Jaji Lubuva: Nape angeijua Serikali asingekurupuka

Jaji Lubuva: Nape angeijua Serikali asingekurupuka

Unafikiri kati ya Al shabaab na kdf nani alianza kuingia kwa mwenzake? na nafikiri watz tunautamani sana ugaidi maana hata askari akivamia na mapanga tunasema ni ugaidi na haliishi midomoni mwa baadhi ya watu kuwa ugaidi upo bongo.....yaani hata kanisani mbona nitakuwa siendi mie,ha! siwapendi kwa kweli...

Walianza alshababu kule mombasa waliteka watalii mara mbili
Nasikia wanapata thawabu wakiuwa watu
Nape anakunywa viroba aina ya valuu huwa inagandisha akili
 

Attachments

  • 1428220375542.jpg
    1428220375542.jpg
    48.5 KB · Views: 310
Aondoke kwanza jk kwa kutoipa tume vifaa vya kutosha na kuishia kutoa Bvr kits 250 badala ya bvr kits 8000.

Hapa ndipo ubabaishaji wa Lubuva ulipo.

Siku ile anaulizwa na waandishi wa habari kama anafikiria kwamba zoezi la uandikishaji litakwisha nchi nzima kwa wakati, yeye akajibu kwamba " we will cross that bridge when we get there"

Alipaswa kuwaambia akina JK muda ule ule kwamba ni ndoto kumaliza uandikishaji katika muda uliopangwa kwa sababu ya resources finyu.Ila hakufanya hivyo ili kulinda kibarua chake.
 
Kama angekuwa mrengo wa mahakama ya kadhi,mahakama ingemnyima haki ya kurithi kutokana na kukosa sifa za kurithi.Hata ukimuambia hana hizo sifa atabisha tu..Mzee Makamba usichoke huyu ni wako tu endelea kumbadilisha...mbona January hayuko hivyo....?
 
NAPE yuko sahihi, LUBUVA achia ngazi huna tija na taifa ni udanganyifu tu, Ukweli umekuwa siri kwani hiyo tume ya kusafirisha madawa ya kulevya??? Tume ya Uchaguzi eti kuna mambo kiongozi mkubwa kama nape hayajui, ni tume au chumba cha kulala cha mtu??? NEC yote iondoke haraka


Ukweli ni kwamba Mwenyekiti wenu DHAIFU amelikoroga na hivi sasa kama ilivyo tabia yake; he wants to pass the buck to The National Electoral Commission kuwa ndio waliozembea!!!! Wanatafuta mahala pa kutokea na wananchi wamewastukia,AIBU!!!!
 
Kwa mtu mwenye akili timamu na anaependa heshima yake.....hii ndio ingekuwa nafasi ya kujiuzulu na kuachana na kazi ambayo itamfedhehesha na kushushia kabisa hadhi yake.! Angesema sawa najiuzuru, angemshukuru Mungu kwa nafadi hii. Ila kwa kuwa nae ana agenda chafu ya siri...mwacheni ashikilie!! Watu wengi hawajui kuwa dada yake mndogo Lubuva wa baba na mama mmoja ...ndie mke wa Lowassa! ......tusubiri...
 
aliyepotosha juu ya kura ya Maoni ni Rais kwa kulidanganya Taifa kuwa itakuwa tarehe 30, April, 2015.
Kwa ni Nappe akimbilie kusema Mwenyekiti wa Tume awajibishwe badala ya kusema Rais wetu Jakaya M. Kikwete wajibika kwa kulidangaya Taifa?

Tunaweza kuchukulia hali iliyjitokeza kama suala la kawaida lakini kimantiki suala hili la Rais wa nchi kusema uwongo linahitaji mjadala zaidi wa kitaifa

Pasaka njema wadau!
 
Yaani kwa kuwa Jaji Lubuva anapewa maagizo na maelekezo ya nini na lini aseme kipi, anataka na Nape naye afanye hivyo hivyo.

Kwa hili Nape yupo sahihi. Lubuva na wababaishaji wenzie hawafai kuendelea kuiongoza NEC
aondoke kwa lipi?
 
Mtizamo wangu, sina hakika na uwezo wa kisiasa wa Waziri mkuu. Pia ninawasiwasi na ushirikishwaji au namna anavyoshirikishwa jambo na nafasi Yake ya kushauri jambo. Je huwa anahisishwa mapema au ametengwa na mambo Yakiharibika ndo yeye anatafutwa kutoa tamko?
Unaudhaifu mkubwa wa namna Ya kuamua mambo kwa watawala wetu ndio maana Jaji Lubuva anamwambia Nape hajui mambo yanayoendelea kwenye serikali yake Ya ccm Japo yupo ndani Ya ccm Tena kama katibu mwenezi.
Kifupi nape ndani Ya chama hadhi yake katika kujua mambo haina Tofauti na Lusinde (kibajaj)
 
Hata kama kuna tatizo kwenye tume ya taifa ya uchaguzi, Nape hakupaswa kuwakoromea kwenye vyombo vya habari bali angemshauri mwenyekiti wake (Kikwete) kuhusu mapendekezo yake binafsi.

Huu ni mwendelezo wa utendaji mbovu wa chama cha mapinduzi na serikali yake. Kila mtu anaropoka kila kinachokuja kinywani...tena kwa kuita waandishi wa habari.
Dhana ya kwamba chama kinaisimamia serikali naona inatafasriwa vibaya na baadhi ya viongozi wa CCM. Naona viongozi hao wameamua sasa kuwa kama ndio serikali kwa kutoa maagizo na kwa watendaji.
 
Hapa ndipo ubabaishaji wa Lubuva ulipo.

Siku ile anaulizwa na waandishi wa habari kama anafikiria kwamba zoezi la uandikishaji litakwisha nchi nzima kwa wakati, yeye akajibu kwamba " we will cross that bridge when we get there"

Alipaswa kuwaambia akina JK muda ule ule kwamba ni ndoto kumaliza uandikishaji katika muda uliopangwa kwa sababu ya resources finyu.Ila hakufanya hivyo ili kulinda kibarua chake.
dah, we unajuaje kama hakumwambia jk juu ya upungufu wa vifaa?
 
cha ajabu ngazi za juu za chama zinaweza pongeza utovu hu wa heshma kwa waliokuzidi UMRI
 
Nape kwa kuropoka hajambo.......kafikiri nini hadi kusema hvyo kwa mfano?au mwenzetu anafikiri kwa kutumia nywele
 
"Kama Nape angeweza kuwauliza wakubwa zake,serikali na Tume ya uchaguzi nina uhakika hayo aliyoyasema asingeyasema, lakini kwakuwa hajui ukweli ndio maana amekurupuka tu na mimi siwezi kujibizana nae,"alisema.
Hivi kwani Nape sio kiongozi mkuu naye!? Si anashikilia cheo muhimu kitaifa!?
Sasa ni wazi kuwa wanaosema kuwa huyu hajitambui ni kweli, yuko pale kama 'geresha'!
hii nimeipenda.
 
Hapa ndipo ubabaishaji wa Lubuva ulipo.

Siku ile anaulizwa na waandishi wa habari kama anafikiria kwamba zoezi la uandikishaji litakwisha nchi nzima kwa wakati, yeye akajibu kwamba " we will cross that bridge when we get there"

Alipaswa kuwaambia akina JK muda ule ule kwamba ni ndoto kumaliza uandikishaji katika muda uliopangwa kwa sababu ya resources finyu.Ila hakufanya hivyo ili kulinda kibarua chake.

Kama aliambiwa na kundi kubwa la watu kwamba hii haiwezekani na akabisha je angemwelewa huyu mmoja tena aliyempa cheo yy mwenyewe...tatizo CCM wanajiona wako sahihi muda wote
 
Aisee kweli hapo alikurupuka kabisa dah! Babalao 2 iko poa.

Ni nani hasa aliyekurupuka kati ya kikwete aliyetangazi umma kuhusu siku ya kura...kwa nn asingewaachia tume watangaze wenyewe...ona sasa rais alisema kura itapigwa mwenyekiti kasema haitapigwa....
 
Vyovyote vile: Vigogo wa nec wajiuzulu. Hawana kichwa wala miguu...
 
Heri ya Pasaka WanaJf

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Lubuva ameshangaa sana Kauli ya katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye aliyoitoa ya kwamba WAJIUZULU NAFASI ZAO kwa kuahhirisha tarehe ya kura ya maoni.
Akiongea kwa masikitiko Lubuva amesema
"Nape ni wa ajabu kwa nini asingeuliza wakubwa zake serikalini ambao ni Viongozi wake wa Chama ili kujua aliyekwamisha ni mimi au wao serikalini hizi ni sifa za Kitoto"
Nape na Kinana ina maana hayo mnayoyaongea huko majukwaani hamshauriani na Mwenyekiti wenu kabla ili mambo mnayoyafanya na kuongea yawe na nguvu zaidi?
Wananchi tutaamini vipi kwamba hayo mnayoyafanya na kuahidi yanaishia hewani tu?
Mwisho chama na Serikali huwa wanafanya kazi pamoja vp wewe hutaki kuuliza hata wateule wa Mwenyekiti wako unashutumu tu kutafuta sifa za muda tu jirekebisheni.

Kwa mujibu wa sheria ya kura ya maoni, NEC ndiyo wanaopaswa kutangaza tarehe na muda wa kura ya maoni. Nakumbuka mzee huyu aliwahi kusema (mtanisahihisha kama si kweli) kuwa NEC hawawezi kutangaza tarehe ya kura ya maoni mpaka maandalizi ya daftari la kudumu la mpiga kura yakamilike. Inawezekana aligoma kutangaza na ndipo JK akachukua jukumu hilo kinyume na sheria.

Ukitazama tamko lake la kusitisha tar 30 April, Lubuva anasema tar nyingine ya kura ya maoni, itatangazwa mara baada ya kushauriana na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar, na hiyo ni kwa mujibu wa sheria.

Tumuhurumie huyu mzee, inaonekana anafanya kazi kwa pressure za maccm na ndiyo maana kachoka sasa hata kuamua kumjibu Nape.
 
Back
Top Bottom