Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,520
- 93,090
Nyongeza, na kwa wale ambao ni wageni hapa JF au ambao hawamfahamu huyu Member mwenzetu Ngongo huyu jamaa hampendi hata chembe Lema na haitokaa aje kumpenda. mwenye akili zake timamu anajuwa ni nini nimeongea na Ngongo ni mkweli kiasi gani kutoka moyoni mwake licha ya kwamba hampendi hata chembe Lema.
Mkuu wangu Ritz nadhani utakubalina na mimi kwamba wanaoshinda kesi yoyote iwe ya jinai au civil case mara nyingine utakuta wanashinda kwasababu ya uhodari wa mawakili wanaowawakilisha na si kwamba wana haki sana.
Katika kesi ya Bwana Lema na wanachama wa CCM yapo mambo kadhaa ambayo kama yangezingatiwa Lema asingechomoka hata kidogo lakini kwa mshangao wa wengi wanaCCM walimfungulia kesi either walishindwa kujipanga au hawakupewa ushirikiano wa kutosha na muathirika mkuu Dr Batilda na uongozi wa CCM mkoa wa Arusha.
Kwa maoni yangu Dr Batilda angetakiwa binafsi amshitaki Lema.Hilo halikufanyika badala yake wakajitokeza wanachama wa CCM ambao walidai matusi ya Bwana Lema yaliwaathiri na kupelekea mgombea wao Dr Batilda kushindwa.Mengine tuwaachie majaji wenyewe wana akili na ujuzi wa kupembua chuya na mchele.
Kwakuwa Dr Batilda hakumshitaki Bwana Lema ilitarajiwa na wengi angekuwa shahidi muhimu hasa ikizingatiwa aliyedhalilisha ni yeye na si wanachama wa CCM au chama cha mapinduzi.Kwa mshangao wa wengi Dr Batilda hakujitokeza mahakamani.
Ilitarajiwa wakili wa wanachama wa CCM wangewasilisha ushahidi wa video kwakuwa ulikuwepo lakini nao pia hakutumika mahakamani !.
Hukumu haikuwa na case law pia jaji alikosea kumkataza Bwana Lema asigombee kwasababu hapakuwa na mashitaka ya rushwa ambayo yanakipengele cha kumzuia anayepatikana na hatia kutogombea.Niko tayari kusahihishwa Mheshimiwa Steven Wasira aliwahi kuzuiliwa kugombea katika kesi aliyofunguliwa na Mhe Jaji Warioba.
Ninaamini Bwana Lema atashinda si kwasababu hakumkashifu Dr Batilda bali ni ubovu wa mawakili wa wanachama wa CCM kwa kutoiandaa kesi vyema na ubovu wa jaji aliyewapa ushindi.Ifahamike wazi ni kweli yapo baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Bwana Lema hasa sakata la Redio Safina kama yangewasilishwa vizuri mahakamani Lema asingekuwa na jeuri ya kukata rufaa.
Ngongo hongera sana kwa hili kwamba nimepata kitu kutoka kwako na nitakutumia pm ni kwa nini unamchukia Lema huenda una sababu za msingi sana. viwavi wadandia hoja hawawezi kukuelewa ila naelekea kukuelewa.
Last edited by a moderator: