Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 61,023
- 36,865
Mh. Jaji Mkuu,
Kwanza nikupongeze sana sana sana kwa kuchaguliwa kuwa Jaji wetu Mkuu wa Tanzania.
Wakati huu unaingia, tunakumbuka kuwa Jaji wetu mstaafu alikuwa akisisitiza sana sana haki na utawala bora. Mungu ambariki.
Pamoja na haya, wapo baadhi ya mahakimu wanaosumbua sana wananchi, hasa hizi kesi za mirathi. Zimekuwa kama ugonjwa wa kansa. Nimepita hizi mahakama za Arusha na Moshi, ni hatari na zinasikitisha sana.
Mwaka 2018, niliwahi kwenda mahakama moja Mamba Kotela kumsaidia ndugu mmoja. Nikakuta msururu wa malalamiko ya kesi za mirathi zaidi ya 10. Haikuwa rahisi kuwaelewa, ila kwa kweli nilimwambia Mungu atunze wazazi wetu wasife, maana wangejua shida wanazopata watoto wao kwa mahakamani kwa mali walizohangaikia, wasingekubali kufa.
Mh. Jaji Mkuu,
Mfano tu: kuna kesi ilihusu ukoo mmoja wa Mbando. Ilisikitisha sana. Hakimu kapewa kila nyaraka anazohitaji. Wakafika sehemu wanahitaji barua ya mahakama kwenda benki ili watoto wagawiwe fedha za baba zao. Mheshimiwa akaulizia ni shilingi ngapi; toka hapo wakaanza kusumbuliwa: "njooni kesho," "njooni siku fulani." Na kila wakifika wanamwona karani sijui wanafanyaje, wanambiwa hakimu atawapigia. Wameenda miaka miwili kwa ajili ya barua tu.
Nikiwa pale, nikakutana na mmoja wa classmate kwenye hiyo familia. Nikampa mwongozo amwone mtu fulani mkubwa, na apeleke nyaraka zote na kumweleza mwanzo hadi mwisho. Wakaambiwa warudi Januari mwakani kwa hakimu husika. Walipoenda kwa yule ndugu, ikapigwa simu moja tu: "Kuna shida gani na hii kesi?" Akajiuma, mwisho wake walipokuwa wanarudi makwao wakapigiwa simu na hakimu husika: "Njooni wiki hii tarehe fulani." Ilikuwa mwezi Novemba. Walipofika, wakakuta barua tayari na wakaambiwa: "Tusiharibiane kazi, ni suala la kujiweka sawa tu." Wakanishukuru sana.
Kisanga kingine cha aibu nilikutana nacho 2019. Kuna familia, sina uhakika ukoo wao, mahakama ni ile ile, hakimu ni yule yule.
Baba yao alifia Dar, kazikwa Dar. Msimamizi akaenda Moshi kutengeneza cheti cha kifo: kafia Moshi, kazikwa Moshi. Walizaliwa wanne: wawili wa ndoa, wawili wa nje.
Bwana yule (msimamizi) akafanikiwa kuandika muhtasari, akawasilisha kwa hakimu. Watoto wawili wakaomba kusoma alichoandika kabla ya kufanya uharamia wake, akawagomea.
Mwanzo walikubaliana kugawana mali za baba yao sawa kwa wote. Kumbe msimamizi akaandika kuwa kiwanja kimoja ni cha watoto wa nje, vingine vyote wagawane sawa.
Watoto walipoona muhtasari Moshi walishangaa sana. Wakakata rufaa na kumwondoa msimamizi.
Baadaye yule hakimu akaanza kuwasumbua: "Njoo leo, njoo kesho." Nikawashauri wakutane na wakili mmoja Dar. Wakaandika barua kwa Jaji Mfawidhi.
Wakapeleka wiki hiyohiyo, wakaitwa Moshi, wakahojiwa, na hakimu akaondolewa, wakapewa mwingine. Walipewa haki zao na kugawana wote.
Wameshinda upande wa pili, wakakata rufaa, wakatengeneza mkataba kuwa baba yao aliwauzia kile kiwanja 2003. Walipofikisha mahakamani, wakahojiwa, wakajichanganya, wakashindwa kesi.
Wameenda Mahakama ya Wilaya Moshi Mjini. Wanachofanya: waliambiwa hata wakishinda, watawapeleka Moshi mpaka wachoke. Aibu sana sana. Wameenda Moshi... hakimu amesafiri. Wamepewa tarehe nyingine.
Walipofika, wale watoto wa ndoa wamekuta upande wa pili wapo. Katika karatasi ya kesi walioshtaki, badala ya kuandika watoto wanaomshtaki msimamizi, wameandika wanamshtaki baba yao.
Hakimu akasema: "Iko kwenye system, hatuwezi kubadilisha. Iondoleeni mlete upya kesi."
Watoto wa ndoa wakamwomba hakimu: "Tunaomba hukumu ya kesi hii." Akajibu kwa urahisi: "Mimi ndiye nimeamua wawithdraw. Waje upya. Swala la hukumu halipo."
Akaulizwa: "Hizi gharama wanazotumia watoto toka Dar zinalipwaje?" Akajibu: "Simple, mimi ndiye nimeamua. Kila mtu atalipa gharama zake."
Mh. Jaji Mkuu,
Hizi kesi zimekuwa kama ugonjwa wa kansa kila mahakamani, haziponi. Kwa nini?
Embu fatilieni. Kuna wanaochanganya watoto wa marehemu bila hatia.
Binafsi nimewapa ushauri waje wakutane Dar na mawakili, waandike malalamiko yao.
Kuna kesi moja: mama amefiwa na mumewe mwaka wa tano. Wamepeleka nyaraka zote. Wanambiwa: "Njooni kesho kutwa," "njooni siku kadhaa."
Embu tuwasaidie hawa wafiwa. Inasikitisha sana sana.
Mungu ibariki Tanzania.