JAJI MKUU atua Arusha kwa Lema

JAJI MKUU atua Arusha kwa Lema

habari zisizokuwa rasmi" eti jey kei alishawahi kuwaambia viongozi wenzake wa sirikali na dola kuwa hapendi akienda arusha apokelewe airport na wapinzani..akimaanisha hataki mbunge, meya na diwani wa upinzani wawepo kwenye mapokezi yake"....

kwa kauli hizo haki hapa itatendeka na kuonekana bila hata kutumia torch kuwa haki imetendeka?????....

Naingiwa na woga maana haki kama inaweza kupigwa kabali na watu kwa kigezo cha jaji mkuu alikuwepo wakaipora haki na kutimuka nayo...ila nilishawahi kusoma kwenye kitabu cha bibilia kuwa "haki huwa inalia na haikai kimya mpaka mungu akisikie kilio cha haki"....

Tusubirie ili tuone na tusikie.
 
Jaji kachaguliwa na Rais na huyo Rais katokea Chama Cha Majangiri a.k.a CCM, na huyo aliekata rufaa ni mpinzani...Je! haki itapatikanwa hapo?......mna Bosi wa jaji ni Kikwete sasa atatetea Chama Cha Majangiri au atafanya vile haki inavyotakiwa??? ukweli hapa Tanzania hakuna haki kwa mpinzani wala masikini.....CCM OYeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Si majaji wote wenye mwelekeo wa upendeleo wa kisiasa.
 
Kuna taarifa kuwa kesi imeahirishwa ila itapangwa kwenye session hii ya mwezi wa tisa mwenye tarehe kamili atuwekee hapa


kama kesi ingekuwa imeahirishwa kungekuwa na haja gani ya jaji mkuu kuja Arusha leo?

au jaji mkuu amekuja kuaihirisha kesi maana mimi binafsi nimekutana na msafara wa jaji mkuu ukiingia mjini.
 
Arusha ilikuwa shwari baada ya huyu mwehu kupigwa chini,sala zetu zote ni kuhakikisha hoja zake zote zinatupiliwa mbali ili amani ya bwana iendelee kudumu.. Ameeeeeeeeen!!!

MWEHU ni wewe usiyejua mbele wala nyuma.
 
Mkuu wangu Ngongo,
Nimekusoma kwa miwani ya 3D nakubaliana na wewe Chadema wakijipanga vizuri kwenye jopo lao la wanasheria wanaweza kumrudisha Lema bungeni. Bahati nzuri Tundu Lissu yupo na kwa mujibu wa kauli yake majaji wengi wa Tanzania ni vodafasta anakwenda kupambana nao kwenye uwanja wa sheria yetu macho matokeo yoyote ya mahakama hatuna budi kuyakubali.


Kwa mara nyingine tena nakugongea like maana nimesisimuka mwili na kutokwa na machozi niliposoma hili uliloliandika.
kiukweli unanipa moyo kuwa ukombozi wa Tanzania umekaribi kama bado haujafika na unakwamishwa na wachache umeongea kwa hekima na busara bila jazba ndivyo inavyotakiwa kunako ukweli kusemwe ukweli na kunako uongo basi isemwe kuwa huu ni uongo na kama chama cha mapinduzi ingekuwa kinazingatia haya basi leo hii kusingekuwa na chama cha upinzani kinachoitetemesha.

Ritz kweli nimekupenda bure leo
 
Last edited by a moderator:
Ipo wazi rufaa ya Mh. Lema hata hakimu aliyetoka shule anaamua na kutoa haki, wakipindisha uma utawahukumu.


Hukumu ya kesi hii ya Lema itampandisha chati huyu Jaji mkuu mbele ya uma wa waTanzania au utathibitisha kuwa yeye yupo kwenye cheo hicho kwa upendeleo na si kwa weledi wake !! It is his integrity that is on the line now and for posterity!! Hopefully, he is aware of what is at stake; if he proves his worth he won't be shuttled out of office come 2015!!
 
Hatima ya Lema ipo hapa ni Chadema wenyewe wanatakiwa kijipanga na jopo lao wa wanasheria Jaji Mkuu ni mtu wa kufuata haki...


CHANDE_OTHMAN.jpg
 
Angalau jaji chande ataokoa hadhi ya mahakama na kurudisha imani ya wanachi kwamba mahakama ni chombo cha haki kwa wote.
 
Nimefarijika kuona wengi wanaliamini jopo litakalosikiliza rufaa hii; naamini haki itaonekana ikitendeka!
 
Nimefurahi mno kwa Jaji Mkuu kusimamia hii kesi. Ni mtu mweledi na anaheshimu kazi yake. Massati naye ni mzuri sana. Kwa kesi ya Zombe hakukosea maana kesi inataka uhakika wa ushahidi bila shaka yoyote. Na ikumbukwe iZombe hakushija bunduki akaua, ila kuna walioshika bunduki na kuua na jaji alisema watafutwe washitakiwe. Kesi ya mauaji ni kunyongwa au kuachiwa huru. Yule muuaji walimficha wenyewe na one day atajitokeza kama bado. Anasubiri upepo upite.
 
Ninahisi kuna uhusiano kati ya hukumu hii ya rufaa ya Lema na kufungwa kwa uwanja wa NMC Arusha. Serikali inajua fika kwamba kama rufaa hii itaamuliwa bila haki wananchi wa Arusha lazima waelekee revolutionary square (NMC). Hivyo solution iliyobakia ilikua kuufunga huu uwanja mapemaaaaa.

Ni mtazamo....
 
kati ya majaji wabovu na wenye skendo hapa tz huyo chande ni mmojawapo. kuna maskendo hapo dsm ajabu. kwanza anawalamba sana mahakimu huyo jaji....huyo jaji mzanzibari kama ameteuliwa na kikwete, unafikiri atakuwa fair? lazima tu atakuwa biased.
 
Back
Top Bottom