Jaji huyu achunguzwe haraka

Jaji huyu achunguzwe haraka

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Kuna hukumu imetolewa na Jaji mjini Moshi ya faini ya Sh milioni 10 kwa raia wa Vietnam aliyetiwa hatiani kwa kosa la kukutwa akiwa na meno 60 (tembo 30) na kucha 260 za simba. Adhabu ya faini ya Sh milioni 10 ni ndogo mno.

Nini kilichomwongoza kutoa hukumu hii? Mamlaka za uchunguzi zifanye kazi kubaini kilichomfanya Jaji atoe hukumu nyepesi namna hii. Tukiwachekea watu wa aina hii wanyama watatoweka.

Nawasilisha.
 
Yawezekana kwenye sheria mtu akilipa faini sio lazima iwe na thamani sawa na kosa lake! mbona makosa ya barabarani yana faini ndogo na unakuta mtu aliyegongwa kafa au hata kapoteza kiungo. hata hivyo mie sio mjuzi wa sheria
 
Kuna hukumu imetolewa na Jaji mjini Moshi ya faini ya Sh milioni 10 kwa raia wa Vietnam aliyetiwa hatiani kwa kosa la kukutwa akiwa na meno 60 (tembo 30) na kucha 260 za simba. Adhabu ya faini ya Sh milioni 10 ni ndogo mno. Nini kilichomwongoza kutoa hukumu hii?
Mamlaka za uchunguzi zifanye kazi kubaini kilichomfanya Jaji atoe hukumu nyepesi namna hii. Tukiwachekea watu wa aina hii wanyama watatoweka.
Nawasilisha.
Wewe ni nani? na unajua sheria inasemaje kuhusu hyo kesi? au unadhan anashauriana na mkewe anakuja kutoa maamuzi? Cha msingi badilisheni sheria hizo ziendane na uzito wenyewe
 
Hii ni hatari, faini inataka kufanana na faini ya kosa la 'uchochezi'.

Afrika kwa waafrika.
 
[HASHTAG]#Sheria[/HASHTAG]
Angemhukumu kwa mihemko vyenye mnataka ni rahisi kwa mtuhumiwa kushinda rufani. Kuna haja ya kubadili sheria iwe strictly vifungo, maana faini ni ahueni kwa matajiri.
 
Yawezekana kwenye sheria mtu akilipa faini sio lazima iwe na thamani sawa na kosa lake! mbona makosa ya barabarani yana faini ndogo na unakuta mtu aliyegongwa kafa au hata kapoteza kiungo. hata hivyo mie sio mjuzi wa sheria

Kwa barabarani dhamana ya fidia hiko kwenye bima ambazo figure zake ni kubwa mno.
 
Kuna hukumu imetolewa na Jaji mjini Moshi ya faini ya Sh milioni 10 kwa raia wa Vietnam aliyetiwa hatiani kwa kosa la kukutwa akiwa na meno 60 (tembo 30) na kucha 260 za simba. Adhabu ya faini ya Sh milioni 10 ni ndogo mno.

Nini kilichomwongoza kutoa hukumu hii? Mamlaka za uchunguzi zifanye kazi kubaini kilichomfanya Jaji atoe hukumu nyepesi namna hii. Tukiwachekea watu wa aina hii wanyama watatoweka.

Nawasilisha.
Kwani sheria inasemaje kabla hujamtuhumu Jaji?!
 
Huenda sheria zetu ndio zina mushkeli maana kumshurutisha atoe hukumu tofauti na hio (kama hakuna nyingine) ni sawa na kumlazimisha avunje sheria ili kuwaridhisha wengine. Tujitathimini wenyewe kwanza
Kuna hukumu imetolewa na Jaji mjini Moshi ya faini ya Sh milioni 10 kwa raia wa Vietnam aliyetiwa hatiani kwa kosa la kukutwa akiwa na meno 60 (tembo 30) na kucha 260 za simba. Adhabu ya faini ya Sh milioni 10 ni ndogo mno.

Nini kilichomwongoza kutoa hukumu hii? Mamlaka za uchunguzi zifanye kazi kubaini kilichomfanya Jaji atoe hukumu nyepesi namna hii. Tukiwachekea watu wa aina hii wanyama watatoweka.

Nawasilisha.
 
Kuna hukumu imetolewa na Jaji mjini Moshi ya faini ya Sh milioni 10 kwa raia wa Vietnam aliyetiwa hatiani kwa kosa la kukutwa akiwa na meno 60 (tembo 30) na kucha 260 za simba. Adhabu ya faini ya Sh milioni 10 ni ndogo mno.

Nini kilichomwongoza kutoa hukumu hii? Mamlaka za uchunguzi zifanye kazi kubaini kilichomfanya Jaji atoe hukumu nyepesi namna hii. Tukiwachekea watu wa aina hii wanyama watatoweka.

Nawasilisha.
Labda ametumia sheria za Burundi si unajua tupo EAC
 
Ila kijana aliyeshikwa na sijui mirungi amefungwa miaka 29 jela ,hii ndio Tanzania
Ama sijui kumuita nani nani Bw.....faini milioni Saba

Hivi tuna uchungu na hii nchi ? Mtu wa aina hiyo angeingia kwenye mikono yangu kama angetoka hai basi angeenda kumshukuru Mungu wake kwa sadaka za kuteketeza
 
Wakati fulani huwa ninafikiria kuwa, kwa makosa yanayofikiriwa yatafanywa na watu wenye uwezo, basi adhhabu zake huwa nafuu. Na sheria hizi huwa hazirekebishwi mara kwa mara, kama ile ambazo walalahoi ni rahisi kuzivunja. Ni tafakari yangu tu kwawakati fulani fulani.
 
Back
Top Bottom