Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
.
Mkutano wa Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (Mb) ambaye pia ni Waziri kivuli wa mambo ya ndani, habari yake sio tu kwamba haijapewa kipaumbele, Bali haijaoneshwa kabisa katika kituo cha televisheni cha ITV.Kuna taarifa kwamba kituo hicho na vingine vilionywa kutorusha taarifa hiyo.
Kituo cha televisheni cha ITV kimeonesha mapungufu makubwa mno kupata kutokea nchini Kwa Kutokuonesha habari ya Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani, ambaye alikuwa Magereza Kwa zaidi ya miezi minne kwasababu ya kesi za kisiasa.
ITV mmeitia doa tasnia ya habari, mmeonesha mapungufu makubwa katika kuiishi demokrasia ambayo watanzania wanaipigania, na mmesahau kwamba vyombo vya habari ni wadau wakubwa wa demokrasia kwani bila demokrasia hata uwepo wenu kama wanahabari utakuwa mashakani.
Watanzania hawajawahi kukata tamaa, jua liwake, mvua inyeshe, mabadiliko ya kisiasa tutayafikia lazima, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo yote.