Iwe sharti wanaume kuhamisha mali kwa watoto wa mwanzo kabla ya kuoa mke mwingine ili kuepusha dhuluma kwenye urithi baada ya kufariki

Unakuta mamtu mazima nayo yanagombania mali za urithi na watoto wadogo........hadi mnakuwa watu wazima mzee ameshawapa michongo yote au mmeshatafuta dili zenu, mali za urithi achieni watoto wadogo au zisimamieni kwa niaba yao.
Umeandika kitu usichokuwa na uelewa nacho, endelea kujifunza duniani kuna haki na kuna wajibu, haki ya mtu ni haki yake haijarishi umri, halafu unafuata wajibu.
 
Wewe ukihamisha ya kwako kuna shida?
 
Umeandika kitu usichokuwa na uelewa nacho, endelea kujifunza duniani kuna haki na kuna wajibu, haki ya mtu ni haki yake haijarishi umri, halafu unafuata wajibu.
Kuna zee moja lina zaidi ya miaka 70 lilikuwa linagombania eneo ambalo ni moja ya maeneo ya mzee wao na kijana mdogo wa miaka 25 ambaye ni mtoto wa uzeeni wa baba yake tena mbele ya baba yao...........aisee niliona kuna mamtu hayana akili kabisa, miaka 70 umeshindwa kutafuta maeneo yako hadi ugombee maeneo ya baba yako.
 
Wote wawili wana matatizo, huwezi kugombea mali ya mtu aliye hai, hakuna urithi wa mali ya mtu aliye hai.
 
Bakhresa ana akili nyingi pale kila mtoto kampa kampuni yake within the group.

Hamna kugombaniana mali kila mtu kapewa shavu mfano Yusuph yuko na mchongo wote wa majini na investment za Zanzibar ile mijumba na Hotel Verde.
Na wewe G-Funk! Umeishapewa mgao wako?
 
Nadhani ni wakati muafaka wa washua kujifunza kugawa mali zao kabla hawajadedi ili kuzuia vurugu.

Pia suala la pre-nup n muhim katika ndoa hasa hasa za uzeeni, maana hapo bi mdogo anaingia ndani akiwa anajua kbsa atakachoondoka nacho.

Sema kibongo bongo umwinyi mwingi! Wazee vichwa ngumu
 
Unakuta mamtu mazima nayo yanagombania mali za urithi na watoto wadogo........hadi mnakuwa watu wazima mzee ameshawapa michongo yote au mmeshatafuta dili zenu, mali za urithi achieni watoto wadogo au zisimamieni kwa niaba yao.
NDuGU Kama wewe hukuachiwa urithi acha wenye urithi wapambne.

Mali ya mdingi au Maza uziachie kienyeji tu ndugu kweli??

Wafaidi watu hta ambao hawahusik...

Utapenda hili litokee Kwa watoto wako huko mbele. ??
 
KWA SHERIA ZA TANZANIA, WATOTO HAWANA HAKI YA KURITH MALI ZA WAZAZI.

WAZAZI WANA WAJIBU WA KULEA MTOTO MPAKA PALE WATAKAPO WEZA KUJITEGEMEA.

HIVI HAO WATOTO WA MKE WA KWANZA WASIPO KUWA WA KWANGU?
 
KWA SHERIA ZA TANZANIA, WATOTO HAWANA HAKI YA KURITH MALI ZA WAZAZI.

WAZAZI WANA WAJIBU WA KULEA MTOTO MPAKA PALE TAKAPO WEZA KUJITEGEMEA.

HIVI HAO WATOTO WA MKE WA KWANZA WASIPO KUWA WA KWANGU?
Sheria za vijiweni huwa hazitambuliki mahakamani....
 
Mtu hawajibiki kufanya hivyo, inshort tafuta mali zako, hizo zake mwache azitumie atakavyo, si zake?! Wewe tafuta za kwako!!
 
Mtu hawajibiki kufanya hivyo, inshort tafuta mali zako, hizo zake mwache azitumie atakavyo, si zake?! Wewe tafuta za kwako!!
Ni kitu rahisi sana mkuu, kama hutaki kurithisha kitu nenda hospitalini kakate hio mishipa ya korodani, hutakuja kuwa na watoto, uta enjoy sana mali zako...
 
Tufanye kazi ,tuache kujiita watoto japo tuna umri wa kustaaf
 
Ni kitu rahisi sana mkuu, kama hutaki kurithisha kitu nenda hospitalini kakate hio mishipa ya korodani, hutakuja kuwa na watoto, uta enjoy sana mali zako...
Kuzaa na Kurithisha ni vitu viwili tofauti, ukizaa unawajibika kumtunza huyo mtoto kwa malazi, chakula, nguo, elimu na afya hadi atakapotimiza miaka 18. Zaidi ya hapo ni mapenzi yako wewe mwenyewe, ukitaka unaweza ukalilea jitu hadi likafika miaka 50, hukatazwi hayo ni mapenzi yako, lakini si lazima!! Hali kadhalika kumpa mtu urithi ingali upo hai si lazima, ni uamuzi wako!! Na ukifariki kuna miongozo ya nani atachukua nini na kwa kiwango gani..., ila, mtu chake, atakitumia atakavyo!! Wewe tafuta vya kwako!!!
 
Binafsi naamini ni busara kufa nikiwa nimewaachia watoto Mali....

sioni haja kwa nini watoto waje kutanga tanga baada ya Kifo changu ingali nilikuwa na nafasi ya kuwaachia kitu flani
Kuna muda Watoto wanazinguwa hadi kuna Madingi wengine wako radhi hata Mali zao zichukuliwe na Msikiti ama kanisa!!
 
Urithi uandikwe na kifanyike kikao kila mtu a ajue, kama kupinga, pinga wakati mwenye mali yu hai. Isiwe Siri.
 
Urithi uandikwe na kifanyike kikao kila mtu a ajue, kama kupinga, pinga wakati mwenye mali yu hai. Isiwe Siri.
Ukajiroga ukaandika urithi kwenye kikao kama hivyo na kila mnufaika akajua kwamba yeye anachukua nini, i assure you, humalizi mwaka utaondoka hapa duniani kwa namna ya kutatanisha, maana wataona kama wanachekewa kupewa urithi wao kwa kutokufa kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…