J.K Nyerere na siasa za maji taka

J.K Nyerere na siasa za maji taka

kama umeamua kuwa agaist na ccm lazima uanzie kwa nyerere.he is the axis of evil (mhimili wa uovu) i think he is in hell right now..........[/QUOTE
nyie mbona hamtaki kuelewa? nyerere alifanya mambo makubwa sana katika nchi hii wakati wa uongozi wake lakini ccm kwa miaka 50 ya uhuru wa tanzania haijafanya chochote. shida iko wapi?
 
Bado tutachukua mda mrefu kumpata kiongozi kama mwalimu nyerere. Alitusomesha bure, alitutibu bure, alitutafutia ajira bila kutuma maombi. Alimjali mkulima kwa kununua mazao yake bila kumchelewesha. Aliheshimika na viongozi wa siasa, dini na asasi mbalimbali wa dunia nzima.
Hakuna kama nyerere. Muulize kaunda, nelson mandela, mseveni, jim carter, malikia elizabeth n.k
 
Baba wa taifa. Mh salmini alimwita babu wa taifa huyo
Udini umekujaa sana, lakini kwa kwa tunajua mkakati wenu tangu zamani, hamtafanikiwa. Si salmini, wala mwinyi, wala ****** watapata hiyo hadhi!
 
Hakuna kama nyerere?...NO NO NO kama alikua mzuri kihivo mbona jeshi likataka kumpindua?
 
Kwa mtazamo wangu, unajua mtu waweza fanya mamo mengi sana kwenye jamii au taifa kwa ujumla. Hasa unapokuwa kiongozi mkuu wa nchi,ukiwa kama kiongozi wa nchi vitu kama lawama ni kitu cha kawaida kwa sababu unaongoza makundi mbalimbali ya watu.

Hivyo yawezekana Mwalimu JK alikuwa ana mapungufu yake, lakini amefanya makubwa pia so tusimuhukumu kwa mambo madoga aliyofanya pia tumkumbuke kwa mambo makubwa aliyotutendea.

Binafsi namuona kweli anastahili kuwa baba wa taifa hili kwa sababu naamini kama angelikuwepo hadi leo si dhani kama tungepoteza muelekeo kama hivi sasa. Ange-play part yake anusuru taifa kugawanyika vipande vipande.

Mungu mlaze mahala pema peponi kiumbe wako kwa yoote mazuri aliyetufanyia na pia msamehe kwa yale madogo aliyoteleza kama binadamu.
Tatizo si mapungufu au makubwa aliyotenda Baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere katika taifa hili bali tatizo ni upumbavu wa watu kuficha mapungufu yao kwa kutoa sababu ati hatukuendelea kwa sababu ya nyerere, ati tupo hapa kwa sababu ya nyerere, wakati hata punguwani anajua kuwa JK nchi imemshinda.
Ni kweli kabisa laana inawasumbua, na bado, mtawehuka sana.
 
link sina mkuu, lakini tumeimba sana hule ya msingi, miaka ya themanini.
tuliosoma miaka ya themanini hatukuimba wimbo huu wewe mzuka nini, au uliimbia shule za msingi za malawi?
 
Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?

" Kambona , ah, ah!

Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"

Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.

MY TAKE:

Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.

Naomba kuwakilisha mada.
kama ulikuwa unaimba hivyo na wewe unamatatizo upstairs. hata hivyo ni nyerere aliyetunga?
 
Nyie mnaotaka kumdhalilisha baba wa taifa ny*ro zenu zina shar*wala, pambafu sana.

Huyo kilaza wenu kazi yake kucheka cheka alichakachua kura na nchi imemshinda -amechapisha hela feki na bado nchi haina hela.

Anazurura tuu kuomba misaada wakati nchi ni tajiri ---- anaachia madini yanachukuliwa.

Baba wa taifa his excellence j.k nyerere alitoa elimu bure, afya, barabara alijenga,train alijenga,bandari alijenga, viwanda alijenga.

Hata huyo kilaza kiwete wenu alisoma bure,

sasa nyie na vasco da gama mmejenga kiwanda gani???
 
Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. QUOTE]

Sijui ni nani hasa muasisi wa hii campaign ya kumchafua marehemu. Kwa mila, desturi na hata kwa dini nyingi 'mudslinging' campaign dhidi ya Baba Taifa is the lowest point a nation can reach. Nashindwa kujua kuna nini nyuma ya pazia. Nyerere hayuko hai kujibu hizi tuhuma lakini kwa makusudi kuna watu wameamua kufanya special assignment ya kumchafua. all in all @alldou, kama Nyerere alifanya maji taka na wewe pamoja na wote wenye mtazamo huo, nikuulize, mmefanya nini toafauti na Nyerere ili kweli tukubali haya uliyoandika?

Na siasa zake za maji taka kwa vipi hasa? Ni kwa sababu alileta elimu bure? huduma za afya bure, ATC, ranchi za taifa, au kwa sababu alijenga Mwatex? Tanganyika packers etc? Tarime wameuliwa watanzania wenzako na maiti zao kutupwa barabarani. Arusha wamepigwa rasasis raia watatu na hakuna mtu yoyote amekamatwa wala hakuna uchunguzi! Hili taifa limekuwa fedheha, hakuna msimamo si ndani ya nchi na sio kwenye ulingo wa kimataifa. Tumekuwa tunalishwa na Ghadafi aliyeungana na Idd Amin kutuuwa na sasa tunashindwa cha kusema maana tuna kibakuli Marekani na huku tuna kibakuli kwa Ghadafi. According to Membe - we are lying low! maybe she should say we are low on moral authority! Fedheha!
 
MNASEMA NYERERE NDO ALIKUWA ANAZIIMBA AU NYIE HUKO MITAANI.....?
Mwalimu ni mtu tofauti TUSIMSINGIZIE ...... sema ukweli ili ukweli wako usambae

Umenifurahisha! Kwanza sio kweli wimbo kama huo uliimbwa miaka ya 80. Mchakamchaka ilifikia kilele miaka ya 70! Lakin nakumbuka Nyerere alikuwa na wakati mgumu wa kuwawekea breki wafuasi wake. Wako waliotafisiri siasa ya ujamaa kama chuki na hawa walifanya mambo mengi kwa kiwango cha juu hata kuumiza na kuua bila Mwl kufahamu. Na mara alipofahamu hakusita kuwalaani na kuwakemea. Ninalokumbuka kwa haraka haraka ni lile la kufunga maduka ya watu binafsi, ambapo Nyerere alibidi amkemee Kawawa! Ilitokea wakati fulani ufisadi kwenye kununua ndege, na Nyerere hakusita, alimwadhibu mara moja aliyehusika. Ufisadi wa sasa unawahusisha wakuu, lakini kwa Nyerere, thubutu! Msimlaumu bure baba wa Taifa! Alifanya yake!
 
Sasa huo wimbo ni Nyerere alikuwa anauimba au ni nyie kwa utovu wenu wa heshima ndio mlikuwa mnauimba huko mtaani? Ni Nyerere aliutunga?

Nyimbo nyingi ziliimbwa na kutungwa na watu waliokuwa wakijitafutia riziki kwa viongozi wa wakati huo. kama ilivyo sasa kwamba kuna mashabiki
wanaoshabikia viongozi au makundi fulani ya kisiasa kwa lengo hilohilo la kujitafutia riziki.
 
Mods, hawa watu wanomdhalilisha hivi Baba wa Taifa kwanini tunazilealea threads za jinsi hii? Kuna mambo mengi yanayotukabili kwa Tanzania ya leo na yanahitaji kujadiliwa. Sasa hili la mwaka 1960s linatusaidiaje kwa sasa? Siasa za Nyerere na Kambona zina tija gani hapa? Tazama hata wimbo anaouongelea huyu mtoa mada mtovu wa nidhamu, walio wengi hawaujui, ninyi watu chuki zenu dhidi ya Mwalimu msituletee hapa,, kufeni na chuki na vijiba vya roho zenu.
kwani nini maana ya historia?
 
Kwa mtazamo wangu, unajua mtu waweza fanya mamo mengi sana kwenye jamii au taifa kwa ujumla. Hasa unapokuwa kiongozi mkuu wa nchi,ukiwa kama kiongozi wa nchi vitu kama lawama ni kitu cha kawaida kwa sababu unaongoza makundi mbalimbali ya watu.

Hivyo yawezekana Mwalimu JK alikuwa ana mapungufu yake, lakini amefanya makubwa pia so tusimuhukumu kwa mambo madoga aliyofanya pia tumkumbuke kwa mambo makubwa aliyotutendea.

Binafsi namuona kweli anastahili kuwa baba wa taifa hili kwa sababu naamini kama angelikuwepo hadi leo si dhani kama tungepoteza muelekeo kama hivi sasa. Ange-play part yake anusuru taifa kugawanyika vipande vipande.

Mungu mlaze mahala pema peponi kiumbe wako kwa yoote mazuri aliyetufanyia na pia msamehe kwa yale madogo aliyoteleza kama binadamu.

Nyerere hawezi kuwa baba wa taifa. Kwanza lazima ujue TZ haifuati tena sera zake, Ni sera za Mwinyi ndizo zinazofuatwa, Free Market, na siyo Ujamaa. Kwa hiyo Mwinyi ndiye aliyeweka foundation ya nchi. Kwa hiyo Mwinyi ndiyo anatakiwa apewe heshima zote na siyo Nyerere, kwa sababu alifeli.
 
hata mimi niliimbishwa sana sec na za kumtusi idd amini dada maiti
 
Jamani mbavu zangu!Mkuu umenikumbusha mbali sana. Sina nia ya kumdhikaki mwalimu ila nataka kuonyesha jinsi tuilivyokuwa tunakaririshwa mistari biila kuelewa maana yake.Huu wimbo tuliuimba sana shuleni kwetu, ila sikuwahi kuhisi au kufikiri kuwa ulikuwa na maana uliyoyotuambia. Sisi tulikuwa tunaimba: Kambona ah ha... aha. kamboana... AMEULIWA, wapii.... huko ULAYA. Kilichonichekesha ni kuwa imepita miaka mingi sasa( zaidi ya 20) lakini sikuwahi kuhisi kwamba huo wimbo ulikuwa na maana nyingine!
 
Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?

" Kambona , ah, ah!

Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"

Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.

MY TAKE:

Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.

Naomba kuwakilisha mada.

Sio wimbo tu bali Nyerere aliwadhalilisha wapigania uhuru wengi tu na kuwaswaka jela kama akina Bibi TITI Mohamed, Tewa S. Tewa na wengine kwa chuki zake tu!! Mungu amlaani huko aliko!!!!!
 
Mods, hawa watu wanomdhalilisha hivi Baba wa Taifa kwanini tunazilealea threads za jinsi hii? Kuna mambo mengi yanayotukabili kwa Tanzania ya leo na yanahitaji kujadiliwa. Sasa hili la mwaka 1960s linatusaidiaje kwa sasa? Siasa za Nyerere na Kambona zina tija gani hapa? Tazama hata wimbo anaouongelea huyu mtoa mada mtovu wa nidhamu, walio wengi hawaujui, ninyi watu chuki zenu dhidi ya Mwalimu msituletee hapa,, kufeni na chuki na vijiba vya roho zenu.
We waache tu watokwe povu vinywani mpaka likauke. Hadhi ya Mwalimu itabaki pale pale. Don't bother with these goons!
 
Back
Top Bottom