Jaji Mkuu (Chande) amedanganya umri?

Jaji Mkuu (Chande) amedanganya umri?

umeongea vizuri mkuu lakini tatizo hapa sio ccm bali ni Watanzania (yaani sisi). Hivi fikiria kidogo: Ukija kupanda ndege alafu ukapata ushuhuda wa wazi kuwa rubani hana uwezo wa kutosha unafanyaje? ...au chukulia unaenda kituo cha basi alafu unaona dereva amelewa chakali si unachagua gari nyingine na hata kama umeshalipa si angalau unaonyesha ujasiri wa kudai kurudishiwa nauli yako!?
Sasa sisi tumeshawajua hawa watu na hatufanyi maamuzi yoyote.
Nakumbuka issue ya akliyekuwa mbunge wa Temeke (Kihiyo) ilianza kama masihara lakini ikaishia kujulikana kuwa hakuwahi kusoma DIT/Dar Tech

mkuu njia unayoweza kupendekeza ya wananchi kuchukua hatua apart from ballot box labda ni maandamano,na hawa jamaa kwa sababu wanajua kuwa hawako fair watatumia polisi, na kwa sababu polisi wetu akina Chagonja wenyewe hawako safi watakupiga risasi kesho yake haraka chagonja atatangaza kuwa umepigwa na kitu kizito kilichorushwa na waandamanaji na marehemu alikuwa anakimbilia polisi kupata ulinzi,kwisha.
 
Kama unamtetea Jaji mkuu kudanganya umri ni haki yako lakini si kwa staili hii ndugu yangu.
Kama aliruka madarasa basi isemwe hapa kwamba aliruka kutoka darasa la kwanza hadi la tano, na ilikuwa lini, i mean mwaka gani, sio maneno matupu kama haya unayoandika hapa, muhimu ni kuweka ushahidi tu wa hilo.

Kama ulivyowekwa ushahidi wa kuwa alianza darasa la kwanza na miaka minne!


Mwalimu Nyerere alipata bahati hiyo ya kuruka madarasa na wengine wapo waliopta bahati hiyo. Kinachotafutwa hapa ni ukweli wa umri wake na si kutafuta njia nyingine yeyote nyepesi nyepesi na za uongo uongo ya kujustfy utetezi wako juu ya tuhuma hizi za kughushi umri

Mimi simtetei Chande, ila ninachotetea ni mantiki. Kama wapo walioweza kupata bahati ya kurukishwa madarasa, kwa nini uwezekano huo usiwekwe wazi pia watu wakajadili? Kwa nini watu wang'ang'anie kuwa "alianza darasa la kwanza akiwa na miaka minne" wakati hakuna ushahidi wa hilo?

Hii ya kujadili upande mmoja tu, inadumaza akili.
 
Jitu ni zee lile ila nashangaa kabisa kuwa eti 60 hajafikisha? Kweli achunguzwe huyu na data ziwekwe kweupe. Najua JF ni kisima cha habari zote nyeti na wenye wazazi wao ambao wamekuwa wanasheria na wameshastaafu hebu waulizeni historia ya huyu Jaji Chande ili tupate credibility yake ya kuongoza taasisi adilifu kama hii!!!! Kama ni kweli!!! Tindu Lisu hebu tuulizie wajameni halafu tupatie vijana tuweke humu!!
 
Wana jf ktk hali ya kawaida haiwezekani kwa miaka ile mtu amalize BACHELOR akiwa na 22yrs. hapa hakuna cha kurushwa darasa wala nini CJ wetu amedanganya umri . mambo ya kustaafu ije baadae kwn kwa record ya kosoma mpaka chuo ndo inatoa walakini kwa ss tunao chambua kwa kina.
 
Hebu watu ambao wanataalamu za ualimu na hesabu waje hapa ili tupate majibu sahihi kabla ya kutoa hukumu kama jaji mkuu anatakiwa kustaafu mwaka huu au mwaka ujao. Mfano kama alianza darasa la kwanza akiwa na miaka sita, msingi na sekondari na jeshi miaka 8 + 2 + 1 na chuo kikuu 4, jumla ni 21, toka 1974 mpaka leo ni miaka 38.Anatakiwa kustaafu mwakani maana atakuwa na miaka 60. Hapo ndipo Lissu alipokuwa anapasemea kuhusu tume ya kuteua majaji kama Kenya.
 
Hongera Tundu Lissu nchi nzima inakuogopa wewe hadi wanaamua kufocha mafaili
Kuna kila dalili za ukweli kuhusu hili.
Kuna jamaa wa TISS kanitonya hiyo issue ipo na Usalama wa taifa walikuwa wanatafuta namna ya kuificha sana tangu Lissu alipoanza kufumua uozo wa baadhi ya majaji.
 
Napenda kuwaelewesha wasioelewa jambo hili katiba ya JMT ya mwaka 1977 imetamka waziwazi kwenye 120-(1)kila jaji wa rufani atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini na tano,lakini masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila kuathiri masharti yafuatayo katika ibara hii.

(2)jaji yoyote wa rufani aweza kustaafu kazi ya ujaji wa rufani wakati wowote baada ya kutimiza umri wa miaka sitini ...................

kwahiyo umri wa kustaafu wa hiyari kwa watumishi wengine wa umma(pamoja na majaji wasio wa rufani) ni miaka 55,kwa majaji wa rufani umri wa hiyari wa kustaafu ni miaka 60,kwa watumishi wengine wa umma(pamoja na majaji wasio wa rufani) umri wa lazima wa kustaafu ni miaka 60,kwa majaji wa rufani umri wa lazima wa kustaafu ni miaka 65.

Jaji mkuu pia ni jaji wa rufani na kama amezaliwa 1952 basi atastaafu mwaka 2017.
 
Ataficha miaka ,lakini uso hautauficha utazidi kumporomoka tu na atazidi kuonekana babu,si mashavu yameshaanza kulegea tayari muda si mrefu atakuwa kama babu mla tambuu
 
Nilipoleta Uzi kuhusu Utata wa Umri wa Jaji Mkuu, sikuwa na shaka kuwa sheria inasema ajiuzulu akiwa na miaka 65. Tatizo kubwa katika mjadala wote tangu jana, ni baadhi ya wachunguzi wakiwemo wa Idara yake kusema kuwa alizaliwa 4/9/1949, lakini kutokana sababu ambazo bado hazijawa wazi, wakati jaji Mkuu Augustino Ramadhani anastaafu, kuna Jaji Mwingine aliarifiwa kuwa angekuwa Jaji Mkuu. Haikujulikana ni kwa sababu zipi, kwa ushauri wa ndugu yake, Rashid Othman, Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, ilibadilishwa ghafla, akateuliwa Jaji Mohamed Othman Chande, na tarehe ikawa 1/1/1952. Utata ulianzia hapa, kama alizaliwa mwaka 1952, na kusoma hadi kumaliza Chuo Kikuu akiwa na miaka 22 mwaka 1974, ukikokotoa vema ikaonena kuwa jaji Mkuu alianza shule akiwa na miaka minne. hofu ikaongezeka baada ya kuonekana kuwa Wenakae wote waliosoma naye darasa moja wanastaafu 2013, iweje sasa kustaafu kwake kuwe 2017? Iweje taarifa zake zikawa siri kuna nini kinafichwa? Je Ndugu yake ambaye ni Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa haionekani kuwa kulikuwa na Mgongano wa kimaslahi katika kumteua mdogo wake baada ya kumshauri Rais kama katiba inavyoelekeza. Huu ndio Mjadala, watu wajitokeze ili tusiingize nchi katika Historia ya Kughushi hadi Umri wa jaji Mkuu. Na kama amedanganya Umri ni kwa ajili ya nini?.......... mwaga jamvini.............
 
Hakuna marefu yasiyokua na ncha

Mola aniweke hai hadi 2016 nione kama ataendelea au la
 
Ataficha miaka ,lakini uso hautauficha utazidi kumporomoka tu na atazidi kuonekana babu,si mashavu yameshaanza kulegea tayari muda si mrefu atakuwa kama babu mla tambuu

.
Unaweza kujificha unapozini lakini huwezi kujificha kuugua ukimwi ulioupata kifichi.
.
 
itafikia wakati atakuwa kama mugabe na wasirra atakuwa anasinzia kazini na kusahau maofisa wa ofisi yake, please mr judge go back to the reality
 
jamani nyosheni maelezo kuwa kipindi hicho kuanza la kwanza ukiwa na miaka 4 ilikuwa haiwezekani kwani hata miaka ya 80 ulikuwa ukitaka kuanza unaambiwa ushike mkono sikio kwa kupitisha mkono wako kichwani..kifupi kama huna mika nane na kuendelea ilikuwa haiwezekani..tumchunguze hata jk utakuta naeyumo maana tuliambiwa ni kijana mwenzetu..
Na kwa lishe gani aliyoipata miaka hiyo hadi alipokuwa na miaka minne aonekane ana urefu au size ya kumruhusu kuanza Darasa la kwanza???? Mimi nadhani ilipaswa ajitokeze atufafanulie umri wake ili mgongano huu uishe na heshima yake, ya serikali na ya chombo anachokiongoza viweze kutendewa haki. Akikaa kimya na kujifungia haitamsaidia zaidi ya kumvunjia heshima yeye, familia yake, aliyemteua na ya serikali kwa ujumla. Nadhani ni wajibu wa kiongozi wa umma kutoa ufafanuzi wa jambo ambalo umma umeli-doubt on you or on your office.
 
tukitaka mabadiliko majuha wengi wanatuona wehu, ni nafas ngap zimepigwa chenga hivyoo...? kila m2 akifia madarakani, taaluma ip itatumika kwa jamii ye2?
 
Kajitoa kesi ya Lema! Hii ina uhusiano na tuhuma hizi. Anajiandaa kuchukua maamuzi mazito? You know what I mean.
 
Madoro inaonekana wewe ni Hakimu sasa una hasira cheo hakipandi na umehamishiwa Tandahimba!!! Pole sana kaka ndio kazi hizo
 
Back
Top Bottom