke. Kwa sababu mimi sijawahi kuona Tume ya kuandika maoni tu ya Katiba inavyojipachika madaraka makubwa kama tume hii, Mwenyekiti wao alikuwa anaongea kama vile amepewa kazi ya kutengeneza katiba wakati ukweli ni kwamba kazi yao ilikuwa ni kusikiliza tu maoni ya wananchi na kuyaandika chini na kuyakabidhi kwa Taifa tuyafanyie kazi wenyewe kwa kutumia Bunge letu la Taifa na sio anything else!

- Naomba kusema tena kwenye Katiba mpya tunaongelea Taifa letu wote sio la mtu mmoja, Tume ya Katiba wanatakiwa kuelewa kwamba wanatakiwa kujiuzulu kwanza kutoka kwenye kamati ndio waanze kudai madai yao kuhusu Katiba, tumewashuhudia wakipigana sana na Wananchi kwenye kuwasikiliza wakijaribu kila wanaloweza kulazimisha mawazo yao yawe ya wananchi ambayo yalikuwa ni makosa makubwa sana sio tu politically bali hata legally ninaamini walikuwa wanavunja kiapo chao cha kukusanya tu maoni ya wananchi na sio kuyatengeneza kama walivyofanya.

- Binafsi ninaamini kazi yao sasa imekwisha, waondoke ili kutupa nafasi Taifa kujadili tunataka nini. CCM ndio chama Tawala kinchoshika Dola na kukubalika na wananchi wengi kwa mujibu wa kura za uchaguzi wa mwisho uliopita so hakuhitaji kuwa na na hata majadiliano kwamba CCM ndio wenye upper hand katika kutengeneza katiba mpya kwa sababu ndicho chama kinachokubalika na wananchi wengi uthibitisho huo upo wazi kwenye idadi ya Wabunge ambapo CCM ina Wabunge 280 Chadema wana Wabunge 46 tu,

- I mean kwa political standards za Dunia maana yake ni kwamba Tanzania hakuna serious Upinzani kabisa na hata uchaguzi wa mwisho haukuwa na Competition rather than CCM against CCM itself. Tume ya Katiba wacheni kututisha na maneno maneno mengi hewa, hiyo nguvu ya kutuamulia Katiba mpya mmepewa na nani? Huu ni wakati muafaka mkaondoka kwa amani, tupeni maoni mliyokusanya halafu muondoke now!!, then mpige makelele yenu ya binafsi mkiwa nje ya kamati hiyo inakubalika kisheria sio sasa.

Le Mutuz on my way to Lushoto.​


 
Kwa nini ajiuzulu ? Kuna sababu zipi za msingi zipelekee yeye ajiuzulu ? Na kwa nini alikubali hii kazi in the first place ? kwani hakujua ina changamoto zake ? Apambane tuu, vinginevyo arudishe kodi zetu tumpe mtu mwingine hii kazi.

Ila sii ni tetesi tu ? Au ndio tunapima speed ya upepo ?

Respect !!!
 
Kama ni Kweli basi Huyo mzee mjanja sana, atakuwa amenusa tetesi kuwa Kikwete amesha saini mswaada uliopitishwa na Bunge.

Warioba ameshavuna 'mpunga' wa kutosha na muda wa tume kuendelea kufanyakazi uko ukingoni kwa kuwa sheria ya bunge iliyopiitishwa inaondoa uwepo wa tume baada ya bunge la katiba kuanza.
Warioba anatafuta heshima tu kwa sasa...

ni upuuzi kuongelea pesa kwa Warioba! Ushauri wa kisheria tu ofisini kwake ukienda unamlipa zaidi ya laki 4 kwa saa! Pia ana malipo ya kiserikali kama mstaafu na tena hata bungeni hayapiti. Acha kupotosha
 
Naamini atakuwa anamjibu Bulembo, moja ya viongozi vilaza kabisa katika CCM
 
Akifanya hivyo nitamuona mtu wa ajabu sana... Nionavyo mimi mchakato wa katiba TZ ndio mchakato "mpole" zaidi ikilinganishwa na nchi kadhaa zinazoendelea zilizoandika katiba mpya miaka ya karibuni. Siamini kama Warioba alitegemea process rahisi kuliko hii siku anakula kiapo...
 
Huku kwetu jamaa wameleta ngiri leo mbona hafanani na warioba aisee...dah..ila jamaa ana masihara sana.
 
Ikitokea warioba akajiudhuru naacha kuchangia mada za siasa kwani najua ni kitu kisichowezekana pia hakuna sababu ya kufanya hivyo.
 
Warioba anataka serikali tatu or no deal.

Nomba nikusahihihishe wananchi waliotoa maoni wanataka serikali mbili sio Warioba kwani yeye anawakilisha tuu aliyoyakusanya kutoka kwa wananchi.
 
Ikitokea warioba akajiudhuru naacha kuchangia mada za siasa kwani najua ni kitu kisichowezekana pia hakuna sababu ya kufanya hivyo.

Utaacha au utalogin kwa jina lingine'!!!!?
 
Wakati wa kutishiana nyau ulishaisha kama warioba angetaka kuondoka angeondoka tu bila hata shida kwani mpaka akajitangaze.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom