ITV mmewakosea sana watanzania

ITV mmewakosea sana watanzania

Sio hiyo tu! Hata lile tamko la Jaji Warioba kuwa nchini kuna njaa kwenye taarifa yao ya habari wameikata! ITV you can run but you can not hide!
time for 'njaa politics' is over. there was no news.
 
Baba magufuli wewe chapa kazi achana na mavuvuzela hayo ya cdm. Hawana kazi ya kufanya. Watabaki na gwajima wao na usanii wa kukataa kuhojiwa kwa tuhuma ya madawa ya kulevya kwa kufungua kesi mahakamani. ukituhumiwa na kuitwa kuhojiwa lazima uitikie wito na sio jeuri
 
Sasa kwan mkato wa lema ulikua na umuhimu gani kwa Taifa...hata hajasema cha maana
 
Kwa nini hamuanzishi kituo chenu, wazee wa mipango?!!
 
Si mhariri wa tanzania daima aandike kwenye front page ya gazeti lenu atoe nakala hata elfu kumi hiyo habari msome?
 
Sio kwamba mmngejiuliza kulikuwa na habari ngapi zenye maslahi kwa taifa kwa siku hiyo?
 
Wakuu ukweli ni kwamba kwa Tanzania ya sasa vyombo vya habari vipo ovyo sana na ni bora mitandao ya kijamii kuliko ivi ooh bora jf na mange
Kweli mlogolaje,kama walishindwa kuihoji NECTA kuhusu vyeti kama mali yao,kama walishwindwa kumhoji BASHITE kuhusu fa fa fa kama anaijua????? Hovyo sana hawa
 
Hill tulishalijua mapema ,ila ITV & IPP Media isiporekebisha hizi kasoro ndogo ndogo itakuja Julia kama mile kilio kikuu cha Diallo Anton na Sahara yake..
 
.

Mkutano wa Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (Mb) ambaye pia ni Waziri kivuli wa mambo ya ndani, habari yake sio tu kwamba haijapewa kipaumbele, Bali haijaoneshwa kabisa katika kituo cha televisheni cha ITV.Kuna taarifa kwamba kituo hicho na vingine vilionywa kutorusha taarifa hiyo.

Kituo cha televisheni cha ITV kimeonesha mapungufu makubwa mno kupata kutokea nchini Kwa Kutokuonesha habari ya Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani, ambaye alikuwa Magereza Kwa zaidi ya miezi minne kwasababu ya kesi za kisiasa.

ITV mmeitia doa tasnia ya habari, mmeonesha mapungufu makubwa katika kuiishi demokrasia ambayo watanzania wanaipigania, na mmesahau kwamba vyombo vya habari ni wadau wakubwa wa demokrasia kwani bila demokrasia hata uwepo wenu kama wanahabari utakuwa mashakani.

Watanzania hawajawahi kukata tamaa, jua liwake, mvua inyeshe, mabadiliko ya kisiasa tutayafikia lazima, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo yote.
Kwani Lema Criminal ndio nani???
 
Huko tuendako watu watutumia zaidi mitandao ya kijamii kupashana habari kuliko vyombo hivi vya habari ambavyo vinaonekana kutokizi malengo.

Media hizi zitaathirika kama jinsi mashirika ya Posta dunani yalivyoathiriwa na ujio wa simu za mikononi kiasi kwamba utumaji wa barua siku hizi umepungua sana na wamebakiwa na kazi ya kushughulikia barua za kikazi tu(za maofisi,n.k) .

Huko tuendako watu watatumia zaidi clip za mitandaoni na maandishi kupitia mitandao kupashana habari kama ilivyo sasa.
Anzisheni tv yenu
 
Sio hiyo tu! Hata lile tamko la Jaji Warioba kuwa nchini kuna njaa kwenye taarifa yao ya habari wameikata! ITV you can run but you can not hide!
Itv kwa kuwa ni ya mchaga mlidhani ataiendesha kikabila!!? Nyumbu bana!
 
Back
Top Bottom