VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kumekucha watanzania na wapenda haki.Jaji Mkuu wa Tanzania,Mheshimiwa Mohamed Chande Othman tayari amewasili jijini Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya Mh.Godbless Lema. Jaji Mkuu,katika jopo la Rufaa,atakuwa na Majaji Massati(wa Zombe) na Kimario. Rufaa ya Mh.Lema imepangwa kuanza kusikilizwa kuanzia tarehe 20/9/2012 katika Mahakama ya Rufaa kituo cha Arusha.
Hii inafuatia kuwasilishwa kwa hoja za rufaa na pande za kesi husika kimaandishi(written submissions) kama inavyotakiwa na Kanuni za Mahakama ya Rufaa,2009(kanuni ya 106). Arusha wanahitaji Mbunge.Walimchagua Lema na bado wanamhitaji.Wanaisubiri Mahakama ya Rufaa kuamua.