Jaji mstaafu Mark Bomani naye atoa mpya..

huwezi kujua kwa sababu uko ndani ya 'box' la dr slaa hivyo uwezo wa kufikiri umeisha. try to get out of the box and think objectively as a learned brother
Na wewe unaweza chomoka kidogo kwenye box la Kikwete ili ufikiri na kuandika kitu cha kueleweka?
 
Judge Bomani karudia nilichosema hapa kabla, huwezi kusema humtambui rais wakati unahudhuria vikao vya bunge ambalo sehemu yake ni rais.

Of course Judge Bomani ni CCM na hawezi kuwa impartial, kwa hiyo mchukulie si kama neutral observer, bali msemaji wa CCM. Lakini hata kama maneno haya yangesemwa na Makamba Katibu Mkuu wa CCM ambaye kazi yake ni kutetea CCM, hukatai maneno yake outright. Point anayo Judge.

Huwezi kusema baniani mbaya, kiatu chake dawa. Bunge la rais Kikwete (bunge linamtambua Kikwete kama sehemu yake) mnahudhuria, mnatunga sheria ambazo zitaenda kupigwa sahihi na Kikwete kama rais, lakini rais Kikwete hamumtambui, what kind of BS is this ?
 
Katika gazeti la leo la Mtanzania limetuhabarisha ya kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani amehoji kuhusu Dr. Slaa kukataa kuyatambua matokeo ya kura ya Uraisi huku akiyatambua yale ya wabunge na madiwani...............

Tukumbuke kwanza Jaji huyu amekuwa akinufaika na teuzi nyingi mbalimbali za CCM na ndiyo maana anaona kuna uhaja wa kujitokeza kutetea wale wanaompa ulaji wa kudumu......Hivyo ana masilahi mazito ya ubia na serikali kadha wa kadha za CCM ikiwemo hii ya JK inayotuhumiwa kuiba kura za raia wanyonge na kujisimika madarakani isivyo halali na kinyume cha sheria................................

Maoni yangu ni kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani tumpuuze kwa sababu hajajikitisha kujibu hoja ya msingi ya Dr. Slaa ambayo ni matokeo ya kura yaliyotangazwa na NEC yanatofautiana kabisa na yale ambayo yalitangazwa vituoni..........Hivi NEC matokeo waliyoyatangaza waliyatoa wapi?.........au waliyatoa kibindoni tu?....Hii ni hoja ya msingi kabisa ambapo tungelimtegemea kiongozi wa siku nyingi kama Jaji Mstaafu Bomani kuijibu badala ya kurukia kuwa mbabaishaji tu kwa kuishambulia taswira ya haiba ya Dr. Slaa na kuhoji uwezo wake kama kiongozi..........................

Kushindwa kwa jaji huyu kujibu hoja za kimsingi tajwa kunanithibitishia ya kuwa hoja za Dr. Slaa ni za kweli tupu na hazina majibu zaidi ya JK kukiri kuwa yeye siyo Raisi halali aliyechaguliwa na watanzania kulingana na mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania............

Ama kwa hakika Jaji Mstaafu Mark Bomani ametoa mpya hii ya kujidhalilisha machoni mwa jamii......

Huyu Mzee bado anahamu ya kutoa maoni??

The most important thing in your life is to know When to Shut up.
 
akumbushwe tena kuwa kifungu cha katiba namba 41 kinataka raisi awe amechaguliwa na kushinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa (kulingana na version ya kiingereza ya hiyo katiba). Tuna ushahidi wa kutosha kuwa kikwete hakupata idadi hiyo ya kura kwa hiyo hakuchaguliwa kwa mujibu wa katiba, hivyo yeye siyo rais halali wa jamhuri ya tanzania.

Uchaguzi wa rais hauna uhusiano wowote na uchaguzi wa wabunge ingawa wote wanachaguliwa siku moja. Uchaguzi wa wabunge unatawaliwa na vifungu vya katiba namba 77 hadi 79 wakati uchaguzi wa raisi unatawaliwa na kifungu 41. Kwa hiyo tunaweza kuwatambua wabunge bila kumtambua rais na kusiwe na tatizo lolote.

Kumbe uwezo wa bomani katika kutafsiri sheria ni sifuri kweli kweli, inatia shaka sana kwenye umakini wa mashauri aliyoamua wakati wakiwa jaji; inawezekana ndiyo maana tuna majaji wanashindwa kuamua kesi za muhimu kama ile ya mgombea huru kwa sababu uwezo wao wa kuchambua sheria ni kama ulivyo wa jaji bomani. Nina wasi wasi wanazidiwa hata na walimu wa ngumbaru kabisa watu hawa.

safi sana nimeipenda hii,imekaa vizuri ,na hivi ndivyo viongozi wa tz walivyo,wamekuwa wanfiki wakati watanzania wanateseka.
 
Katika gazeti la leo la Mtanzania limetuhabarisha ya kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani amehoji kuhusu Dr. Slaa kukataa kuyatambua matokeo ya kura ya Uraisi huku akiyatambua yale ya wabunge na madiwani...............

Tukumbuke kwanza Jaji huyu amekuwa akinufaika na teuzi nyingi mbalimbali za CCM na ndiyo maana anaona kuna uhaja wa kujitokeza kutetea wale wanaompa ulaji wa kudumu......Hivyo ana masilahi mazito ya ubia na serikali kadha wa kadha za CCM ikiwemo hii ya JK inayotuhumiwa kuiba kura za raia wanyonge na kujisimika madarakani isivyo halali na kinyume cha sheria................................

Maoni yangu ni kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani tumpuuze kwa sababu hajajikitisha kujibu hoja ya msingi ya Dr. Slaa ambayo ni matokeo ya kura yaliyotangazwa na NEC yanatofautiana kabisa na yale ambayo yalitangazwa vituoni..........Hivi NEC matokeo waliyoyatangaza waliyatoa wapi?.........au waliyatoa kibindoni tu?....Hii ni hoja ya msingi kabisa ambapo tungelimtegemea kiongozi wa siku nyingi kama Jaji Mstaafu Bomani kuijibu badala ya kurukia kuwa mbabaishaji tu kwa kuishambulia taswira ya haiba ya Dr. Slaa na kuhoji uwezo wake kama kiongozi..........................

Kushindwa kwa jaji huyu kujibu hoja za kimsingi tajwa kunanithibitishia ya kuwa hoja za Dr. Slaa ni za kweli tupu na hazina majibu zaidi ya JK kukiri kuwa yeye siyo Raisi halali aliyechaguliwa na watanzania kulingana na mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania............

Ama kwa hakika Jaji Mstaafu Mark Bomani ametoa mpya hii ya kujidhalilisha machoni mwa jamii......

Ulipotaja tu Gazeti la Mtanzania basi nikaona sina hoja tena maana lile ni gazeti la udaku halina manufaa tena ya watanzania
 
Akumbushwe tena kuwa kifungu cha katiba namba 41 kinataka raisi awe amechaguliwa na kushinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa (kulingana na version ya kiingereza ya hiyo katiba). Tuna ushahidi wa kutosha kuwa Kikwete hakupata idadi hiyo ya kura kwa hiyo hakuchaguliwa kwa mujibu wa katiba, hivyo yeye siyo rais halali wa jamhuri ya Tanzania.

Uchaguzi wa Rais hauna uhusiano wowote na uchaguzi wa wabunge ingawa wote wanachaguliwa siku moja. Uchaguzi wa wabunge unatawaliwa na vifungu vya katiba namba 77 hadi 79 wakati uchaguzi wa raisi unatawaliwa na kifungu 41. Kwa hiyo tunaweza kuwatambua wabunge bila kumtambua rais na kusiwe na tatizo lolote.

Kumbe uwezo wa Bomani katika kutafsiri sheria ni sifuri kweli kweli, inatia shaka sana kwenye umakini wa mashauri aliyoamua wakati wakiwa jaji; inawezekana ndiyo maana tuna majaji wanashindwa kuamua kesi za muhimu kama ile ya mgombea huru kwa sababu uwezo wao wa kuchambua sheria ni kama ulivyo wa JAJI bomani. Nina wasi wasi wanazidiwa hata na walimu wa ngumbaru kabisa watu hawa.

Mkuu Kichuguu,

Katiba katika sheria 20 ya 1992 Katika kifungu cha 41 (6) "(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote".

Katika kifungu hicho hicho 41 lakini kipengele cha 10 inasema "(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake".

Maana yake ni kwamba kesi imekwisha, tukitaka kushinda lazima tuombe katiba mpya. Hicho kifungu hapo juu kinaonyesha ni jinsi gani kilitengenezwa kulinda CCM kuwa maraisi daima dumu. Tume iwe huru, na hicho kipengele kifutwe.
 
Judge Bomani karudia nilichosema hapa kabla, huwezi kusema humtambui rais wakati unahudhuria vikao vya bunge ambalo sehemu yake ni rais.

Of course Judge Bomani ni CCM na hawezi kuwa impartial, kwa hiyo mchukulie si kama neutral observer, bali msemaji wa CCM. Lakini hata kama maneno haya yangesemwa na Makamba Katibu Mkuu wa CCM ambaye kazi yake ni kutetea CCM, hukatai maneno yake outright. Point anayo Judge.

Huwezi kusema baniani mbaya, kiatu chake dawa. Bunge la rais Kikwete (bunge linamtambua Kikwete kama sehemu yake) mnahudhuria, mnatunga sheria ambazo zitaenda kupigwa sahihi na Kikwete kama rais, lakini rais Kikwete hamumtambui, what kind of BS is this ?
Bandiko hili ni mwarubaini kwa Chadema!
 
Who is Jaji Bomani..? ignore him, old folk, outdated, we are young, energetic, we know the truth, na aluta continua we don't care 101% about him, Bomani mnafiki mkubwa,anajua ukweli kwsbb ya manufaa yake anatetea tumbo lake, alinyamaza wakati JK anawapigia kura Mramba, Chenge, Lowassa, RA, na anajua hawa ni mafisadi, eti anahoji Dr Slaa, HATUDANGANYIKI, these old folks hawasomi nyakati, nasema mnafiki mkubwa mzomeeni huyoooooooooo, aibuuuuuuu, hopeless
 
Kama CHADEMA haimtambui Kikwete kwa nini wabunge wa CHADEMA wamepiga kura kumratify Waziri Mkuu Pinda aliyependekezwa na Kikwete?

Walikuwa wanampigia kura PM aliyependekezwa na nani pale ?

CHADEMA wanamtambua Kikwete, hizi nyingine longolongo, matendo yao hayaonyeshi kwamba hawamtambui.

Don't get me wrong, simtetei Kikwete wala CCM. Na sijapenda habari yote ya NEC kuhodhi matokeo ya uchaguzi mpaka yatangazwe pamoja, na CCM inaweza kuwa imeiba kura, I have no way of disputing these notions outright.

Lakini at the same time, ukiibiwa na kusema humtambui rais huwezi kumpigia kupiga kura katika kuhakiki uteuzi wa PM ambaye kapendekezwa na rais huyu huyu ambaye humtambui. Unapigia kura uteuzi wa nani sasa ?

Slaa/ CHADEMA wanachemsha hapa, kama humtambui rais itisha mgomo nchi nzima, wafanyakazi wa serikali wasiende kazini kwani hakuna rais halali, wabunge wasiende bungeni, mpaka rais halali apatikane.
 
The guy has a point. Kama mnasema uchaguzi haukuwa wa huru na haki. Mbona mnamkubali Mdee, Mnyika halafu mnamkataa Kikwete? au ni masuala ya ruzuku?

I think CCM should replace Chiligati and put somebody who can effectively call your bluffs na hoja zenu za upande mmoja. Its Chadema's way or no way.
Selemani,
Hoja yako haina logic. Mnyika na Mdee walishinda kwa nguvu za umma. Umesahau patashika za Ubungo? Kikwete hakushinda. Ilichukua muda wa siku 5 kuweza kuchakachua matokeo. Na Dr. Slaa anayo matokeo yanayoonyesha kuwa Kikwete hakushinda. Haihusiani na ruzuku. It does not matter whether ccm replaces Chiligati or Makamba. Ukweli utabaki pale pale kuwa NEC ilichakachua kura in favour of Kikwete.
 
Wabunge wa CHADEMA walivyopiga kura za kumhakiki Pinda walipiga kura kuhakiki pendekezo la nani ?
 
Kiranga,
Ni wabunge wangapi wa CHADEMA waliopiga kura kumhakiki Pinda? Sijaona figures.

Hukuona kina Tundu Lissu na Mnyika wamekuwa mashahidi mpaka wakasema karatasi zina serial numbers, na kumpa kasheshe Spika? Ina maana from Chairman Mbowe to Mnyika and Tundu Lissu pamoja na wabunge wengine wa CHADEMA walishuhudia na kushiriki uhakiki wa Pinda kama wanahakiki uteuzi wa nani?

Jamaa wanachemsha big time kwa style hii.
 
Wewe Sombyo ni wachache enlightened ndani ya ccm, you may perfectly prosper for you love the truth na si unafiki!

Mkuu ni vizuri tukirudia kauli ya Profesa Mwesiga Baregu. Unyonge wa watanzania ndio political capital ya CCM. CCM ilipata kura nyingi kwenye maeneo ambayo watu wako hoi, na ambako watu hawana mwamko na elimu. Ambako hawana access ya information, na ambako hawana idea ya nini wanafanyiwa na wanaowachagua. There is a syndrome (forgot how it is called) of a captive to associate himself/herself with captors, this is what majority of Tanzanians are in. Huwezi kuamini ni kwanini watu wanazidi kudunika na kukubali kuwadumisha wanaowadunisha. Ni wazi kuwa sasa hivi hali ya watu kuendelea kuwa hoi inaendelea kuongezeka, na viongozi kuendelea kujinemeesha inaongezeka. Sasa wanajua kuwa siku zinahesabika kwa hiyo watanyonya na kukwapua zaidi.

No wonder watu wamekuwa mawaziri kwa muda mrefu na wengine sasa wanang'an'ganiza wapewe uwaziri, sababu wanajua wanachokitaka.
 
Jaji Bomani, ni mtu anayeheshimika katika jamii yetu na hivyo sio wa kupuuzwa hata kama ametofautiana na msimamo wa Chadema, the same applies to Jaji Warioba, Jaji Mfalila, Salim Salim, Ibrahim Kaduma etc, wale waumini wazuri wa Mwalimu Nyerere.
ukiwa mtu unayeheshimika lazima ulinde heshima yako kwa hili Jaji Bomani amepoteza heshima yake maana hajajaribu hata kujibu swala ambalo Dr Slaa alisema kuwa NEC wamechakachua matokeo yaani sasa maneno yake ni ya kutoa tu kama vile hajui hata sheria kwa maana hiyo heshima yake itaendeleaje na hizo pumba?
 
Mkuu Kichuguu,

Katiba katika sheria 20 ya 1992 Katika kifungu cha 41 (6) "(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote".

Katika kifungu hicho hicho 41 lakini kipengele cha 10 inasema "(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake".

Maana yake ni kwamba kesi imekwisha, tukitaka kushinda lazima tuombe katiba mpya. Hicho kifungu hapo juu kinaonyesha ni jinsi gani kilitengenezwa kulinda CCM kuwa maraisi daima dumu. Tume iwe huru, na hicho kipengele kifutwe.

Mtanganyika, swala hili la sheria hiyo ya 41 linahitaji watu kuliangalia kwa amkini sana badala ya kuliangalia kwa woga. Mimi ningekuwa katika nafasi nzuri nigelichukua mikononi mwangu hadi mahakamani. Nitaeleza kwa nini.

Inawezekana Katiba ilifanyiwa marekebisho kwenye kifungu cha 41(6) kuondoa ulazima wa kupata kura zaid ya nusu ya kura halali zilziopigwa. Tovuti ya bunge haitoi historia nzuri ya kuonyesha mabadiliko ya katiba yetu kama wenzetu wanavyokuwa na 1st amendment, 2nd amendment na vitu kama hivyo. Kopi niliyo nayo ni ile nilyodownload hapa:

http://www.parliament.go.th/parcy/sapa_db/cons_doc/constitutions/data/Tanzania/TanzaniaC.pdf

Hicho kifungu cha 41(6) kinatofautiana na kile ulichonukuu wewe kwa vile pale kinasomeka hivi:

attachment.php

Kifungucha41.JPG

Iwapo kifungu cha 41(6) kilibadilishwa, bado hakuna tatizo sana kwa sababu kutokana na ukweli kuwa Tume imeshaonyesha kuwa haina uhakika na kura halisi walizopata wagombea hadi inabadilisha idadi ya kura katika baadhi ya majimbo kama huko Vunjo, hiyo ni proof ya kutosha kabisa kuwa walitangaza ushindi wa Kikwete bila kuwa na uhakika, na hivyo ushindi wa kikwete hautoshelezi standard yetu ya "beyond reasonable doubts" hasa kwa vile mshindani wake amekataa kukubaliana na ushindi huo. Kwa hali hiyo bado kifungu hicho cha 41(6) hakijatoshelezwa. Sasa basi, kwa vile kifungu cha 41(6) hakijatoshelezwa, ndiyo maana kifungu cha 41(7) hakina nguvu ya kumlinda kikwete tena kwa vile kifungu hicho kina nguvu tu wakati uchaguzi wa Kikwete umetosheleza aya yote ya 41 ikiwa ni pamoja na kifungu cha 41(6).

Kwanza sielewi kwa nini tuna kifungu hicho cha 41(7) kwa vile hakina kazi yoyote. Kinazuia mahakama kufanya uchunguzi kuhuisiana na ushindi wa mtu aliyetangazwa kuwa rais kihalali. Kifungu hiki kinajaza nafasi tu kwa sababu mahakama zetu hazifanyi kazi ya kuchunguza mambo bali zinaamua mambo kulingana na malalamiko yaliyoletwa na walalamikaji. Kifungu hiki hakiiuzuii mahakama kusikiliza malalamiko yanayoletwa mbele yake kuhusiana na ushindi wa mtu aliyetangazwa kuwa rais mradi tu mahakama hiyo isifanye uchunguzi dhidi yake. Malalamiko ya aina hiyo yatakuwa ni malalamiko ya Kikatiba kwa hiyo mahakama haiwezi kujitoa kuyasikiliza; zitasikiliza na kutolea maamuzi kulingana na ushahidi ulipelekwa na pande zote zinazohusika.

Ninaweza kuelewa tu kuwa mahakama zitafanya makusudi kutotekeleza wajibu wake lakini itakuwa ni jambo jema sana kesi hii iingine katika rekodi za kudumu kusaida vizazi vijavyo vitambue kuwa matatizo watakayorithi kutoka kwetu hayakusababishwa na sisi wote bali wachache tu huko mahakamani.

BTW:

Katiba niliyonukuu ni ya mwaka 1997 kama ilivyoidhinishwa na Fisadi chenge hapa:
attachment.php

katiba1.JPG
 
Huyu mzee nilikuwa namheshimu sana lakini kwa kauli hii nimemshusha sana. Sijui ameanza lini kupotoka. Bila shaka ni sababu ya umri.
 
Hukuona kina Tundu Lissu na Mnyika wamekuwa mashahidi mpaka wakasema karatasi zina serial numbers, na kumpa kasheshe Spika? Ina maana from Chairman Mbowe to Mnyika and Tundu Lissu pamoja na wabunge wengine wa CHADEMA walishuhudia na kushiriki uhakiki wa Pinda kama wanahakiki uteuzi wa nani?

Jamaa wanachemsha big time kwa style hii.

Tuweke record sawa hapa. Kwanza kuhusu upitishwaji wa jina la Waziri Mkuu. Wabunge wa CHADEMA walikuwa wanatuma salamu kwa Anna Makinda kwamba akae chonjo, wapo makini katika kuzingatia kanuni na taratibu za bunge, ambazo watazifuata katika kupigania kile kilichowaleta pale bungeni: maslahi ya wananchi na taifa kwa kujumla. nilivyoona katika TV jinsi mijadala ilivyoendelea, CHADEMA ilitimiza lengo lake kwa hali ya juu kabisa. mfano ule utaratibu wa kupitisha mtu anayegombea nafasi katika bunge bila kumuuliza maswali ya msingi, ulionekana kupitwa na wakati. ilichekesha pale Tundu Lissu alipotumia nafasi ya kuuliza maswali mbunge anayegombea kuwakilisha bunge letu katika bunge la SADCC, na akamuuliza swali dogo tu ni nini kirefu cha SADCC. mgombea huyo ambaye awali alipoeleza cv yake alionesha jinsi alivyoshugulika saaana na mambo ya SADCC. lakini alishindwa kueleza kirefu cha SADCC!! hii inaonesha ugonjwa mkubwa sana kwamba mtu anagombea katika jambo ambalo hata hajalifanyia kazi na kulielewa sawasawa.

kwa hiyo basi, uhakiki wao wa taratibu zinazotumika pale bungeni ni halali kabisa kufanya katika mazingira yoyote yale.

pili, CHADEMA wanayo haki ya kuamua jinsi watakavyofanya protest yao. kwa kuwa sheria ni kandamizi, kwamba huruhusiwi kupinga uteuzi wa rais akishatangazwa na tume, ni juu ya chama chochote kuamua kitumie mbinu gani mbadala. hii ni mbinu ya political pressure, ambayo ilimgusa waziri mkuu mteule Pinda, kama uliangalia runinga wakati anatoa neno la shukrani. hilo ndio lilikuwa jambo la kwanza kulizungumzia, jinsi CHADEMA walivyomweka pembeni, akakumbuka bunge lililopita walivyomuunga mkono. hata wakati wa kumpitisha wakati anateuliwa kujaza nafasi ya Lowasa, za kumpinga zilikuwa ni chache zaidi kulinganisha na za sasa. unaweza kusema, japo kura ni za siri, kwamba CHADEMA hawakumpa kura zao. ni kweli haina impact kubwa kwa upande mmoja, lakini the mere fact kwamba inazungumziwa katika duru mbalimbali, na ni mara ya kwanza kutokea kwa msisitizo mkali namna hii katika siasa za Tanzania, ni dalili kwamba ina impact tayari!! protest imefanyika na imeshafanikiwa. suala la wizi wa kura hasa za urais bado litakuwa katika ajenda mbalimbali kitaifa na kimataifa. hata hapa jf bado ni mada moto. mission accomplished!!
 
Katika gazeti la leo la Mtanzania limetuhabarisha ya kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani amehoji kuhusu Dr. Slaa kukataa kuyatambua matokeo ya kura ya Uraisi huku akiyatambua yale ya wabunge na madiwani...............

Tukumbuke kwanza Jaji huyu amekuwa akinufaika na teuzi nyingi mbalimbali za CCM na ndiyo maana anaona kuna uhaja wa kujitokeza kutetea wale wanaompa ulaji wa kudumu......Hivyo ana masilahi mazito ya ubia na serikali kadha wa kadha za CCM ikiwemo hii ya JK inayotuhumiwa kuiba kura za raia wanyonge na kujisimika madarakani isivyo halali na kinyume cha sheria................................

Maoni yangu ni kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani tumpuuze kwa sababu hajajikitisha kujibu hoja ya msingi ya Dr. Slaa ambayo ni matokeo ya kura yaliyotangazwa na NEC yanatofautiana kabisa na yale ambayo yalitangazwa vituoni..........Hivi NEC matokeo waliyoyatangaza waliyatoa wapi?.........au waliyatoa kibindoni tu?....Hii ni hoja ya msingi kabisa ambapo tungelimtegemea kiongozi wa siku nyingi kama Jaji Mstaafu Bomani kuijibu badala ya kurukia kuwa mbabaishaji tu kwa kuishambulia taswira ya haiba ya Dr. Slaa na kuhoji uwezo wake kama kiongozi..........................

Kushindwa kwa jaji huyu kujibu hoja za kimsingi tajwa kunanithibitishia ya kuwa hoja za Dr. Slaa ni za kweli tupu na hazina majibu zaidi ya JK kukiri kuwa yeye siyo Raisi halali aliyechaguliwa na watanzania kulingana na mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania............

Ama kwa hakika Jaji Mstaafu Mark Bomani ametoa mpya hii ya kujidhalilisha machoni mwa jamii......

Huyu ana matatizo kwa sababu yale ya Rais yametangazwa na NEC huku yakitofautiana na yale ya kwenye vituo vya kupigia kura; pili yale ya wabunge na madiwani sheria hiko wazi kwamba mahakama inaweza kuyatengua lakini si ya Rais; tatu ukisoma kitabu cha Mwalimu Nyerere 'Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania' huyu Jaji Mark ndiye aliyepewa kazi ya kuleta muundo wa uchaguzi na uongozi wa nchi, pia nina wasiwasi ndiye aliyependekeza kifungu kinachoua demokrasia na kuhalalisha 'uchakachuaji' wa kura za Urais cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania 41 (7).
 
CHADEMA mwenzenu kesha kiri kwamba walitumia nguvu ya ziada (kuchakachua) kupata urais. Pelekeni mswada wa kubadili Tume ya Uchanguzi (National Electoral Commission) pamoja na Katiba ili 2015 tuwe na tume huru. Mkwere kesha apishwa na hakuna lolote litabadili hali ilivyo ispokuwa Mungu peke yake. Kiungwana tutambue serikali iliyopo na tufanye kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo ili mwaka 2015 mkomboe majimbo zaidi kutoka kwenye nyororo za SiSiEM. Operesheni Sangara imefanya kazi nzuri sana na matokeo yake tumeyaona kule Mwanza na Shinyanga. Anzeni operesheni Pweza au Jodari ili kukomboa mikoa ya pwani.
 
Back
Top Bottom