Jaji Mkuu: Bajeti finyu chanzo cha mlundikano wa kesi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Jaji Mkuu: Bajeti finyu chanzo cha mlundikano wa kesi Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:37

Fidelis Butahe

NI jambo la kwaida kusikia watuhumiwa wa kesi mbalimbali nchini wakilalamika kuwa wamekaa muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa.

Zimekuwa zikitolewa sababu mbalimbali za kuchelewa kusikilizwa kwa kesi hizo ikiwa ni pamoja na kutomalizika kwa upelelezi wa tuhuma zinazowakabili washitakiwa.

pamoja na hayo inawezekana kauli ya Jaji Mkuu aliyoitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria jijini Dar es Salaam ikawa ndio jibu sahihi ya wale wanaolalamika kukaa muda mrefu bika kusikilizwa kwa kesi zao.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika nje ya Mahakama Kuu hivi karibuni yaliwakutanisha wanasheria mbalimbali ambapo Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman anasema uwelewa wa wananchi kuhusu mahakama na sheria ni mdogo.

Anasema elimu juu ya mahakama itamuwezesha mwananchi kutetea haki zake kikamilifu ndani na nje ya mahakama.

Anasema mahakama imefanya mambo kadhaa kuelimisha wananchi ikiwa ni pamoja na kushiriki katika maonesho mbalimbali na kuandika vipeperushi.

Jaji Othman anaeleza hofu yake kuwa elimu juu ya mahakama inaweza kuzua mzigo kwani shauku ya wananchi kudai haki zao itaongeza idadi ya migogoro mahakamani na kwamba hadi sasa bado kuna mrundikano wa mashauri katika mahakama mbalimbali.

Changamoto zinazoikabili Mahakama

Anasema changamoto zinazoikabili Mahakama ni pamoja na bajeti finyu isiyolingana wala kuzingatia mahitaji ya Mahakama jambo ambalo ni chanzo cha ulimbikizaji wa kesi.

Anasema kiwango cha bajeti ambacho wamekuwa wakiomba kimekuwa kikipunguzwa na kwamba hata kiwango kinachopitishwa na serikali huwa hakitolewi kwa wakati jambo ambalo hufanya mahakama ishindwe kufanya vikao vyake kama ilivyopangwa.

Anasisitiza kuiomba serikali ifikilie kuitengea Mahakama bajeti ya asilimia mbili kama kianzio katika mfuko wa mahakama.

Anasema changamoto nyingine ni upungufu wa mahakimu katika mahakama za mwanzo pamoja na majengo ya Mahakama hizo huku akisema kuwa majengo mengi ya mahakama hizo ni chakavu.

Anasema vituo vingi vya Mahakama za mwanzo viko mbali kiasi kwamba wananchi hutembea umbali mrefu kutafuta haki zao huku mahakimu wengine nao wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 100 kuhudumia mahakama hizo.

Changamoto zajibiwa

Akijibu hoja ya changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama, Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwepo katika sherehe hizo anaitaka Mahakama kuongeza kasi katika Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria.

“Ongezeni kasi ya maboresho ya sekta ya umma. Kwa sasa kasi iliyopo ni ndogo kwani hata wabia huwa wanalalamika kwa kukaa na pesa kwa muda mrefu na wakati mwingine wanalazimika hata kuzirudisha. Pengine hata haya malalamiko mengine yasingekuwepo sasa,” anasema Rais Kikwete.


Rais Kikwete anaitaka Mahakama kuongeza juhudi na hata kubuni maarifa mapya ya kupambana na tatizo la uadilifu kwa baadhi ya watoa uamuzi (mahakimu na majaji).

Anasema bado kuna hisia kwa baadhi ya watoa uamuzi kuwa ni watu wasiokuwa na pesa ni vigumu kuweza kupata haki.

“Uwezo wa kuondoa hisia hizi uko mikononi mwenu. Mafanikio yatarejesha imani kwa wananchi na kwa jamii za kimataifa,” anasisitiza Rais Kikwete.

Kuhusu tatizo la uhaba wa majaji Rais Kikwete anasema kwake si tatizo kuwateua hivyo akaitaka mahakama impelekee tu mapendekezo ya majina ya watumishi wanaostahili kuwa majaji ili yeye aweze kufanya uteuzi.

Mfuko wa Mahakama

Kuhusu mfuko huo anasema mchakato uko katika hatua za mwisho na kwamba kilichobakia ni kuandika tu mswada ili kuuepeleka bungeni na kupitishwa, anaongeza kwamba ni matarajio yake kuwa utaanza katika mwaka wa fedha ujao.

Rais Kikwete anaahidi kuendelea kuongeza bajeti ya Mahakama ikiwa ni pamoja na kuendelea kujenga vituo vya Mahakama Kuu kila mkoa na kuahidi kuendelea kujenga Mahakama za Mwanzo.

“Tengenezeni mpango wa uendelezaji wa mahakama za mwanzo gharama zijulikane tuweze kuandaa bajeti ili kurudisha hadhi ya mahakama hizo ambazo ni mahakama za wananchi,” anasema Rais Kikwete.

Uelewa wa wananchi juu ya sheria

Rais Kikwete anasema baadhi ya wananchi wamekosa imani naye kutokana na msimamo wake wa kukataa kuingilia uhuru wa mahakama wanapomtaka atengue uamuzi mbalimbali unaotolewa na mahakama.

Rais Kikwete anatoa wito kwa Mahakama kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwamo vyombo vya habari katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria na nafasi ya mahakama, akieleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kutoa elimu hiyo kwa umma.

Anasema watu wasiokuwa na elimu kuhusu mfumo wa utekelezaji wa sheria ni rahisi kuonewa na kudhulumiwa haki zao na kwamba wakijua jinsi zinavyofanya kazi na kwamba ziko kwa ajili ya kuwahudumia wao, watakuwa na imani nazo.

“Hii itanipunguzia hata taabu ninayoipata kuwa jambo likishaamuliwa na Mahakama mimi sina uwezo wa kulitengua. Mara nyingi kuna watu huwa wanakuja kwangu wakitaka nitengue uamuzi uliotolewa na Mahakama.

"Nikiwaambia kuwa mimi sina uwezo huo huwa wananishangaa sana na kuona kama ninakwepa wajibu wangu na kusema ni bora tumchague mwingine na kwamba ndio maana wanataka Katiba mpya.”
 
Tatizo la ufanisi kwenye mahakama zetu utaanza kushughulikiwa tu pale ambapo kutakuwepo uhusiuano wa moja kwa moja kati ya ajira za maafisa wa mahakama hizo na raia wa kawaida kwa maana ya kiuwajibikaji kupitia Bunge..............................Nyerere alikwisha kutusaidia aliposema fedha siyo msingi wa maendeleo ila ni matokeo tu...............................

Kwa muundo ulivyo kwenye mahakama zetu ambapo raia wa kawaida hauhusishwi na uteuzi na upandaji wa vyeo wa mahakimu na majaji kamwe wanasiasa pekee yao hawawezi kuwawadibisha watendaji tajwa na hata bajeti yote ya serikali wakipewa Mahakama haki itaendelea kudorora kwa sababu hakuna uwajibikaji kupitia wananchi ambao ndiyo wanaoathirika na utendaji wa muhimili huu..................................
 
Back
Top Bottom