Afungwa miaka 20 jela kwa Utakatishaji Fedha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1686157656409.png

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Jausia Msophe kwenda jela miaka 20 au kulipa faini ya Sh500 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa mashtaka mawili likiwemo la utakatishaji wa fedha kiasi cha Sh158 milioni.

Pia mahakama hiyo imemuamuru kiasi cha fedha cha Sh158 milioni zilizokuwepo kwenye akaunti ya Ajuza Athuman ambaye ni ndugu wa Jausia, zirudishwe akaunti ya kampuni ya Glotel, huku nyumba yake iliyopo Kigamboni iuzwe na fedha itakayopatikana ipewe kampuni hiyo kwa mantinki kwamba ilitokana pesa ya utakatishaji.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Ruboroga ambaye amesema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi kumi wa upande wa Jamhuri huku mshtakiwa huyo akijitetea mwenyewe, imeridhika pasipo shaka lolote.

Ruboroga alisema katika shtaka la wizi wa kujipatia kiasi cha Sh158 milioni mahakama hiyo imemtia hatiani Jausia na kumuhukumu kifungo cha miaka nane jela.

Katika shtaka la pili la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha Sh158 milioni mahakama hiyo imemuhukumu Jausia adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh 500 milioni.

"Adhabu ya kifungo itaenda Kwa pamoja hivyo mahakama hii inamfunga kifungo cha miaka 20 au kulipa faini ya Sh500 milioni," alisema Ruboroga.

Awali Wakili wa Serikali, Rhoda Mwakalemela alieleza mahakama hiyo kuwa itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.

Katika kesi ya msingi inadaiwa Juni Mosi na Septemba 26, 2019, jijini Dar es Salaam, Jausia akiwa wakala wa kampuni Glotel alijipatia Sh158 milioni baada ya kuaminiwa.

Katika shtaka la mwisho ambalo ni utakatishaji fedha, inadaiwa siku hiyo mshitakiwa baada ya kupokea fedha hizo alizitumia kwa matumizi yake, binafsi wakati akijua fedha hizo ni mazalio ya kosa la wizi.

MWANANCHI
 
Kesho tu yupo MTAANI.

RUSHWA.

Chi hii very corrupt
Karibu uraiani Dada.
Jela ni kwaajili ya masikini tu.
 
Back
Top Bottom