ITV kuna ubaguzi kwenye utoaji habari?

ITV kuna ubaguzi kwenye utoaji habari?

Mleta mada ni chuki binafsi zinamsumbua hana hoja kwani kuna mtu analazimishe kuangalia ITV?
 
Sasa kama mikoa mingine hawapeleki matangazo ya vifo watawalazimisha? Utamadun wa kutangaza vfo upo kanda hyo ndo mana unackia matangazo ya huko peleka lako kama halitasomwa ndo uje useme hayo hapa

Au mwambie afe yeye tutampelekea tangazo....
 
"Ndg Mushi wa kilaracha anasikitika kutangasa kifo ndg Macha wa Rombo, habari ziwafikie, Chuwa, Tarimo, Shayo, Lema, Aikaeli, Manka, Kekuu, Haika, na Mareale wote wanapatikana Kilimanjaro na Arusha" na ndg walioko Kimara bucha dsm.

ha ha ha ha umenivunja mbavu zangu aisee hii ni hatari sana
 
Acha Roho Mbaya Wewe,Kama vipi hamia televisheni nyingine,hulazimishwi kuangalia ITV
 
Kuanzishwa kwa Azam na ufunguzi wa studio mpya itakuwa ni raha kwangu baada ya kuishia kulalama sana ITV huku wakiweka pamba masikioni, suala la kuibagua mikoa flani kwenye habari zao na kuibeba mingine kila leo halivumiliki, sielewi ni mmiliki ama ni uongozi lakini mnafanya ubaguzi wa wazi mno.

Haiwezekani habari husika mkoa Fulani haioneshwi makusudi zaidi ya Mara kadhaa wakati tayari inatokea pale chini ya kioo kwa habari ya Sikh hiyo, ni ubaguzi. Kutwa Isidingo na movie?

Angalieni wenyewe kama hamuwezi kutengeneza vipindi vya kijamii kaeni na Wafilipino wenu..
ITV is not a national TV so, the owner can do whatever he wants, inter-alia, the owner is not wantonly prejudicing certain parts of Tanzania, in contrast, he is exercising his rights.
 
Hee maajabu, kumbe hata hujui kwa nini Chadema mnamuhusisha Mungu katika kueneza chuki na machafuko? Inashangaza kuona mtu kama wewe unajiuliza swali hili badala sisi ndio tukuulize. Usishangae sana kijana, mleta mada ni miongoni mwa watu walioiga staili yenu ya kumuhusisha Mungu katika kueneza wivu, chuki, machafuko na visasi.
The thread is about ITV and not a political party as you construed above.
 
Ujinga nikitu kibaya sana Yooote haya ni upumbavu na ujinga.

Kila mmoja wetu nyumbani kwakwe anatune nakuangalia ile kitu roho yake inapenda.

Kwasisi wapenzi wa soka tuko radhi kulipa Tsh. 142,000 na tumeshatangaziwa mwezi wa nne inapanda itakuwa zaid ya Tsh 160,000/month.

Kwasababu ndo raha yetu ilipo tutalipa na wapenzi wa usanii na maigizo watalipia zao. Nawewe lipia inayokufaa. usitushirikishe kwenye starehe zako?

kuleta lawama hapa zisizo na msingi nimatunda ya kampeni za udini 2010, ccm wametufikisha pabaya. ujinga na udini kila eneo hatakama mhusika anahiari bado atafanya uchochezi.
 
The thread is about ITV and not a political party as you construed above.

Niliyemjibu anajua why nimemjibu hivyo, so kama vitu huvielewi ni bora ukae kimya. Mie siyo mjinga hicho nikashindwa kujua hii mada siyo ya kisiasa.
 
ITV ni Televisheni ya TAIFA...inakubalika kila kona na kada zote..
 
Acha Roho Mbaya Wewe,Kama vipi hamia televisheni nyingine,hulazimishwi kuangalia ITV

Unataka tuhame Mara ngapi mkuu? na wewe unakaribishwa kwenye vilivyo na ubora
 
Mleta mada mpaka sasa umejiridhisha kwamba umesukumwa na chuki.
Hivi watanzania nani aliye tuloga? Television na radio zinazoendeshwa kwa kodi yako unafurahishwa na matangazo yake? Ningekushukuru sana kama ungelalamikia vipindi vya hovyo na matangazo au habari za UPENDELEO, USIRI na UONGO WA WAZI vinavyo rushwa na vituo vinavyo tafuna kodi yako nami, badirika! Vinginevyo una chuki binafsi su maslahi ya kibiashara na ITV. Kama ulivyo ambiwa na wana jamvi wengine, Subiri katuni na nyimbo za wenyewe hao ulio wasifia.

Acha wehu,una presha kama mja mzito.Kwani kumilikiwa na mtu ndo unapoteza haki ya mawazo na maoni? sasa sie watizamaji tusipitoa maoni mnataka sokwe ndo wakatoe maoni badala yetu watizamaji ..kwani ni taasisi ngapi tena za kibnafsi ukifika pale wanaruhusu utoe maoni/ ushauri kwenye boksi lao la maoni ama na wewe ndo wale waoga wa kukosoa kila kitu ni twende tu liwalo na liwe.Mile nawapenda ITV na ndo maana nawasahauri,Sikh zote in bora useme ukweli kwa mhusika hats kama anakuchukia kuliko kusema pembeni ama kusemea uvununi,na huo ndo upendo maana ashakumu ni ushauri tu wala so ugomvi/ matusi,wachache wasioelewa ndo wanaweza kuchukulia ushauri kuwa ni matusi
 
Awa ITV habari zao nyingi ni moshi na arusha...mara wahoji wamasai mara wanazindua saccos kishimundu. Huwezi kuona Mtwara au Njombe kibwegebwege.

Kulikuwa hakuna maendeleo..afadhali ya mtwara sasa hivi kwa sababu ya gesi....HUO NDIO UKWELI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom