J.K Nyerere na siasa za maji taka

J.K Nyerere na siasa za maji taka

allydou

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2009
Posts
1,603
Reaction score
1,065
Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?

" Kambona , ah, ah!

Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"

Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.

MY TAKE:

Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.

Naomba kuwakilisha mada.
 
kwa hiyo unapendekeza nani awe baba wa taifa!? Na hiyo historia unapendekeza iweje.
 
dah sijawahi kuusikia huu wimbo...nipe link
 
Nimesoma sana Historia yetu lakini bado sijaona kosa na ubaya wa hawa waheshimiwa / wanasiasa / wanamapinguzi mashuhuri katika historia ya nchi yetu.

1. Oskar Kambona - RIP
2. Christopher Kasangatumbo - RIP (Balozi wa kwanza nchini uingieleza baada ya uhuru)

Yaani ulipokuwa unatofautiana focus & Vision tu na TICHA aka Mwalimu, basi wewe hesabu maumivu - yaani adhabu ya maisha wewe na familia yako.
 
dah sijawahi kuusikia huu wimbo...nipe link
 
Sikuwahi kuusikia huu wimbo ingawa akulikuwepo nyimbo zingine zinazolandana
na huu kuwahusu kina Banda wa Malawi, Iddi Amin Dadaa, nk. Anyway, nilipita tu.
 
Mzee Mwanakijiji aliyasema haya na kweli yameanza kutokea. Ngoja tuone yatakapofika, by the way nilikua napita tu
 
Mods, hawa watu wanomdhalilisha hivi Baba wa Taifa kwanini tunazilealea threads za jinsi hii? Kuna mambo mengi yanayotukabili kwa Tanzania ya leo na yanahitaji kujadiliwa. Sasa hili la mwaka 1960s linatusaidiaje kwa sasa? Siasa za Nyerere na Kambona zina tija gani hapa? Tazama hata wimbo anaouongelea huyu mtoa mada mtovu wa nidhamu, walio wengi hawaujui, ninyi watu chuki zenu dhidi ya Mwalimu msituletee hapa,, kufeni na chuki na vijiba vya roho zenu.
 
Wana MAGAMBA hizi propaganda haziwasaidii chochote zaidi ya kutafuta laana tu!!
 
Mods, hawa watu wanomdhalilisha hivi Baba wa Taifa kwanini tunazilealea threads za jinsi hii? Kuna mambo mengi yanayotukabili kwa Tanzania ya leo na yanahitaji kujadiliwa. Sasa hili la mwaka 1960s linatusaidiaje kwa sasa? Siasa za Nyerere na Kambona zina tija gani hapa? Tazama hata wimbo anaouongelea huyu mtoa mada mtovu wa nidhamu, walio wengi hawaujui, ninyi watu chuki zenu dhidi ya Mwalimu msituletee hapa,, kufeni na chuki na vijiba vya roho zenu.

kama hujui umuhimu wa historia ya nchi yako kwenye maendeleo yake, hufai kuwa humu , kwa sababu wewe sio GREAT THINKER. Nyerere hajadhalilishwa humu, hapa tunaongea ukweli, its whrere we dare to talk openly. hii ni FORUM
 
MNASEMA NYERERE NDO ALIKUWA ANAZIIMBA AU NYIE HUKO MITAANI.....?
Mwalimu ni mtu tofauti TUSIMSINGIZIE ...... sema ukweli ili ukweli wako usambae
 
kama hujui umuhimu wa historia ya nchi yako kwenye maendeleo yake, hufai kuwa humu , kwa sababu wewe sio GREAT THINKER. Nyerere hajadhalilishwa humu, hapa tunaongea ukweli, its whrere we dare to talk openly. hii ni FORUM
Hiyo siyo historia ya nchi wala hakuna ukweli wowote bali udaku tu. Nyerere hakuwa mwimbaji wala hakutunga au kubariki wimbo wa aina hiyo. Ukiwa unataka kujua historia sawasawa, SOMA hotuba zote zilizotolewa na nyerere au interview alitofanya na Peter Enahoro wa Africa Now kuhusu mgogoro wake na kambona.
 
Mimi sijawahi usikia huo wimbo, na wewe kama uliusikia je ni Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa anaimba au ni walimu wako ndiyo walikuwa wanakuimbisha ?
 
Huo ulikuwa wimbo wa mchakamchaka huko jeshini. Haukuwa wimbo rasmi wa kiserikali. Ulifikishwa mashuleni na walimu waliotokea JKT
 
Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?

" Kambona , ah, ah!

Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"

Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.

MY TAKE:

Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.

Naomba kuwakilisha mada.

Sasa huo wimbo ni Nyerere alikuwa anauimba au ni nyie kwa utovu wenu wa heshima ndio mlikuwa mnauimba huko mtaani? Ni Nyerere aliutunga?
 
Mods, hawa watu wanomdhalilisha hivi Baba wa Taifa kwanini tunazilealea threads za jinsi hii? Kuna mambo mengi yanayotukabili kwa Tanzania ya leo na yanahitaji kujadiliwa. Sasa hili la mwaka 1960s linatusaidiaje kwa sasa? Siasa za Nyerere na Kambona zina tija gani hapa? Tazama hata wimbo anaouongelea huyu mtoa mada mtovu wa nidhamu, walio wengi hawaujui, ninyi watu chuki zenu dhidi ya Mwalimu msituletee hapa,, kufeni na chuki na vijiba vya roho zenu.

Tunajifunza kutokana na matukio ya zamani ili tusirudie makosa.

Kama ni hivyo basi hata somo la historia lisifundishwe mashuleni.

Nyerere sio mtume jamani acheni woga aaaaagrrr
 
Mara 100 ya Nyerere kuliko viongoziwetu wa sikuhizi.
 
Kama hizo zilikuwa siasa za maji taka, sijui za siku hizi zitaitwaje ( labda tuziite siasa za mav* taka)

All in all,

Hizi siasa za kulialia, kulalamika, kusingizia, kuchekacheka, kubeza,
Siasa za kidole juu,
Siasa za mipasho,
Siasa za ufinyu wa fikra hazitatutoa kwenye lindi la kifo,

Tuachane nazio hizi,

Tuje front kujenga nchi yetu "leo"

Hayo ya kale tutayatafutia mahali muafaka kwenye museum zetu

Tuache kulialia kama watoto walionyimwa pipi

Tuchkue hatua sasa!

Katiba ya watu na ije

Ameen!
 
Una umri gani ndugu, maana hujui kitu, hata hiyo national service yako ni ya mashakamashaka sijui kama kweli ulitumikia JKT alafu ukawa na akili uliyonayo. Any way tunaelewa magamba siku hizi hawataki kusikia habari wala jambo lolote la Mwl JKN. Ebu television yoyote iweke speech za Mwalimu, itakuwa dhambi mbele ya ccm magamba maana zinawachoma, zinawanyonga,zinawahukumu kisawasawa.
Ebu kumbuka speech hii " Watanzania kama msipoangalia litaibuka kundi la wahuni, litamobilise watu, litachukuwa utawala wa nchi hii, litaongoza nchi kihuni"Je ccm mnalo hapo?
"ccm siku moja Watanzania hawa watapotambua kwamba mmewaibia mali zao wote mtaishia jela!" ccm semeni.
Tusiandikie mate wino upo, wekeni hotuba za mwl Nyerere. kwishney, kwishney!
Huyu MZEE alikuwa kama mtabiri, subirini jela.
Hata wewe umekodishwa kumshambulia mwalimu, mmemshindwa Dr wa kweli ,Slaa, mnamrukia Nyerere, mmekwisha kabisa, hata mwenyekiti mliyemtukuza sasa mnamtukana.
Kumbukeni Mwalimu aliwahi kusema, "CHADEMA vema" Sasa CDM INAWATESA kisasawa na kweli mtaishia jela.Hofu imewatawala, imewatafuna hadi kwenye mifupa. CCM hawana hata Baba wa Taifa, eti wanamwita mzee Nyerere!!!

Natoa hoja ccm wekeni hotuba za mwl Nyerer tujadili.
 
Back
Top Bottom