omujubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 4,444
- 2,702
umeongea vizuri mkuu lakini tatizo hapa sio ccm bali ni Watanzania (yaani sisi). Hivi fikiria kidogo: Ukija kupanda ndege alafu ukapata ushuhuda wa wazi kuwa rubani hana uwezo wa kutosha unafanyaje? ...au chukulia unaenda kituo cha basi alafu unaona dereva amelewa chakali si unachagua gari nyingine na hata kama umeshalipa si angalau unaonyesha ujasiri wa kudai kurudishiwa nauli yako!?Nimeona alikuwa darasa moja na PM Mizengo Kayanza Pinda. Hivi PM wetu ana umri gani? We can start from there kufanya estimation ya umri HALISI wa CJ Omari Chande.
Haya mambo ya kugushi UMRI na ELIMU imeyalea CCM na inaonekana haijali kabisa unless someone has steped on their toes ndiyo utasikia sio RAIA (Ulimwengu, Bashe case). ame-forge Umri (Masauni, Nape case).
Mimi najua Omary Chande na Mdogo wake Othman Chande (boss wa TISS) wanasoma sana JF. Kwanini basi Chande asijitokeze hadharani hata kama sio JF aka clear the air kuhusu UMRI wake halisi? Hang on a little bit, nimesahau kwamba hii ni Tanzania chini ya CCM, ni Upepo tu utapita! You can forge everything with impunity.
Hebu angalia nchi za wenzetu makini, kama the MOST POWERFUL MAN ON EARTH, Barak Obama President of the USA alituhumiwa na mwananchi wa kawaida tu kwamba sio RAIA wa Marekani, lakini IKULU ya Marekani ikachukua liberty ya ku prove kwamba ni raia kwa kuonesha LIVE kwenye TV vyeti vya kuzaliwa vya Obama vinavyoonesha alizaliwa USA na ni Raia halali wa Marekani. Iweje Omary Chande au mahakama yenyewe ishindwe kufanya hivyo?!
Kama Chande ataendelea kuzika kichwa chake mchangani (style ya mbuni) ili hali kiwiliwili chake chote kikiwa nje, basi sisi wananchi tutaamini kwamba kweli amegushi UMRI wa kuzalia kwa KUOGOPA kustaafu mapema na hii itakuwa kashifa nyingine kwa mhimili huu wa kutoa HAKI.
Sasa sisi tumeshawajua hawa watu na hatufanyi maamuzi yoyote.
Nakumbuka issue ya akliyekuwa mbunge wa Temeke (Kihiyo) ilianza kama masihara lakini ikaishia kujulikana kuwa hakuwahi kusoma DIT/Dar Tech