Jaji mstaafu Mark Bomani naye atoa mpya.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji mstaafu Mark Bomani naye atoa mpya..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 17, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,247
  Trophy Points: 280
  Katika gazeti la leo la Mtanzania limetuhabarisha ya kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani amehoji kuhusu Dr. Slaa kukataa kuyatambua matokeo ya kura ya Uraisi huku akiyatambua yale ya wabunge na madiwani...............

  Tukumbuke kwanza Jaji huyu amekuwa akinufaika na teuzi nyingi mbalimbali za CCM na ndiyo maana anaona kuna uhaja wa kujitokeza kutetea wale wanaompa ulaji wa kudumu......Hivyo ana masilahi mazito ya ubia na serikali kadha wa kadha za CCM ikiwemo hii ya JK inayotuhumiwa kuiba kura za raia wanyonge na kujisimika madarakani isivyo halali na kinyume cha sheria................................

  Maoni yangu ni kuwa Jaji Mstaafu Mark Bomani tumpuuze kwa sababu hajajikitisha kujibu hoja ya msingi ya Dr. Slaa ambayo ni matokeo ya kura yaliyotangazwa na NEC yanatofautiana kabisa na yale ambayo yalitangazwa vituoni..........Hivi NEC matokeo waliyoyatangaza waliyatoa wapi?.........au waliyatoa kibindoni tu?....Hii ni hoja ya msingi kabisa ambapo tungelimtegemea kiongozi wa siku nyingi kama Jaji Mstaafu Bomani kuijibu badala ya kurukia kuwa mbabaishaji tu kwa kuishambulia taswira ya haiba ya Dr. Slaa na kuhoji uwezo wake kama kiongozi..........................

  Kushindwa kwa jaji huyu kujibu hoja za kimsingi tajwa kunanithibitishia ya kuwa hoja za Dr. Slaa ni za kweli tupu na hazina majibu zaidi ya JK kukiri kuwa yeye siyo Raisi halali aliyechaguliwa na watanzania kulingana na mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania............

  Ama kwa hakika Jaji Mstaafu Mark Bomani ametoa mpya hii ya kujidhalilisha machoni mwa jamii......
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umri nao tatizo huyo (dead speaking age). Poor comments.
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ni yaleyaleeeeeee, 'NJAA'. Anavizia cheo anadhani safari hii jk atachukua tena kwenye 'recycle bin'. Thubutu!!!!
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Akumbushwe tena kuwa kifungu cha katiba namba 41 kinataka raisi awe amechaguliwa na kushinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa (kulingana na version ya kiingereza ya hiyo katiba). Tuna ushahidi wa kutosha kuwa Kikwete hakupata idadi hiyo ya kura kwa hiyo hakuchaguliwa kwa mujibu wa katiba, hivyo yeye siyo rais halali wa jamhuri ya Tanzania.

  Uchaguzi wa Rais hauna uhusiano wowote na uchaguzi wa wabunge ingawa wote wanachaguliwa siku moja. Uchaguzi wa wabunge unatawaliwa na vifungu vya katiba namba 77 hadi 79 wakati uchaguzi wa raisi unatawaliwa na kifungu 41. Kwa hiyo tunaweza kuwatambua wabunge bila kumtambua rais na kusiwe na tatizo lolote.

  Kumbe uwezo wa Bomani katika kutafsiri sheria ni sifuri kweli kweli, inatia shaka sana kwenye umakini wa mashauri aliyoamua wakati wakiwa jaji; inawezekana ndiyo maana tuna majaji wanashindwa kuamua kesi za muhimu kama ile ya mgombea huru kwa sababu uwezo wao wa kuchambua sheria ni kama ulivyo wa JAJI bomani. Nina wasi wasi wanazidiwa hata na walimu wa ngumbaru kabisa watu hawa.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nilitegemea ange hoji ilikuwa je JK kuwana nadi Mramba, Chenge kuwa ni watu safi wakati akijua serikali yake inakesi mahakamani na wahusika....
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nashukuru!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  Jaji Bomani, ni mtu anayeheshimika katika jamii yetu na hivyo sio wa kupuuzwa hata kama ametofautiana na msimamo wa Chadema, the same applies to Jaji Warioba, Jaji Mfalila, Salim Salim, Ibrahim Kaduma etc, wale waumini wazuri wa Mwalimu Nyerere.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,247
  Trophy Points: 280
  Lakini heshima lazima uifanyie kazi na hawezi kuwa anatoa kauli za hovyo hovyo na jamii ikaendelea kumsikiliza tu kwa sababu hizo ulizozitoa...............Respect is earned via our actions it is neither demanded nor doled out for free.................
   
 9. M

  MBWEHA Member

  #9
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi vizee mungu angekuwa anavichukua mapema tu vikapumzike milele hakuna wanachokifanya huku duniani,HIKI NI KIZAZI CHA DOT COM wao hawana nafasi bongo zao zinaona mwaka 47 na si 2025:hippie::hippie::hippie::hippie::hippie:
   
 10. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
   
 11. s

  sombyo Member

  #11
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 19, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The time to fool Tanzanians is over. CCM is my party, but I do not like the way we silence others oponios and observations. Sijasoma gazeti hilo ila watanzania tunatakiwa kuheshimiana kwa kauli zetu hasa wazee wetu watulie na mirija yao!
   
 12. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2010
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani ehe JK mwenyewe alikiri katika hotuba yake kuwa wapinzani walimpa changamoto mpaka wakatumia nguvu ya ziada kupata ushindi. basi tumkubalie kaishakili kilichotokea
   
 13. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,324
  Trophy Points: 280
  Good analysis,

  Mark ameishiwa anatafuta jinsi sisiem watamsupport
   
 14. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wewe Sombyo ni wachache enlightened ndani ya ccm, you may perfectly prosper for you love the truth na si unafiki!
   
 15. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwalimi sana.yaani asanteni sana kwa analysis
   
 16. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Kama hayo unayosema ni kweli basi wanazeeka vibaya!!!
   
 17. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #17
  Nov 17, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kweli we ni MBWEHA:smile::smile::smile:
   
 18. M

  Mama PC Member

  #18
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa kweli jamaa ni MBWEHA! Na hayuko peke yake, watajitokeza na wameshajitokeza MBWEHA wengi. Wao wanafaidi ndio maana hawajali. Wamemuweka mtoto wa Mkulima PM na Makinda ili watawale uchumi kwa raha zao wanasahau kuwa Watanzania wamebadilika si wale wale.
   
 19. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pasco, ukumbuke hata pamoja na umahiri wa Nyerere, mwenyewe alitahadharisha kuwa hata yale aliyotenda yeye, viongozi wachambue yale ya maana wayatekeleze, na yale ya kipumbavu
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkulu Pasco, naona umechomekea neno Mwl. Nyerere hapo ili kuhalalisha msimamo wako kuhusiana na swala hili, ukiamini kuwa kumtaja Mwalimu kama mentor wa hao uliowataja kunahalalisha yoyote wanayoiambia jamii ya Watanzania.

  Kwa maoni yangu, ni misimamo kama hii ndiyo inayodumaza Tanzania yetu na bara letu la Afrika. Tuheshimu hili, tuheshimu lile; eti tu kwa vile aliyetamka ni kiongozi wa muda mrefu wa Taifa au ni mmoja wa waasisi. Ndiyo, tunatakiwa kuheshimu mawaidha yao kama vile tu tunavyoheshimiana hapa kwenye kutoa comments zetu jamvini. Lakini hiyo 'tuheshimu' uliyotumia mimi nafikiri ni ile ya 'kivitendo'. Kwa maana kwamba, alichokisema Jaji Bomani ndiyo ukweli na kitekelezwe. Jambo ambalo sikubaliani nalo.

  Nakubaliana nawe kuwa tuwaheshimu na kuwaenzi hawa viongozi wetu. Tena tunawaheshimu kwa marefu na mapana kama wazazi wetu na wanaukoo. Lakini pale wanapotoa maelezo kama miongozo ili jamii itekeleze, hatuna budi kuyapima maelezo hayo katika mizani ya umakini.

  Ni mara nyingi hawa viongozi wetu wanajitokeza tu pale maslahi ya CCM yanapokuwa yanaonekana kubinywa, au pale wanapostaafu. Hali maoni na mapendekezo yao tunayahitaji nyakati zote. Hivi wanakuwa wapi kutoa maelezo yao pale maslahi ya Taifa hili yanapowekwa majaribuni, kama vile kwenye swala la Richmond, EPA, IPTL, Meremeta, n.k.?? Na kila wanapojitokeza basi ni katika kutetea system iliyopo... Sometimes najiuliza, kwa muda wote huu hivi hizi hekima na busara zao ziko wapi katika kuliongoza hili Taifa lililoneemeka kwa maliasiri lakini uduni ndiyo uliotapakaa?!!
   
Loading...