Dkt. Mussa: Warioba Tatizo Kuu la Watanzania

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,147
Reaction score
891
Dkt. Khamis Mussa, mchambuzi wa masuala ya siasa, amemtaja Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa ni “tatizo kuu la matatizo ya Watanzania”, akidai kuwa sehemu kubwa ya changamoto zinazohusu Katiba nchini zinatokana na nafasi na maamuzi ya Warioba katika vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania.

Akizungumza leo Ijumaa, Septemba 4, 2026, Dkt. Mussa amesema Warioba ndiye aliyeandika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akidai kuwa Katiba hiyo ilimpa Rais madaraka makubwa kiasi kwamba hata Mwalimu Julius Nyerere alilazimika kuifanyia marekebisho mwaka 1982 na 1984. Amesema kinachomshangaza ni baadhi ya wakosoaji wa Katiba hiyo kumtaja Warioba kama shujaa licha ya kuwa ndiye aliyeshiriki kuiandaa.

Dkt. Mussa pia amemlaumu Warioba kwa kile alichokiita kushindwa kutumia nafasi aliyopewa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akidai kuwa mapendekezo ya Serikali Tatu yaliyotokana na Tume hiyo ndiyo yaliyoibua mvutano mkubwa katika Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014 na hatimaye kuzuia kupatikana kwa Katiba Mpya. Kwa mujibu wa Dkt. Mussa, kama pendekezo hilo lisingekuwepo, huenda Tanzania ingekuwa tayari imepata Katiba Mpya.

Akizungumzia mwenendo wa Warioba baada ya kustaafu, Dkt. Mussa amesema tofauti na viongozi wastaafu kama Cleopa Msuya na Benjamin Mkapa ambao, kwa mujibu wake, walikuwa wakitoa ushauri kwa viongozi walioko madarakani moja kwa moja, Warioba amekuwa akizungumza kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Amehusisha kauli za Warioba kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025 na madai ya mgawanyiko ndani ya Jeshi la Polisi na kusema kuwa kiongozi mwenye uzoefu kama Warioba alipaswa kutumia nafasi yake kumshauri Rais moja kwa moja badala ya kulalamika hadharani.
HRXOdGqa0AAvCqW.jpg
 
Dkt. Khamis Mussa, mchambuzi wa masuala ya siasa, amemtaja Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa ni “tatizo kuu la matatizo ya Watanzania”, akidai kuwa sehemu kubwa ya changamoto zinazohusu Katiba nchini zinatokana na nafasi na maamuzi ya Warioba katika vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania.

Akizungumza leo Ijumaa, Septemba 4, 2026, Dkt. Mussa amesema Warioba ndiye aliyeandika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akidai kuwa Katiba hiyo ilimpa Rais madaraka makubwa kiasi kwamba hata Mwalimu Julius Nyerere alilazimika kuifanyia marekebisho mwaka 1982 na 1984. Amesema kinachomshangaza ni baadhi ya wakosoaji wa Katiba hiyo kumtaja Warioba kama shujaa licha ya kuwa ndiye aliyeshiriki kuiandaa.

Dkt. Mussa pia amemlaumu Warioba kwa kile alichokiita kushindwa kutumia nafasi aliyopewa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akidai kuwa mapendekezo ya Serikali Tatu yaliyotokana na Tume hiyo ndiyo yaliyoibua mvutano mkubwa katika Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014 na hatimaye kuzuia kupatikana kwa Katiba Mpya. Kwa mujibu wa Dkt. Mussa, kama pendekezo hilo lisingekuwepo, huenda Tanzania ingekuwa tayari imepata Katiba Mpya.

Akizungumzia mwenendo wa Warioba baada ya kustaafu, Dkt. Mussa amesema tofauti na viongozi wastaafu kama Cleopa Msuya na Benjamin Mkapa ambao, kwa mujibu wake, walikuwa wakitoa ushauri kwa viongozi walioko madarakani moja kwa moja, Warioba amekuwa akizungumza kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Amehusisha kauli za Warioba kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025 na madai ya mgawanyiko ndani ya Jeshi la Polisi na kusema kuwa kiongozi mwenye uzoefu kama Warioba alipaswa kutumia nafasi yake kumshauri Rais moja kwa moja badala ya kulalamika hadharani.View attachment 3663247
Dr.Mussa yupo sahihi 100%,

mzee wetu huyo wa heshima ndio chimbiko la mapungufu machache ya katiba na kwakweli amekua changamoto zaidi kuelekea mchakato wa katiba mpya:KasugaYeah:
 
Dkt. Khamis Mussa unayejiita Dr,nina uhakika , huo uDr unaojiita hauna tofauti na ule wa Saa100.
Matatizo makuu tuliyo nayo ni
1. CCM na uongozi wake
2. CCM kuwa chama dola na sio Chama cha siasa
3. Muungano mbovu kuwahi kutokea
4. Simba na yanga
5. Dini
 
Mzee Warioba ndiye mtu aliyekuwa anaweza kuwapinga Nyerere na Sokoine walipokuwa wanazidisha ubabe na kwenda nje ya sheria.

Kuna mtu aliachiwa na mahakama, Nyerere akaagiza akamatwe tena ashitakiwe upya, kwa kosa lile lile. Warioba akamwambia Nyerere kuwa hatuwezi kufanya kitu hicho ni kinyume na sheria, ni double jeopardy. Nyerere akaishia kulalamika chinichini akimwambia balozi Opanga kwamba rafiki yake balozi Opanga, Warioba anamdhibiti yeye Nyerere kwa sheria, lakini Nyerere ikibidi akubali kushindwa kwa sababu hiyo ilikiwa ni sheria.

Warioba hakumuogopa Nyerere, alimuambia Mwalimu hapa utavunja sheria. Kwa namna ambayo wanasheria wakuu wa serikali wengi wasingeweza.

Kwenye uzinduzi wa kitabu cha Sokoine Warioba alielezea jinsi Sokoine alivyotaka kuondoa mambo ya kikatiba katika vita dhidi ya wahujumu uchumi, na Warioba alivyomkatalia mpaka Sokoine akaenda kwa rais Nyerere kumshitaji Warioba, wakapata some compromise, ila Sokoine hakupata kike alichokitaka originally.

Sokoine alitaka kufuta haki ya kikatiba ya watu kupata dhamana, pamoja na haki nyingine za kikatiba. Warioba akakataa, akatishia kujiuzulu . Nyerere akawasawazisha kwa kuondoa vipengele fulani ambavyo Sokoine alivitaka na Warioba hakuvitaka, na kuacha vingine. Kukawa na compromise.

Warioba stood up for the rule of law.

1977 chama kilishika hatamu, katiba imeandikwa na kina Msekwa more than Warioba, Warioba ndiyo kwanza alikuwa anaingia kuwa AG hakuwa na nguvu ya kubishia mabadiliko ya katiba kihivyo, huu mzigo wa jamii nzima msimtwishe mtu mmoja.
 
Dkt. Khamis Mussa, mchambuzi wa masuala ya siasa, amemtaja Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa ni “tatizo kuu la matatizo ya Watanzania”, akidai kuwa sehemu kubwa ya changamoto zinazohusu Katiba nchini zinatokana na nafasi na maamuzi ya Warioba katika vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania.

Akizungumza leo Ijumaa, Septemba 4, 2026, Dkt. Mussa amesema Warioba ndiye aliyeandika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akidai kuwa Katiba hiyo ilimpa Rais madaraka makubwa kiasi kwamba hata Mwalimu Julius Nyerere alilazimika kuifanyia marekebisho mwaka 1982 na 1984. Amesema kinachomshangaza ni baadhi ya wakosoaji wa Katiba hiyo kumtaja Warioba kama shujaa licha ya kuwa ndiye aliyeshiriki kuiandaa.

Dkt. Mussa pia amemlaumu Warioba kwa kile alichokiita kushindwa kutumia nafasi aliyopewa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akidai kuwa mapendekezo ya Serikali Tatu yaliyotokana na Tume hiyo ndiyo yaliyoibua mvutano mkubwa katika Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014 na hatimaye kuzuia kupatikana kwa Katiba Mpya. Kwa mujibu wa Dkt. Mussa, kama pendekezo hilo lisingekuwepo, huenda Tanzania ingekuwa tayari imepata Katiba Mpya.

Akizungumzia mwenendo wa Warioba baada ya kustaafu, Dkt. Mussa amesema tofauti na viongozi wastaafu kama Cleopa Msuya na Benjamin Mkapa ambao, kwa mujibu wake, walikuwa wakitoa ushauri kwa viongozi walioko madarakani moja kwa moja, Warioba amekuwa akizungumza kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Amehusisha kauli za Warioba kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025 na madai ya mgawanyiko ndani ya Jeshi la Polisi na kusema kuwa kiongozi mwenye uzoefu kama Warioba alipaswa kutumia nafasi yake kumshauri Rais moja kwa moja badala ya kulalamika hadharani.View attachment 3663247
Warioba ndio kasabisha barabara ya kutoka Mbezi kwa Yusufu kupitia Mpiji Magohe hadi Bunju isiwekewe lami hadi leo?
Watanzania tunawajua fika maadui zetu, nao ni CCM, katiba ya mwaka 1977 na muungano
 
Mzee Warioba ndiye mtu aliyekuwa anaweza kuwapinga Nyerere na Sokoine walipokuwa wanazidisha ubabe na kwenda nje ya sheria.

Kuna mtu aliachiwa na mahakama, Nyerere akaagiza akamatwe tena ashitakiwe upya, Warioba akamwambia Nyerere kuwa hatuwezi kufanya kitu hicho ni kinyume na sheria, ni double jeopardy. Nyerere akaishia kulalamika chinichini akimwambia balozi Opanga kwamba rafiki yake balozi Opanga, Warioba anamdhibiti yeye Nyerere kwa sheria, lakini Nyerere ikibidi akubali kushindwa kwa sababu hiyo ilikiwa ni sheria.

Warioba hakumuogopa Nyerere, alimuambia Mwalimu hapa utavunja sheria. Kwa namna ambayo wanasheria wakuu wa serikali wengi wasingeweza.

Kwenye uzinduzi wa kitabu cha Sokoine Warioba alielezea jinsi Sokoine alivyotaka kuondoa mambo ya kikatiba katika vita dhidi ya wahujumu uchumi, na Warioba alivyomkatalia mpaka Sokoine akaenda kwa rais Nyerere kumshitaji Warioba, wakapata some compromise, ila Sokoine hakupata kike alichokitaka originally.

Warioba stood up for the rule of law.

1977 chama kilishika hatamu, katiba imeandikwa na kina Msekwa more than Warioba, Warioba ndiyo kwanza alikuwa anaingia kuwa AG hakuwa na nguvu ya kubishia mabadiliko ya katiba kihivyo, huu mzigo wa jamii nzima msimtwishe mtu mmoja.
 
Attachments

  • IMG-20260827-WA0012.jpg
    IMG-20260827-WA0012.jpg
    22.3 KB · Views: 5
Ni kawaida ya uoongozi dhaifu, usioweza kazi, usio na uhalali, kutengeneza mazingaombwe ya kuwachota watu akili zitoke kwenye matatizo yao ya msingi, na kupeleka akili kwenye hayo mazingaombwe.

Hii ni sehemu ya propaganda ambazo zilikuwapo tangu kabla ya enzi za "Circus Maximus" ya Warumi walipotawala watu kwa distractions za "bread and circuses".

The Roman poet Juvenal (Decimus Junius Juvenalis) AD 55 - 128 talked about this in his book Satires X.

This is the circus coming to town.

Maneno "Mazinga Ombwe" yanatokana na kuzinga, maana yake kuficha, kukinda, na ombwe, maana yake utupu.

Yani uongozi ambao ni mtupu, hauna kitu, uko uchi, unatengeneza vi story vya ajabu ajabu kujificha ili utupu wake usionekane, watu waangalie hivyo vi stories vya mazinga ombwe.

Ndiyo hivi vi stories vya Warioba mbaya.
 
Dr.Mussa yupo sahihi 100%,

mzee wetu huyo wa heshima ndio chimbiko la mapungufu machache ya katiba na kwakweli amekua changamoto zaidi kuelekea mchakato wa katiba mpya:KasugaYeah:
Alitimiza wajibu wake, ikabaki wajibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiongozwa na wingi wa Wabunge wa ccm ndio walizuia kuipitsha rasimu ya pili ya Katiba ikakwama Bungeni.
 
Dr.Mussa yupo sahihi 100%,

mzee wetu huyo wa heshima ndio chimbiko la mapungufu machache ya katiba na kwakweli amekua changamoto zaidi kuelekea mchakato wa katiba mpya:KasugaYeah:
Ile rasimu yake iliwatoa jasho mkaona dawa ni kuitengenezea alternative ya kijinga.

Nina mashaka na doctorate ya huyo Dr. wa lumumba.
 
Huyo Dr kakosea kwa sababu katiba sio kitabu cha dini kwa nini miaka yote hiyo hawajafanya marekebisho unamlaumu mtu kwa katiba ya mwaka 1977 wamepita viongozi wangapi wamekaa kimya hawataki hata kuibadilisha huyo Dr atakua wa mchongo mchongo tu.
 
Back
Top Bottom