J.K Nyerere na siasa za maji taka

Kwa mtazamo wangu, unajua mtu waweza fanya mamo mengi sana kwenye jamii au taifa kwa ujumla. Hasa unapokuwa kiongozi mkuu wa nchi,ukiwa kama kiongozi wa nchi vitu kama lawama ni kitu cha kawaida kwa sababu unaongoza makundi mbalimbali ya watu.

Hivyo yawezekana Mwalimu JK alikuwa ana mapungufu yake, lakini amefanya makubwa pia so tusimuhukumu kwa mambo madoga aliyofanya pia tumkumbuke kwa mambo makubwa aliyotutendea.

Binafsi namuona kweli anastahili kuwa baba wa taifa hili kwa sababu naamini kama angelikuwepo hadi leo si dhani kama tungepoteza muelekeo kama hivi sasa. Ange-play part yake anusuru taifa kugawanyika vipande vipande.

Mungu mlaze mahala pema peponi kiumbe wako kwa yoote mazuri aliyetufanyia na pia msamehe kwa yale madogo aliyoteleza kama binadamu.
 
MM aliyasema haya kati ya tarehe16/6/2011 hadi 18/6/2011 kuwa kuna watu watakuja kwa kasi ya ajabu na kuaanza kumshambulia mwalimu nyerere,naona tayari wameanza.
 
Naomba msaada jamvini, who is behind this campaign to discredit Baba wa Taifa?
1.Is it Edward kwa vile viwango alivyoweka Mwl kamwe hawezi kuvifikia na tukisikiliza ushauri alioutoa hakuna atakayemchagua?
2.Ni JK katika kufunika udhaifu wake na kuchochea udini?

It has to be one of these two gentlemen au wote kwa pamoja.
 
MWALIMU NAE ALIKUWA GAMBA TUU,NA HAYA MAGAMBA YALIYOPO SASA NI WATOTOT WAKE,NYOKA ANAZAA NYOKA

msisahau
 
Tatizo hapa ni kuchanganya mambo! Nyerere hakutunga wimbo kama huo ni hao walimu toka JKT ndo waliusambaza.Sasa ulitaka Nyerere awe anafuatilia nyimbo za mchakamchaka! Hata hvyo yeye ameshakiri kwamba, katika awamu yake amefanya mazuri na mabaya pia Kwani yeye ni binadamu! "UBAYA WENU NYINYI MNACHUKUA MABAYA TU" Aliwahi kusema Mwalimu.Kinachokusumbua Wewe Ally ni udini tu!.
 
Hivi huu wimbo aliutunga wapi vile.....????, sikujua kwamba mwalimu alikuwa Mtunzi

sijasema alitunga yeye, doesnt matter alitunga nani, lakini kama uliumika sana, iwe uraiani au jeshini, no matter ni JKT au JW, lakini alikuwa anaujua, na kama ulitumika JKT ndio kabisaa atakuwa aliufahamu. Point ni kwamba, wimbo wa kumdhalilisha kiongozi mwenzio, unaachwa utumike miaka yote hiyo, huoni kama something is wrong hre. Dont treat the guy the same way as GOD.

pili, tujaribu kutofautisha mistakes, na mambo yanayofanywa kwa makusudi. huwezi kusema kulifumbia macho hilo ni mistakes, no hiyo ni dhamira.

wana JF, naomba ieleweke kwamba this is not a personel attack or hatred to the late old guy. kujua ulipojikwaa ndio mwanzo wa kutatua tatizo, kwa hiyo si kosa kuangalia tulijikwaa wapi.
 
Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?

" Kambona , ah, ah!

Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"

Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.

MY TAKE:

Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.

Naomba kuwakilisha mada.

Inaonekana Mwalimu alikuwa na juhudi sana hadi miaka ya 80's alikuwa anakimbia na nyie mchakamchaka na kuwaanzishia hako ka wimbo?
 
kama umeamua kuwa agaist na ccm lazima uanzie kwa nyerere.he is the axis of evil (mhimili wa uovu) i think he is in hell right now..........
 
Ni kweli. Mmojawapo wa hawa wawili ndiye aliye behind kampeini hii. La ajabu ni kuwa waling'ang'ania katika chama kilichoasisiwa na mtu huyo huyo wanayemkshaifu leo. Wangelikuwa na akili ni afadhali wangeanzisha chama chao tofauti na CCM ya Nyerere. Lakini wakati wa uchaguzi wanatumia kivuli cha Nyerere huku mitaani wakimkashifu.
Naomba msaada jamvini, who is behind this campaign to discredit Baba wa Taifa? 1.Is it Edward kwa vile viwango alivyoweka Mwl kamwe hawezi kuvifikia na tukisikiliza ushauri alioutoa hakuna atakayemchagua?2.Ni JK katika kufunika udhaifu wake na kuchochea udini?It has to be one of these two gentlemen au wote kwa pamoja.
 
Point ni kwamba, wimbo wa kumdhalilisha kiongozi mwenzio, unaachwa utumike miaka yote hiyo, huoni kama something is wrong hre. Dont treat the guy the same way as GOD.

pili, tujaribu kutofautisha mistakes, na mambo yanayofanywa kwa makusudi. huwezi kusema kulifumbia macho hilo ni mistakes, no hiyo ni dhamira.

wana JF, naomba ieleweke kwamba this is not a personel attack or hatred to the late old guy. kujua ulipojikwaa ndio mwanzo wa kutatua tatizo, kwa hiyo si kosa kuangalia tulijikwaa wapi.
Kwahiyo ulitaka aupige marufuku...??, Si ungekuja ukasema jamaa alikuwa Dikteta..., na ule wa nduli Iddi Amini vipi nao ungepigwa marufuku au wenyewe poa tu..
 
nyerere wa kazi gani tena! Yupo anabanikwa na roho yake ya ubinafsi na ubaguzi.
 
kwa hiyo unapendekeza nani awe baba wa taifa!? Na hiyo historia unapendekeza iweje.
Kwanini baba? Hili neno baba limekaa kikanisa kanisa. Mimi siliafiki hata kidogo. Ubaba wa Taifa ndio nini? Hatuna haja ya baba wa Taifa. Tanzania haikuasisiwa na Nyerere pekee ni makubaliano ya watu wawili Nyerere na Karume sasa inakuwaje baba awe Nyerere na Karume awe nani?
 
Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?

" Kambona , ah, ah!

Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"

Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.

MY TAKE:

Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.

Naomba kuwakilisha mada.

nadhani sasa tumeanza kutumia tumbo ktk kufiki kama vijana wa ccm wanavyoyanya ktk kujivua gamba.! wewe uanaye andika kuwa mwl na siasa za maji taka ni sawa na kumtukana driver baada ya kukufikisha salama kutoka safari ndefu.nchi inayumba na inchi ina sambaratika na mumebaki na siasa za kutumwa kumchafua mwl ili kuhalalisha udhaifu wa utawala wenu.mwl aliheshimika kwa kauli na kwa matendo yake.mwl iliheshimika hata na maadui wake.jf kennedy akimkaribisha mwl white house 1963, kennedy,alisema,your the most admired personality here in usa! wewe kapuku kwa kujua tu kutumia computer unadhiriki kutoa maneno ya dhihaki ya mtu huyu wa watu!
katika safari ile mwl alikuwa na kambona uanye msema.! mwl amejenga misingi ya uchumi, utawala,ninyi mmekuja kuibomoa! ningefurahi kama ungesema leo huyu mwisilmu wenu anafanya nini na hali ya umeme, ajira ,uchumi na mstakala wa taifa. rais pekee anaye kula nyama na wali katika ndege akiwa safarini.! rais pekee anaye sikiliza mziki akiwa safarini kwenda kuliongelea taifa un! mwl alikuwa aki soma akijielimisha na mambo ambayo alikuwa akiyaendeya kufafanya nje. hukusiliza mziki wala hakula wali zaidi ya kahawa tena isiyokuwa na maziwa.leo unamwita mtu wa maji taka.watawala wenu wameshindwa nchi ninyi mmekuwa wapiga debe wao! kumbuka na tena naomba mjielimishe kuwa mwl hachafuliwi na maneno yenu. hii nisawa na kossovo kujadili namna ya kuipiga marekani kwa smg...! utawala umeshindwa na umebaki na hofu ya kivuli cha mwl. hii nifaraja ya kweli kumbe pamoja na mwl kufariki 10 yrs ago bado anaishi miongoni mwetu.
 
Kwanini baba? Hili neno baba limekaa kikanisa kanisa. Mimi siliafiki hata kidogo. Ubaba wa Taifa ndio nini? Hatuna haja ya baba wa Taifa. Tanzania haikuasisiwa na Nyerere pekee ni makubaliano ya watu wawili Nyerere na Karume sasa inakuwaje baba awe Nyerere na Karume awe nani?
wewe nawe! Swali gani hili unauliza?! Kwani Tanganyika na zanzibar hujui nani aliolewa??? Nyerere ndiye baba banaa...!!!
 
Sina hakika kama J. K. Nyerere alipata kuusikia. Hata hivyo uliimbwa kambona KALOWEA kwa maana ya mlowezi kama tulivyowaita wazungu walowezi. Wapuuzipuuzi kama mwanzisha mada waliimba KAOLEWA. Nawasilisha!
 
Ushahidi uko wapi kwamba TICHA alitunga na kufundisha wimbo huo, kisha akashiriki kuimba. Nakumbuka wimbo huo uliimbwa miaka hiyo wakati wa kumlaani Banda wa Malawi na Makaburu wa Afrika Kusini. Kambona aliigia baada ya kulikimbia Azimio la Arusha ambalo leo wengi wanalilia, kuwa kuvunjwa kwake ndio chanzo cha ufisadi wa sasa wa wanamagamba. Kosa la Nyerere liko wapi?
 
Kwanini baba? Hili neno baba limekaa kikanisa kanisa. Mimi siliafiki hata kidogo. Ubaba wa Taifa ndio nini? Hatuna haja ya baba wa Taifa. Tanzania haikuasisiwa na Nyerere pekee ni makubaliano ya watu wawili Nyerere na Karume sasa inakuwaje baba awe Nyerere na Karume awe nani?

Kamwulize Mzee Mwinyi wakati angali hai, kwani ni yeye aliyempatia heshima hiyo ya Baba wa Taifa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom