Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 8,938
- 25,282
Jaji Mkuu mstaafu Mh. Barnabas Albert Samatta ameongelea ongezeko la uvunjifu wa haki za msingi za binadamu nchini Tanzania kuliko kipindi kingine chochote.
Amesema kuwa hivi sasa imekuwa ni kawaida kuona mtu akikamatwa na vyombo vya ulinzi na kuhukumiwa kwa tuhuma zisizokuwa na hoja yoyote ya msingi. Amesema hayo katika maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi ya kupigania haki za binadamu LHRC. Jaji Samatta amesisitiza umuhimu mkubwa wa taasisi hiyo kuendelea kufanya kazi nchini Tanzania hasa katika kipindi hiki.
Source: