Jangili ahukumiwa Jela miaka 20 na Faini ya Tsh. Bilioni 1 kwa kukutwa na Pembe za Tembo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Jumanne Hamis kwenda jela miaka 20 na kulipa faini ya zaidi ya Sh1 bilioni, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na vipande nane vya meno ya tembo.

Pia mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa Joseph Jeremiah baada ya upande WA mashtaka kishindwa kuthibitisha kosa linalomkabili.

Inadaiwa kuwa mshitakiwa Jumanne Machi 30, 2017 maeneo ya Temeke alikutwa na polisi akiwa amebeba vipande nane vya meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, ambapo amesema mshatakiwa huyo anakabiliwa na kosa la kukutwa na nyara za Serikali bila ya kuwa kibali.

Awali kabla ya hukumu, Hakimu Ruboroga amesema kuwa, upande wa Jamhuri walikuwa na vielelelezo vitano na mashahidi 11 huku washitakiwa hao walijitetea wenyewe, na hawakuwa vielelezo vyovyote walivyowasilisha.

Ruboroga amesema mahakama hiyo imeona ushahidi uliopitishwa na upande wa mashtaka ulikuwa hauna mashiko hivyo mshtakiwa Jeremia hana hatia kama alivyoshtakiwa

Amesema kutokana na hilo, mahakama hiyo imemwachia huru mshatakiwa Jeremia baada ya ushahidi kuonyesha kuwa hana hatia katika kesi hiyo.

Ruboroga amesema mshtakiwa Hamisi ametiwa hatiani baada ya upande wa Jamuhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

"Mahakama imeona ushahidi uliopitishwa na upande wa mashtaka una mashiko hivyo mshtakiwa ana hatia kama alivyoshtakiwa," amesema Ruboroga.

Baada ya maelezo hayo mshtakiwa Hamisi aliomba mahakama hiyo itoe maamuzi kwa kuzingatia muda aliokaa gerezani.

Awali wakili wa Serikali, Roida Mwakamele alidai mshtakiwa huyo apewe adhabu kali kwa kosa la uhujumu uchumi, upotevu wa rasilimali za nchi, ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Ruboroga, amesema mahakama hiyo inamuhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 20 jela na faini ya zaidi Sh1 bilioni.

"Tunachukua thamani ya vipande nane vya meno ya tembo ambayo ni Sh100, 215, 000; tunazidisha mara 10; hiyo ndiyo faini mshitakiwa anakuwa kuilipa," amesema Ruboroga.

MWANANCHI
 
Hukumu za ajabu hizi.

Mitembo kila siku inaua watu huko kusini.

Mazao yanaliwa fidia zenyewe za kingese ila wewe ukimuua tembo unatiwa matatizoni
 
Back
Top Bottom