Iwe amri vijana wakitaka kwenda vyuoni wawe na ujuzi wowote wa stadi kazi, wahitimu wanaokosa ajira wasio na ujuzi wanatia aibu kushindwa kujitegemea.

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Haingii akilini hata kidogo mtu apambane zaidi kutafuta njia ya kujitegemea kwa kutegemea elimu ya chuoni impe ajira ambazo hazina uhakika huku hana ujuzi wowote wa kumfanya ajiajiri kwa uhakika hata akikosa ajira.

Mwenye ujuzi ni ngumu sana kulala njaa lakini mtu hata uwe na masters yako kama huna ujuzi na hujapata ajira unaweza kutia aibu na kudharaulika sana.

Mtu akiwa na ujuzi wa kuwa seremala, mama ntilie, fundi simu, fundi nguo, n.k, inakuwa rahisi kwake kujiajiri kabla ya kuajiriwa panapo majaliwa.

Elimu imeletwa kutukomboa, ni vipi mtu kwa kukaa darasani mpaka form 4 au form 6 kabla ya kuingia chuoni asijifunze chochote cha kujikomboa na kujipigania yeye kama yeye kabla hajaanza kusomea vya kuajiriwa serikalini au kwenye taasisi ambako ni sanda kalawe mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose ?

Chukulia tu mfano mtu ana ujuzi wa kupika chakula, ujuzi wa kawaida kabisa huu na wenye umuhimu mkubwa, mtu huyu hata akikosa ajira afungue kamgahawa kake utaweza kumlinganisha na yule waliehitimu pamoja hana ujuzi wowote kutwa nzima ku apply ajira ?? hapana!!

Leo hii kuna vijana wengi wanakimbilia vyuoni bila ya kuwa na ujuzi wowote ule, wakimaliza vyuo wanabaki nyumbani wakitegemea ajira ndio ziwachomoe maana wao kama wao hawana ujuzi wowote hasa katika stadi kazi, matokeo yake mtu anakaa nyumbani anageuka tegemezi, hii sio sawa jamani, watoto waandaliwe na vitu vya msingi kwanza kabla ya vingine
 
istockphoto-1218972142-612x612.jpg
 
Huna hoja kwani kuwa na ujuzi ndio kijana atapata hizo kazi sasa..
Au unadhani vipi ..
hata mafundi pia wanapata kazi sababu ya connection..

Ukweli ni kwamba serikali na jamii haikujiandaa kupokea idadi kubwa ya vijana kiasi hiki tulidanganywa kwa kuambiwa tuzae tu shule ni bure ila tulisahau tuna limited resources kwa sasa.
 
Mtu ni fundi seremala, mama ntilie, fundi simu, mpaka rangi, n.k. huyu hana haja ksubiri ajira anaweza kujiajiri kwanza kabla ya kusubiri ajira
 
Kwani zamani walikuwa wanaenda chuo na ujuzi? Hata kubeba zege mama ntilie ni ujuzi pia
Zamani ukiwa na diploma tu serikali inakutafuta uende kufanya kazi sio wewe uanze kutafuta, kwa sasa hali ni tofauti
 
Haufungui mgahawa kwa kuwa na ujuzi wa kupika bali kwa kuwa na MTAJI, migahawa yote unaona mjini mmiliki ni aliyekuwa na mtaji sio mpishi na wapishi unaowasema wanaujuzi wameajiriwa hapo na wengine wanasota kutafuta ajira za kupika
 
Back
Top Bottom