...ondoa wasi wasi...kwa maoni haya matumaini yako...nimepatwa na wasi wasi.........
Nina imani sana na Jaji Massati ni jaji asiyeyumbishwa ( mgombea binafsi) pia Chande, hawa ni majembe 90%, wana wa Arusha anzeni kushangilia ushindi, ila M4C itayumba...dah!
Mhe.Jaji Kimario alikuwa mmoja wa majaji watatu walioamua rufaa yangu pia. Hili ni jopo lisiloyumbishwa. Huwa linapenda kufanya kazi kwa standard ya kuweka Case study nzuri kwa ajili ya mifano siku zijazo.. Nawaamini.
Kumekucha watanzania na wapenda haki.Jaji Mkuu wa Tanzania,Mheshimiwa Mohamed Chande Othman tayari amewasili jijini Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya Mh.Godbless Lema. Jaji Mkuu,katika jopo la Rufaa,atakuwa na Majaji Massati(wa Zombe) na Kimario. Rufaa ya Mh.Lema imepangwa kuanza kusikilizwa kuanzia tarehe 20/9/2012 katika Mahakama ya Rufaa kituo cha Arusha.
Hii inafuatia kuwasilishwa kwa hoja za rufaa na pande za kesi husika kimaandishi(written submissions) kama inavyotakiwa na Kanuni za Mahakama ya Rufaa,2009(kanuni ya 106). Arusha wanahitaji Mbunge.Walimchagua Lema na bado wanamhitaji.Wanaisubiri Mahakama ya Rufaa kuamua.

Next to Impossible, tarehe 20 mwili wa baba yake ndio unaagwa Tegeta Dar kuelekea Singida na kuzika ni Jumamosi, kama Rufaa itasikilizwa mfulululizo Lisu ni wa kumtegemea kuanzia Jumatatu. ila Wanasheria wenyewe wanajuwa namna ya kuendesha mambo yao. Lisu he know how to handle those matters.
chadema hoye
Independent Thinker Dr Ngongo,
Naomba maoni yako kwenye kadhia hii.
Mkuu wangu Ritz nadhani utakubalina na mimi kwamba wanaoshinda kesi yoyote iwe ya jinai au civil case mara nyingine utakuta wanashinda kwasababu ya uhodari wa mawakili wanaowawakilisha na si kwamba wana haki sana.
Katika kesi ya Bwana Lema na wanachama wa CCM yapo mambo kadhaa ambayo kama yangezingatiwa Lema asingechomoka hata kidogo lakini kwa mshangao wa wengi wanaCCM walimfungulia kesi either walishindwa kujipanga au hawakupewa ushirikiano wa kutosha na muathirika mkuu Dr Batilda na uongozi wa CCM mkoa wa Arusha.
Kwa maoni yangu Dr Batilda angetakiwa binafsi amshitaki Lema.Hilo halikufanyika badala yake wakajitokeza wanachama wa CCM ambao walidai matusi ya Bwana Lema yaliwaathiri na kupelekea mgombea wao Dr Batilda kushindwa.Mengine tuwaachie majaji wenyewe wana akili na ujuzi wa kupembua chuya na mchele.
Kwakuwa Dr Batilda hakumshitaki Bwana Lema ilitarajiwa na wengi angekuwa shahidi muhimu hasa ikizingatiwa aliyedhalilisha ni yeye na si wanachama wa CCM au chama cha mapinduzi.Kwa mshangao wa wengi Dr Batilda hakujitokeza mahakamani.
Ilitarajiwa wakili wa wanachama wa CCM wangewasilisha ushahidi wa video kwakuwa ulikuwepo lakini nao pia hakutumika mahakamani !.
Hukumu haikuwa na case law pia jaji alikosea kumkataza Bwana Lema asigombee kwasababu hapakuwa na mashitaka ya rushwa ambayo yanakipengele cha kumzuia anayepatikana na hatia kutogombea.Niko tayari kusahihishwa Mheshimiwa Steven Wasira aliwahi kuzuiliwa kugombea katika kesi aliyofunguliwa na Mhe Jaji Warioba.
Ninaamini Bwana Lema atashinda si kwasababu hakumkashifu Dr Batilda bali ni ubovu wa mawakili wa wanachama wa CCM kwa kutoiandaa kesi vyema na ubovu wa jaji aliyewapa ushindi.Ifahamike wazi ni kweli yapo baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Bwana Lema hasa sakata la Redio Safina kama yangewasilishwa vizuri mahakamani Lema asingekuwa na jeuri ya kukata rufaa.
Hata Mbowe alisema akifa yeye waweke mwili wake pembeni na makamanda waendelee mbele na Jeshi la ukombozi...Naamini jembe Lisu lazima ahudhurie hukumu...Vipi kuhusu Tundu Lisu kufiwa na baba yake? Ataweza kweli kuwepo kwenye shauri hiyo siku?
...huyo bwana wako ameshidwa na sasa amemtuma mke wake(CUF)...Arusha ilikuwa shwari baada ya huyu mwehu kupigwa chini,sala zetu zote ni kuhakikisha hoja zake zote zinatupiliwa mbali ili amani ya bwana iendelee kudumu.. Ameeeeeeeeen!!!
Amani ya Bwana SHETANI inataka watu wakiibiwa waseme hewala baba!! wakiporwa rasilimali; hewalla baba! wakishiba wao wengine wakifa njaa waseme hewalla bwana!! amani inayotakiwa na CCMABWEPANDE ni AMANI YA SHETANI. Karibu kamanda LEMA utuondolee huu ushetani!!Arusha ilikuwa shwari baada ya huyu mwehu kupigwa chini,sala zetu zote ni kuhakikisha hoja zake zote zinatupiliwa mbali ili amani ya bwana iendelee kudumu.. Ameeeeeeeeen!!!
sana sana arusha, watu wa arusha ni wa kuhurumia sana, shughuli za kiuchumi arusha zimepungua mno kiasi cha kwamba mji ukifika saa 10 jioni ni mweupeee hauna watu tofauti na zamani. Watu wa arusha wameathirika sana sana na vurugu za lema za kisiasa.
Nyongeza, na kwa wale ambao ni wageni hapa JF au ambao hawamfahamu huyu Member mwenzetu Ngongo huyu jamaa hampendi hata chembe Lema na haitokaa aje kumpenda. mwenye akili zake timamu anajuwa ni nini nimeongea na Ngongo ni mkweli kiasi gani kutoka moyoni mwake licha ya kwamba hampendi hata chembe Lema.