ITV kuna ubaguzi kwenye utoaji habari?

ITV kuna ubaguzi kwenye utoaji habari?

Kuanzishwa kwa Azam na ufunguzi wa studio mpya itakuwa ni raha kwangu baada ya kuishia kulalama sana ITV huku wakiweka pamba masikioni, suala LA kuibagua mikoa flani kwenye habari zao na kuibeba mingine kila leo halivumiliki, sielewi ni mmiliki ama ni uongozi lakini mnafanya ubaguzi wa wazi mno.

Haiwezekani habari husika mkoa Fulani haioneshwi makusudi zaidi ya Mara kadhaa wakati tayari inatokea pale chini ya kioo kwa habari ya Sikh hiyo,ni ubaguzi. Kutwa isidingo na movie? Angalieni wenyewe kama hamuwezi kutengeneza vipindi vya kijamii kaeni na wafilipino wenu

mkuu punguza kulalama. kama unaona ITV kwani usihamie TBCCM, hasa chanel ya TBC2?
 
Watu wengine kwa chuki bhana sasa kisa bharesa hana c mzawa ndo unaiona ya maana sana asee fkria mh. kaenda kuzndua azam tv ila ukiangalia TBC n ya taifa ina kila miundombinu ila habar inarusha kisiasasiasa tu huoni hlo unaona la ITV ubaguzi uliopo kchwani mwako unahtaj maombi:flypig::flypig:
 
Unaelewa maana ya Habari? Kuna mikoa hakuna habari mpya labda makala maana ilishajifia mfano Lindi,

Na hapo ndo hoja yangu ilipo mkuu,hauwezi kudharau maeneo kiasi hicho na hauwezi ukawa unaelewa maana ya habari usione kupata habari kutoka Lindi,kwani huko Lindi wanaishi sokwe? kwani huko hamna taasisi za serikali,hakuna masoko,hakuna bidhaa,hakuna wanaopata ajari na maafa? unamaanisha hakuna shida na raha Kule isipokuwa maeneo mengine ya nchi? anyway,hatuhangaiki nao tens na habari zao
 
Lazima tukubali kuna mikoa iko active na inamatukio meng zaid kuliko mingne
 
Sijui kwanini tunamhusisha Mungu katika chuki na wivu wetu

Hee maajabu, kumbe hata hujui kwa nini Chadema mnamuhusisha Mungu katika kueneza chuki na machafuko? Inashangaza kuona mtu kama wewe unajiuliza swali hili badala sisi ndio tukuulize. Usishangae sana kijana, mleta mada ni miongoni mwa watu walioiga staili yenu ya kumuhusisha Mungu katika kueneza wivu, chuki, machafuko na visasi.
 
Huo ni utashi wa mfiwa kwasababu matangazo ya vifo hupelekwa na wafiwa kwa gharama zao cyo bure. Yangekuwa yanasomwa kwenye taarifa ya habari ungesema yanakusanywa kibaguzi kwani taarifa ya habari hailipiwi. Watu wa kilimanjaro na Arusha hususani wachaga wana utamaduni wa kutangaza vifo redioni sana huwezi linganisha na wamakonde au wakurya....

Mtoa mada ni mkazi wa mkoa gani hapa Tanzania ambapo habari zenu hazifiki kwenye luninga?

......umesahau Wahaya
 
mkuu punguza kulalama. kama unaona ITV kwani usihamie TBCCM, hasa chanel ya TBC2?

Mkiwa kwenye jamii ya watu wanaopenda use me mazuri tu na ukijaribu kuongelea kero ama mapungufu unaonekana mpuuzi matokeo yake yatawarudi nyinyi wrnyewe kama jamii.Sasa mnataka hawa watu was media watambueje umahiri na madhaifu yao kama tu eti mnaogopa kusema? hiyo nidhamu na unafiki wa uoga mnaoulea ndo vilio vyenu Leo watanzania mlio wengi,mnaogopa watu watanionaje
 
"Ndg Mushi wa kilaracha anasikitika kutangasa kifo ndg Macha wa Rombo, habari ziwafikie, Chuwa, Tarimo, Shayo, Lema, Aikaeli, Manka, Kekuu, Haika, na Mareale wote wanapatikana Kilimanjaro na Arusha" na ndg walioko Kimara bucha dsm.

we jamaa bwana daah teh teh teh!
 
ITV Ni tumaini letu kwa habari na matukio...inaaminika na wasomi, na wananchi wote ukipita kijiweni mida ya saa mbili usiku unakuta wanaitazama ITV... Mimi ni wa nyanda za juu kusini mbn cioni huo ubaguziii?? bravoo ITV
 
"Ndg Mushi wa kilaracha anasikitika kutangasa kifo ndg Macha wa Rombo, habari ziwafikie, Chuwa, Tarimo, Shayo, Lema, Aikaeli, Manka, Kekuu, Haika, na Mareale wote wanapatikana Kilimanjaro na Arusha" na ndg walioko Kimara bucha dsm.

Kilaracha ni wapi?
 
Nadhani itv ni kituo binafsi na mmiliki kawekeza fedha zake binafsi. Tutumie muda kuichambua tbc ambayo sisi ndo tunailipia kodi, mtu binafsi ana mitazamo yake binafsi na malengo binafsi. Haitasaidia kulalamika humu. Tv yetu ni tbc sio itv wala azm tv. Nawaza tu
 
Lazima tukubali kuna mikoa iko active na inamatukio meng zaid kuliko mingne

Sikiliza mkuu usiwe na haraka,Luna habari zinapita pale chini kama habari muhimu za Sikh hiyo ama highlights alafu unagundua kati ya hizo zipo zinasomwa na zingine hazisomwi kana kwamba hazikuwepo kabisa ila ukiangalia ile strip inayozunguka ile habari IPO,mpaka habari inaisha hairushwi na hakuna cha kumradhi wala nini,inapigwa chini kimyakimya as if Sir watizamaji hatuko smart na kinachotokea wakati huo ..hiyo ndo hoja yangu
 
Kuanzishwa kwa Azam na ufunguzi wa studio mpya itakuwa ni raha kwangu baada ya kuishia kulalama sana ITV huku wakiweka pamba masikioni, suala LA kuibagua mikoa flani kwenye habari zao na kuibeba mingine kila leo halivumiliki, sielewi ni mmiliki ama ni uongozi lakini mnafanya ubaguzi wa wazi mno.

Haiwezekani habari husika mkoa Fulani haioneshwi makusudi zaidi ya Mara kadhaa wakati tayari inatokea pale chini ya kioo kwa habari ya Sikh hiyo,ni ubaguzi. Kutwa isidingo na movie? Angalieni wenyewe kama hamuwezi kutengeneza vipindi vya kijamii kaeni na wafilipino wenu

Hauna mantiki chuki binafsi inakutafuna na wewe anzisha yako uwe unatangaza habari uzipendazo.
 
"Ndg Mushi wa kilaracha anasikitika kutangasa kifo ndg Macha wa Rombo, habari ziwafikie, Chuwa, Tarimo, Shayo, Lema, Aikaeli, Manka, Kekuu, Haika, na Mareale wote wanapatikana Kilimanjaro na Arusha" na ndg walioko Kimara bucha dsm.

Uuuwi,ha,ha,ha,ha,umetisha Mkuu.
 
na hawa wasiporeport sijui utakuja na jipya gani
 
Ubaguzi hauna nafasi bali kuongezeka kwa media ni swala la msingi saaaana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom