Jaji Lubuva: Nape angeijua Serikali asingekurupuka

Jaji Lubuva: Nape angeijua Serikali asingekurupuka

pesa zote anamaliza mwenyekiti wake kwa kuzurura,hivi ninavyoandika yupo hollywood anapiga selfie na anjelina jolie!
 
Hapo naona Nape katuma taarifa kwa M/kiti wake kupitia kwa Lubuva. Lakini Hii tume nayo imezidi kutumiwa kama toilet paper. Kwa hili Nape nakupongeza maana hii tume mmeshazoea kuitumikisha mtakavyo na haina mpangilio maalum. Akisimama JK akasema uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 this month hii tume itabadili maamuzi. Nawashauri Nape & Kinana ongezeni Matusi dhidi ya huyu kibaraka wenu, M/kiti wa tume ya uchaguzi.
 
Heri ya Pasaka WanaJf

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Lubuva ameshangaa sana Kauli ya katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye aliyoitoa ya kwamba WAJIUZULU NAFASI ZAO kwa kuahhirisha tarehe ya kura ya maoni.
Akiongea kwa masikitiko Lubuva amesema
"Nape ni wa ajabu kwa nini asingeuliza wakubwa zake serikalini ambao ni Viongozi wake wa Chama ili kujua aliyekwamisha ni mimi au wao serikalini hizi ni sifa za Kitoto"
Nape na Kinana ina maana hayo mnayoyaongea huko majukwaani hamshauriani na Mwenyekiti wenu kabla ili mambo mnayoyafanya na kuongea yawe na nguvu zaidi?
Wananchi tutaamini vipi kwamba hayo mnayoyafanya na kuahidi yanaishia hewani tu?
Mwisho chama na Serikali huwa wanafanya kazi pamoja vp wewe hutaki kuuliza hata wateule wa Mwenyekiti wako unashutumu tu kutafuta sifa za muda tu jirekebisheni.

Jk aliwahi kusema "Nape ni mtu ambaye hata akisimama sina uhakika na anachotaka kusema" mwisho wa kunukuu.
 
Kwa hiyo wakishajiuzulu achukue hizo nafasi zao yeye!! Yaani ukishazoea kuropoka hata kwa mke wako hutaona aibu... angekuwa mwanamke angevalishwa khanga huyu
 
Mkuu mwambieni Jaji Lubuva hana haja kujisumbua kufikiri sana.Yupo katikati ya watu wasiojua wanaenda wapi.
Ni kweli kabisa ulichosema mkuu.

Kwa mtu muadilifu na anayezingatia taaluma yake ya uanasheria, hawezi kumudu kutumikia Tume ya uchaguzi ya nchi yetu kwa mfumo wake ulivyo hivi sasa.

Kwanza tutambue Jaji Lubuva na wajumbe wote wa Tume ya uchaguzi, wameteuliwa na JK, ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kilichokuwa kimeandaliwa na hao Sisiem ni kuwa watu wapige kura ya maoni hapo tarehe 30 mwezi huu kwa kutumia vitambulisho vya zamani.

Mkakati huo ulitengenezwa ili kuliepuka kundi la asilimia 60 ya vijana ambao hawaiungi mkono kabisa Sisiem kwa sasa, ambao kama wangekuwa tayari wamejiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa mfumo wa BVR, kundi hilo lingeitosa kwenye 'dustbin' katiba pendekezwa ya magamba!

Hebu tujiulize swali moja tu la msingi, hivi kama Nigeria waliagiza vifaa zaidi ya 15,000 vya kujiandikisha kwa mfumo wa BVR, na wakaandikisha wapiga kura wao kwa zaidi ya mwaka mmoja, iweje basi serikali ya CCM iagize BVR kits 250 pekee, na wategemee kuvifanyia 'muujiza' kwa kuandikisha wapiga kura wa nchi nzima kwa kipindi cha miezi 2 pekee?!

Ndiyo maana lengo hilo la miezi miwili waliojiwekea kwa nchi nzima, hata mkoa mmoja tu wa Njombe hawajaumaliza!

Ndiyo maana alichofanya Jaji Lubuva naweza kukifananisha na kitendo cha kishujaa, na ameamua kuvua unafiki kwa kuwa kamgomea 'bosi' wake wa Sisiem aliyemteua kwenye nafasi hiyo, kufanya 'consiparancy' ya kuipitisha katiba pendekezwa ya Lumumba, kiujanja ujanja!
 
Hata kama kuna tatizo kwenye tume ya taifa ya uchaguzi, Nape hakupaswa kuwakoromea kwenye vyombo vya habari bali angemshauri mwenyekiti wake (Kikwete) kuhusu mapendekezo yake binafsi.

Huu ni mwendelezo wa utendaji mbovu wa chama cha mapinduzi na serikali yake. Kila mtu anaropoka kila kinachokuja kinywani...tena kwa kuita waandishi wa habari.

Kweli rafiki yangu umenena sawia kabisa. Ni serikali ya JK pekee yenye wasemaji lukuki. Hata NEC wenyewe si nao kabla walikuwa wakisisitiza kuwa April 30, upigaji kura ya maoni upo palepale? Kwani hata wao hawakujua kuwa muda huo kiutendaji hautoshi pamoja na uzoefu wao wa jiografia ya nchi yetu? Hapo hawahitaji kusutana kwa jambo hili ambalo liko wazi. TUSEME TU. !!! WANALENGO LA KUJENGA NYUMBA MOJA LAKINI HAWAELEWANI. MOJA AKIAMBIWA NA FUNDI MKUU ALETE TOFALI YEYE ANALETA JIWE AU ALETE NYUNDO YEYE ANALETA UFITO. NA HII IMEANDIKWA KAMA NDIYO MWANZO WA ANGUKO LA UTAWALA HUO KIUTENDAJI. Tusubiri, lisemwalo lipo kama halipo linakuja.
 
Hao vigogo wa NEC waondoke kwa kumpotosha Rais na Taifa kwa ujumla, Wamelitia aibu Taifa.

Kama rais ana weza akapotoshwa kirahisi namna hii na yeye akakubali kupotoshwa kirahisi namana hii, hafai kuwa rais na anatakiwa aondoke yeye ili mpotoshaji awe rais kwa maana ana akili na uwezo kumzidi rais.
 
Nape ni Juha kama majuha wengine kwanza hana criteria za kujadiliwa humu mtu ana division 5 leo katibu itikadi na uenezi aha aha only in Tz.
 
Nape amekuwa akitoa maneno pasipo uchunguzi wowote, Kama tume ingepewa fedha Na vifaa vya kisasa, kwa wingi unaotakiwa kuweza kuandikisha nchi hii nzima kwa muda uliowekwa, Na pia kupewa manpower ya kutosha then wakaulizwa Na kukubali, then wakashindwa kufankisha uandikishwaji huo kwa Wakati, Kama hayo yote yangefanyika sawasawa hapo ningemuunga mkono Nape. Lakini udhaifu mkubwa wa serikali awamu ya nne Ni poor organisational skills, Kama ukiangalia vzuri tume zote hizi kwa sasa haziwasiliani vema, Mara nyingi viongozi wanatoa kauli za kutofautiana, Na hata kupingana kwa suala moja. Kila mmoja Na kauli take, no common say on a certain issue, pamoja Na udhaifu mwingi wa serikali hii Ni poor coordination kwa mfano the same government regime, Tibaijjka anaanzisha plan ya mji wa kisasa Kigamboni, then Lukuvi anaukataa within the same regime, Kikwete anakataa serikali Na bunge visianzishe Mahakama ya Kadhi, huku Pinda anaipigania ipitishwe bungeni what a Shame Government Regime? Na mengine, Na mengine, mengi. So Nape you didn't go deep to justify your Claim.
 
Nape ni Juha kama majuha wengine kwanza hana criteria za kujadiliwa humu mtu ana division 5 leo katibu itikadi na uenezi aha aha only in Tz.

wakuu mnisaidie kujibu swali hili"Eti shetani angekua mtanzania angekua chama gani cha siasa"?
 
Hilo swali ata ukimuuliza mtoto wa kindagaten atakwambia jibu ni CCM.
wakuu mnisaidie kujibu swali hili"Eti shetani angekua mtanzania angekua chama gani cha siasa"?
 
Nape amekuwa akitoa maneno pasipo uchunguzi wowote, Kama tume ingepewa fedha Na vifaa vya kisasa, kwa wingi unaotakiwa kuweza kuandikisha nchi hii nzima kwa muda uliowekwa, Na pia kupewa manpower ya kutosha then wakaulizwa Na kukubali, then wakashindwa kufankisha uandikishwaji huo kwa Wakati, Kama hayo yote yangefanyika sawasawa hapo ningemuunga mkono Nape. Lakini udhaifu mkubwa wa serikali awamu ya nne Ni poor organisational skills, Kama ukiangalia vzuri tume zote hizi kwa sasa haziwasiliani vema, Mara nyingi viongozi wanatoa kauli za kutofautiana, Na hata kupingana kwa suala moja. Kila mmoja Na kauli take, no common say on a certain issue, pamoja Na udhaifu mwingi wa serikali hii Ni poor coordination kwa mfano the same government regime, Tibaijjka anaanzisha plan ya mji wa kisasa Kigamboni, then Lukuvi anaukataa within the same regime, Kikwete anakataa serikali Na bunge visianzishe Mahakama ya Kadhi, huku Pinda anaipigania ipitishwe bungeni what a Shame Government Regime? Na mengine, Na mengine, mengi. So Nape you didn't go deep to justify your Claim.
Kwa kweli serekali ya sasa hivi imekuwa kama lugha gongana haina nidham kila mtu ana weza akajisemea chochote ana chotaka,hajulikani nani ana pembe na nani asiye na pembe wote wanajiona ni vifaru wanaoweza kujifanyia kitu chochote bila kuhojiwa.

Wasio heshimiana wao kwa wao,walio kosa adabu kwa wananchi wote kwa ujumla wao,kama Nape alivyokosa adabu hata kwa watu asiolingana nao kiuwezo, na kielimu pia.
 
Mmoja wa wanaopunguza kura. Za ccm ni Nape.Jamaa ni ZERO kabisa,sijui alipewaje nafasi kubwa hivyo!!
 
Hao vigogo wa NEC waondoke kwa kumpotosha Rais na Taifa kwa ujumla, Wamelitia aibu Taifa.

Akili mgando hiyo,ulitaka Lubuva atoe pesa zake mfukoni kununua vifaa?Nape hana ujuzi wowote ya kazi wala hajawahi kufanya kazi zaidi ya bla bla mtaani.Huoni Kikwete ndiyo wa kunyongwa baada ya kuliingiza taifa ktk hasara hii?
 
Nape ni Mzee wa ajabu sana. Anakauli za kijinga, binafsi kama taarifa inamhusu huwa nabadilisha channel MAANA sichele kufyonya TV.
 
Back
Top Bottom