Kapinga
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 727
- 18
Mimi nadhani hakuna haja ya kupiga kelele na kulalamika, ITV haiendeshwi juu ya sheria na taratibu za nchi. Kama ilikubali masharti ya kufanya shughuli zake ndani ya Tanzania, basi haina budi kufuata taratibu hizo. Na kama wataonekana wamekosea ni imani yangu kuwa hatua zifaazo za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Lakini hata hivyo ITV inayo haki ya kupinga adhabu yeyote katika vyombo au mamlaka husika ya kisheria.
Sikubaliani na hii tabia ya Mengi kuanika hizo barua kwa kutaka kuonewa huruma, atumie mawakili wake na awaache wafanye kazi zao kitaalam bila ya kuanza kuanika hizo correspondences za mawakili na hizo taasisi zingine. Kwa kifupi Mengi anaifanya kazi ya mawakili wake kuwa ya kisiasa zaidi na kuingiliwa na influences za public.
Mkuu unalalamika kitendo cha barua kufika JF au yaliyosemwa kwenye hizo barua?
Analysis yako ya hizo barua ni hipi exactly?...zisome alafu tueleze kama mengi anaomba huruma!
Umejiuliza kama TCRA wametuma TBC1 barua kuhusu rostam? Kama jibu ni NO! Je bado Mengi anaomba huruma?