sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,028
Ishu kuu ni hawa mama wa kambo kuchota kila kitu huku, watoto wa mwanzo wanaambulia patupu...Je ni haki hawa mama wa kambo kuzoa kila kitu?
Binafsi nimeona kabla mwanaume hajaoa mwanamke mwengine (hasa hawa wazee wanao oa mabinti) , ingependeza haya mambo ya urithi yawe wazi ili kuepusha shari huko mbele, hii itakuwa kama bima ya kuwakinga watoto wa mwanzo kudhulumiwa urithi wao.
Siku hizi pia kumekua na trend ya wazee wanaoamua kuoa mabinti wadogo wakidhani wamepata kumbe wao ndio wamepatikana, binti anakua amehapiga hesabu zake anajua kabisa huyu mzee ni tajiri na havuki miaka 10 kwisha habari, Hapa binti atamzuzuzua kwa mapenzi moto moto huyo mzee mpaka mzee anajikuta anatoa mali zote, mzee akiwa mgumu basi anapigwa juju na malimbwata ya kumhamisha akili kushoto ili ahamishe mali kwa huyo binti.
nadhani kuwe na sheria za kuwalinda watoto wa mwanzo, kama baba anataka kuoa ni sawa haina shida lakini alazimishwe kuwajibika linapokuja swala la watoto wake wa mwanzo
Mifano ipo mingi sana ila hii ni michache.
1. Watoto wa marehemu Mengi wa mwanzo walivyotaka kunyimwa urithi, urithi karibu wote ungeenda kwa mama yao wa kambo, ilibidi wapambane sana kupata haki yao.
2. Watoto wa Marehemu Likwelile, ambao sasa wanapitia msoto, Mama yao wa kambo ni Vicky Kamata ambae kajihamishia uriithi huku watoto wa mwanzo wakiwa hoi bin taaban.
3. Watoto wa Marehemu Kimambi nao walipitia huu msoto, ilibidi wafike huko mahakamani wayamalize ila bila hivyo, mama wa kambo alikuwa anazoa kila kitu.
4. Nakumbuka mwenzetu tuliekuwa tunasomanae chuoni alikatisha masomo yake mwaka wa pili baada ya baba yake kufariki kwa sababu mali zote zilienda kwa mama yao wa kambo ambae aliacha hata kumlipia ada na kumpa hela za matunzo.
5. Mzee Mrema, pongezi kwako, nimeona habari unakaribia kuoa binti lakini jitahadhari please.
Urithi ni haki ya watoto, haki ya mtu ni haki yake haijarishi umri, Hata kama mtoto wa mwanzo anatembelea mkongojo na mtoto mwengine anatambaa, wote wana haki ya urithi wa mali za baba yao.