Jaji Lubuva: Nape angeijua Serikali asingekurupuka

Jaji Lubuva: Nape angeijua Serikali asingekurupuka

Maamuzi ya Judge ni maamuzi ya serikali thus ni maamuzi ya chama tawala
 
Heri ya Pasaka WanaJf

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Lubuva ameshangaa sana Kauli ya katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye aliyoitoa ya kwamba WAJIUZULU NAFASI ZAO kwa kuahhirisha tarehe ya kura ya maoni.
Akiongea kwa masikitiko Lubuva amesema
"Nape ni wa ajabu kwa nini asingeuliza wakubwa zake serikalini ambao ni Viongozi wake wa Chama ili kujua aliyekwamisha ni mimi au wao serikalini hizi ni sifa za Kitoto"
Nape na Kinana ina maana hayo mnayoyaongea huko majukwaani hamshauriani na Mwenyekiti wenu kabla ili mambo mnayoyafanya na kuongea yawe na nguvu zaidi?
Wananchi tutaamini vipi kwamba hayo mnayoyafanya na kuahidi yanaishia hewani tu?
Mwisho chama na Serikali huwa wanafanya kazi pamoja vp wewe hutaki kuuliza hata wateule wa Mwenyekiti wako unashutumu tu kutafuta sifa za muda tu jirekebisheni.

Inashangaza kuona kiongozi mkubwa wa chama hajui au anajifanya hajui tatizo lililosababisha zoezi la uandikishaji wapiga kura lichelewe, hata watu ambao hawako katika mtandao wa serikali wanajua ni kwa nini zoezi linasuasua. Kuelekea uchaguzi mkuu wa serikali tutasikia mengi watu kujitafutia sifa (cheap popularity) ili ziwasaidie katika uchaguzi.
 
Hao vigogo wa NEC waondoke kwa kumpotosha Rais na Taifa kwa ujumla, Wamelitia aibu Taifa.

Aibu amajitia mwenyewe kwa kuingilia kazi za watu kisheria. Nani anamamlaka ya kuitisha uchaguzi? Jaji Lubuva ameona, UKAWA wangeenda mahakama kuu kupinga uchaguzi kwa kutumia huja za kisheria
 
Hivi Nape na Zitto ni mapacha? Mbona wanafanana sana kifikra na matendo.
 
Dhana ya kwamba chama kinaisimamia serikali naona inatafasriwa vibaya na baadhi ya viongozi wa CCM. Naona viongozi hao wameamua sasa kuwa kama ndio serikali kwa kutoa maagizo na kwa watendaji.
Kweli kabisa, Nepi kakosa nidhamu kabisaaa, anatukana watu wenye heshima na hadhi kubwa ambao wamelitumkia Taifa hili kwa muda mrefu na udilifu. "mtoto wa kikopo aachi asili yake"
 
Nape anatakiwa akatolewe mitambiko kwa baba yake ila tatizo hamjui baba yake mzazi.
 
mtakubaliana tu, na sisi kina gogo la shamba tuliposema kwamba,ccm inayoubiriwa na Nape na Kinana ni tofauti sana na ccm inayoongozwa na Kikwete
 
Jamaa hua anajitia aibu sana ,ndo matatizo ya ma X children ,wanakuaga manunda
 
Hao vigogo wa NEC waondoke kwa kumpotosha Rais na Taifa kwa ujumla, Wamelitia aibu Taifa.

Waondoke kwa lipi iwapo tu wenyewe walisema kufanya mazoezi mawili kwa mwaka mmoja yaani kura ya maoni na uchaguzi ni vigumu,ccm wakalazimisha
 
Ni kwamba nape anaficha ukweli ni kwamba serikali haina pesa ndiyo maana hii issue ya BVR hakuna atakayesema kweli kama pesa ipo hawakujua kama kuna marekebisho ya daftari la wapiga kura.aibu kwa nchi kwenda kuazima vifaa kwa nchi kama kenya malawi na kwingine mh yupo nje anakula bata nchi haina vifaa vya kuandikisha wapiga kura jaji lubuva anashindwa kuongea ukweli kwa sababu anaona atamuumbua mwajiri wake.
 
hawa wateuliwa wa raisi wana vituko sana, uwwa namsikilizaga na kinana anavyouchachafa serikali kama sio chama chake.
 
Sasa mbona sioni tofauti ya chama tawala na chama shindani? Manake viongozi wa chama tawala nao wanalalamika kwa wananchi dhidi ya watumishi wa serikali yao wenyewe, badala ya kuwaadhibu kama wametenda makosa. Wanalalamika dhidi ya watu walio ndani ya uwezo wao chama tawala. Sasa ile tofauti na vyama shindani ni ipi?
 
yote ni miCCM inajuwana wanataka kupumbaza watu wote ni shauri moja Nape na CCM na LUBUvu na CCM namba moja
 
Sasa mbona sioni tofauti ya chama tawala na chama shindani? Manake viongozi wa chama tawala nao wanalalamika kwa wananchi dhidi ya watumishi wa serikali yao wenyewe, badala ya kuwaadhibu kama wametenda makosa. Wanalalamika dhidi ya watu walio ndani ya uwezo wao chama tawala. Sasa ile tofauti na vyama shindani ni ipi?
Mkuu wapo kwenye rehearsal ya Kuwa chama cha upinzani
 
Back
Top Bottom