Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

- Mimi ni Kiongozi wa Taifa nimechaguliwa na Wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa na pia ni Kiongozi wa CCM kata ya Kivukoni, so pole sana mkuu naona huwa husomi sana media za bongo ungejua kwamba mimi sio kama wewe, ha1 ha!

Le Mutuz
"...ungejua kwamba mie sio kama wewe"? Kwani wewe unanijua mimi nani? Sina njaa mzee/kijana kama wewe ambaye tunakufahamu ulivyo. Kama kweli wewe ni kiongozi wa Taifa na unaishia kumshikia jukwaa kwa nyuma Bulembo,basi wewe ni janga huko walipokupa huo uongozi. Nina mashaka na hao wapiga kura kuwa hawakukusikiliza hoja zako ila walikuangalia ukubwa wa Tumbo tuu basi.
 
Watu wote wanaompinga warioba na tume yake ni yale mazezeta...

Tunataka katiba itakayo toa haki kwa chama chochote kutawala ....na kustawi ikiwemo kurudi madarakani pale kitakaposhindwa uchaguzi kama marekani...
Sasa ccm kama chama tawala leo tusifanye kama tuna mkataba wa kutawala milele ....tuteee katiba iandaliwe iwe rafiki ambayo hata leo na kesho chama kikitoka madarakani keshokutwa kirudi...kisijekandamizwa kikafutika ..
Tumeshuhudia Vyama vinatoka madarakani vinafutika kabisa ..hatutaki itokee hapa ..tunataka tuwe kama marekani Vyama viwe vinashindwa na kukubali matokeo vikijuwa katiba inatoa uhuru sawa

- Unaongea ndoto za mwendawazimu tunaongea sasa, CCM ndio chama tawala na ndio chenye mamlaka kisheria ya kuamua katiba iwe vipi sio Chadema wala Warioba. FULL STOP!!

Le Mutuz
 
- Mngeanza kujadili content kwanza, kulia kwamba wanachama wa CCM wamefundishwa maoni ndio kujadili content? ha1 ha! ha! ha!

Le Mutuz
Wewe umekosa busara na hekima; mbona dada zako ni watu makini! Tafadhali badili mwelekeo wa maisha; badala ya kufukuzia posho kupitia safari za Bulembo; nenda Mtera kafanye shughuli ya kuvua samaki zitakulipa na kurudisha heshima miongoni mwa jamii
 
"...ungejua kwamba mie sio kama wewe"? Kwani wewe unanijua mimi nani? Sina njaa mzee/kijana kama wewe ambaye tunakufahamu ulivyo. Kama kweli wewe ni kiongozi wa Taifa na unaishia kumshikia jukwaa kwa nyuma Bulembo,basi wewe ni janga huko walipokupa huo uongozi. Nina mashaka na hao wapiga kura kuwa hawakukusikiliza hoja zako ila walikuangalia ukubwa wa Tumbo tuu basi.

- the bottomline is Warioba hana mamlaka kisheria ya kuamua katiba yetu, poleni sana CCM ndio tumeshinda uchaguzi subiri mwaka 2015 ndio mkishinda mdai katiba mpya ya kwenu na CUF sasa hivi CCM ndio tuna uamuzi wa mwisho kisheria.

Le Mutuz
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wanasiasa wameacha kujadili rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake badala yake wamejikita katika kuijadili Tume yake na Wajumbe.

Kauli ya Jaji Warioba imekuja kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdallah Bulembo mkoani Tanga zilizonukuliwa na ITV na baadhi ya magazeti leo.

Katika taarifa hizo, Bulembo anaelezwa kusema kuwa Tume ya Warioba imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya badala ya kukusanya maoni ya wananchi hao na kuongeza ikiwa Tume au Jaji Warioba anataka kufanya kazi hiyo, basi ajiuzulu kwanza katika Tume.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Warioba, ambaye ameshawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu, amesema kauli hizo ni upotoshaji na kuwa Tume yake ina jukumu la msingi la kutoa elimu kwa umma.

“Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote,” anaelezwa kusema Jaji Warioba wakati akijibu swali la mwandishi mmoja kutoka Star TV aliyeongozana na baadhi ya waandishi wengine kutoka ITV, Channel Ten na Clouds FM.

Kwa mujibu wa Warioba, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao walikuwa ni wajumbe wa Mabaraza hayo walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na Wajumbe wa Tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.

“Sasa anaona (Bw. Bulembo) kuwa kutoa elimu ni dhambi,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Bulembo kutoa kauli kama hizo.

“Nilimsikia Mbeya, Moshi na sasa Tanga akitoa matamshi hayo… kwa kawaida huwa sizungumzii mambo haya, huwa tunayaacha yapite,” alisema na kufafanua kuwa kauli kama hizo zimekuwa zikiwafanya wajumbe wa Tume kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Nilisema katika mkutano wangu na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa, zikiwemo zake (Bulembo),” alisema na kuongeza kuwa, pamoja na kauli hizo, Tume yake inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

“Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu,” anaelezwa kusema.

Jaji Warioba alisema Tume yake siku zote imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida lakini akaongeza kuwa ni vema wananchi na wanasiasa wakajadili rasimu ya katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

“Nadhani wangezungumzia rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu,” amesema Jaji Warioba.

Kuhusu kujiuzulu, Jaji Warioba anaelezwa kusema kuwa haamini kuwa kauli zinazotolewa na Bulembo ni kauli za CCM kwa kuwa CCM haijawahi kuitaka Tume ijiuzulu.

“Sina hakika kama anazungumza kwa niaba ya CCM kwani CCM haijasema tujiuzulu,” anadaiwa kusema.

Imeandikwa na mwandishi wa JF

Kosa analofanya Waryoba ni kuendekeza siasa katika hili. Kitendo cha kujibizana na wanasiasa tayari ni siasa hizo.
 
- Kaiz ya Warioba ilikuwa kukusanya maoni, na kuyakabidhi kwa Taifa sio kutuamulia maoni yawe ya Serikali tatu, maoni yamekusanywa na sasa yatachambuliwa yakiwa kama muswaada.

Le Mutuz

kweli wenye pesa ni tofauti na maskini. Kwa wewe pesa ndo imesoma lakini kichwani peupe kama ngozi ya mama Ana Kilango Malecela.
 
- the bottomline is Warioba hana mamlaka kisheria ya kuamua katiba yetu, poleni sana CCM ndio tumeshinda uchaguzi subiri mwaka 2015 ndio mkishinda mdai katiba mpya ya kwenu na CUF sasa hivi CCM ndio tuna uamuzi wa mwisho kisheria.

Le Mutuz

Nani awape ushindi 2015 hawa majabali ya siasa za maneno.
 
Wewe umekosa busara na hekima; mbona dada zako ni watu makini! Tafadhali badili mwelekeo wa maisha; badala ya kufukuzia posho kupitia safari za Bulembo; nenda Mtera kafanye shughuli ya kuvua samaki zitakulipa na kurudisha heshima miongoni mwa jamii

- Hapa tunaoingea KAtiba mpya sio dada yako wala jamii, ninasema hivi Sheria ipo wazi kwamba CCM ndio wenye uamuzi wa mwisho wa kuamua katiba sio Chadema wala Warioba, Chadema ombeni Katiba mpya iahirishwe mpaka mskihika madaraka, ila kwa sasa Sheria ipo wazi sana kwamba hamna nguvu hata kama warioba akiwasaidia.

Le Mutuz
 
Wewe umekosa busara na hekima; mbona dada zako ni watu makini! Tafadhali badili mwelekeo wa maisha; badala ya kufukuzia posho kupitia safari za Bulembo; nenda Mtera kafanye shughuli ya kuvua samaki zitakulipa na kurudisha heshima miongoni mwa jamii

Le Mutuz anawaweza kweli kweli, huwa hamna hoja za kupambana naye, sijui alikuwa wapi mlikuwa mnapumua, karudi sasa mmeanza kutoa mapovu.
 
Kauli ya Bulembo ni ya kusikitisha. Nilimsikiliza jana kwenye taarifa ya habari ya ITV. Lakini kwa upande mwingine pengine tujishangae wenyewe kwa kutotarajia haya kutoka kwa wanasiasa. Nina hakika Kama tume ya Warioba ingetoa Rasimu inayolingana na mawazo au matakwa yao, sasa hivi tungesikia wanamsifu na kumtaka aendelee kuongea zaidi kwa sababu 'anawakilisha mawazo ya Watanzania'! Hao ndio wanasiasa...
 
- the bottomline is Warioba hana mamlaka kisheria ya kuamua katiba yetu, poleni sana CCM ndio tumeshinda uchaguzi subiri mwaka 2015 ndio mkishinda mdai katiba mpya ya kwenu na CUF sasa hivi CCM ndio tuna uamuzi wa mwisho kisheria.

Le Mutuz

utakuwa umerogwa tu,
 
"...ungejua kwamba mie sio kama wewe"? Kwani wewe unanijua mimi nani? Sina njaa mzee/kijana kama wewe ambaye tunakufahamu ulivyo. Kama kweli wewe ni kiongozi wa Taifa na unaishia kumshikia jukwaa kwa nyuma Bulembo,basi wewe ni janga huko walipokupa huo uongozi. Nina mashaka na hao wapiga kura kuwa hawakukusikiliza hoja zako ila walikuangalia ukubwa wa Tumbo tuu basi.

Kosa lake nini kumfuata Bulembo? Mbona siku zote mko nyuma ya babu yenu SLAA?
 
Kauli ya Bulembo ni ya kusikitisha. Nilimsikiliza jana kwenye taarifa ya habari ya ITV. Lakini kwa upande mwinhine pengine tujishangae wenyewe kwa kutotarajia haya kutoka kwa wanasiasa. Nina hakika Kama tume ya Warioba ingetoa Rasimu inayolingana na mawazo au matakwa yao, sasa hivi tungesikia wanamsifu na kumtaka aendelee kuongea zaidi kwa sababu 'anawakilisha mawazo ya Watanzania'! Hao ndio wanasiasa...

- Wakuwasikitikia hapa ni Chadema na Warioba kwa kutaka kutuamulia katiba wakati sheria ya sasa ipo wazi kwamba ni CCM tu ndio wenye uamuzi wa mwisho wa katiba mpya.

Le Mutuz
 
- Rasimu haijadiliki tena ndio maana Chadema na CUF wanasema Rais asisaini ili iendelee kujadiliwa naona wewe ndio unahitaji kusoma tena katiba.

Le Mutuz

Duh! Mgumu sana kuelewa! Kumbe ndo unachofikiri siku zote? Kuwa Rais akisaini huu mswada wa kuratibu process ya kupata katiba mpya ndo atakuwa amesaini kupitisha rasimu ya katiba mpya? Hata siamini mtu wa nafasi kama yako unaweza kuwa misinformed kiasi hiki! No wonder arguments zako kwenye thread hii ziko kivichekesho chekesho. Nakushauri ufatilie kidogo process nzima ya katiba mpya, ilipoanza, ilipofikia, na hatua zinazofata ili tuwe na uelewa sawa, otherwise hakuna kitu hapo
 
- I am well informed kwamba Warioba hana mamlaka kisheria kuamua katiba ni kelele za mlango tu, mengine keep it siyahitaji!!

Le Mutuz
 
Back
Top Bottom