ITV kuna ubaguzi kwenye utoaji habari?

ITV kuna ubaguzi kwenye utoaji habari?

Sikiliza radio one matangazo ya vifo utajua radio ya wapi hiyo,

Acheni upimbi nyie matangazo ya vifo huwa yanalipiwa na huwa yanapelekwa na ndugu wahusika sasa wewe unataka ukifiwa wakufuate nyumbani kwako kuja kuchukua habari kati ya maoni mabovu na ya husda kuwahi tokea humu jf hovyo kabisa.
 
Unaelewa maana ya Habari? Kuna mikoa hakuna habari mpya labda makala maana ilishajifia mfano Lindi,

Kuanzishwa kwa Azam na ufunguzi wa studio mpya itakuwa ni raha kwangu baada ya kuishia kulalama sana ITV huku wakiweka pamba masikioni, suala la kuibagua mikoa flani kwenye habari zao na kuibeba mingine kila leo halivumiliki, sielewi ni mmiliki ama ni uongozi lakini mnafanya ubaguzi wa wazi mno.

Haiwezekani habari husika mkoa Fulani haioneshwi makusudi zaidi ya Mara kadhaa wakati tayari inatokea pale chini ya kioo kwa habari ya Sikh hiyo, ni ubaguzi. Kutwa Isidingo na movie?

Angalieni wenyewe kama hamuwezi kutengeneza vipindi vya kijamii kaeni na Wafilipino wenu..

Labda watuletee kule ukerewe mtoto atafuna na mamba ndani ya beseni la kuogea, sumbawanga bibi akutwa juu ya dari akiwa mtupu, na huko simiyu kuna kijiji huwa usiku kinageuka na kuwa New York.
 
"Ndg Mushi wa kilaracha anasikitika kutangasa kifo ndg Macha wa Rombo, habari ziwafikie, Chuwa, Tarimo, Shayo, Lema, Aikaeli, Manka, Kekuu, Haika, na Mareale wote wanapatikana Kilimanjaro na Arusha" na ndg walioko Kimara bucha dsm.

Hahahaaaaaaa,kwani wachagga wengi wanaishi kimara kwa hapa dar?
 
Hata kama wana dosari zao lakini afadhali kuliko itv.azam ni wasikivu watajirekebisha
 
Rweye sijaona hoja yako ya msingi kabisa!
Hivi unafikiri Azam Tv imeanza kuonekana leo? Kilicho fanyika ni uzinduzi wa studio za kisasa kabisa lakini Azam Tv inaonekana kitambo sema sababu si channel kati ya zile Tano za muhimu labda waiweke!

Kusema kweli sijawai kuona huo ubaguzi unao uongelea hapa kabisa na tunatakiwa kujua si lazima ITV wareport kila habari na muda hauwezi kitosha..kwani channel zingine kama walionesha kuna tatizo gani? Kwani habari hufanana kila channell? Kama sehemu fulani likitokea tukio wasilichukue kwa kuwa ni mkoa fulani?

Kwakweli sijaona hoja yako?

So unaangalia taharifa ya habari SAA 2 jioni mkuu? pale chini si huwa kunapita vifupi vya habari za siku hiyo? namaanisha ilo,sasa imetokea Mara kadhaa usipokuwa makini no vigumu sana kugundua.Sasa unaona habari chini inapita lakini mwazo mpaka mwisho hiyo habari haitasomwa,zinatoka eneo Fulani,Leo alafu wiki ijayo tens,si lazima ujiulize? kwa mfano kwanini wanaiweka alafu haisomwi,OK,mbona Hamna kumradhi? unabaki na sintofahamu.Naelewa wana uadilifu lakini kwanini hivi alafu kwanini waliiweka chini na sasa mbona hawatoi maelezo? in bahati mbaya ama in makusudi,hapa hatuwachukii ila in sehemu ya wao kuadmitt na kujiweka sawa,basi.
 
Last edited by a moderator:
Bakhressa alivyokibaraka wa ccm atadhubutu kuikosoa ccm na serikali yake? time will tell, itv daima!
 
Awa ITV habari zao nyingi ni moshi na arusha...mara wahoji wamasai mara wanazindua saccos kishimundu. Huwezi kuona Mtwara au Njombe kibwegebwege.
 
Swali laleo la kumepambazuka......?
 

Attachments

  • 1425728580259.jpg
    1425728580259.jpg
    51.5 KB · Views: 290
.. Ngongoseke hata wewe hujakatazwa kupeleka matangazo radio one acha wivu wa kike
 
Last edited by a moderator:
Naomba elimu.....kwa nini ITV inaonekana ktk Azam kingamuzi lakini Azam tv haionekani katika kingamuzi cha ITV yaani DIGITEK
 
Awa ITV habari zao nyingi ni moshi na arusha...mara wahoji wamasai mara wanazindua saccos kishimundu. Huwezi kuona Mtwara au Njombe kibwegebwege.

Kwa dharau wanasema eti huko hamna habari mkuu,ila kwingine ndo kuna habari ..kweli nimeamini akutukanaye hakuchagulii tusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom