Waislamu 11 Wakamatwa Nigeria kwa kutokufunga Mfungo wa Ramadhani

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Polisi wa Kidini nchini Nigeria wamekamata watu 11 siku ya Jumanne kwa kuonekana wakila chakula mchana katika mwezi wa Ramadhani.

Watu hao wamekamatwa katika jimbo la kaskazini la Kano.

Kano ina idadi kubwa ya Waislam, ambapo sheria ya kidini – Sharia- inatumika pamoja na sheria za kawaida za nchi.

Polisi wa Kiislam, maarufu kama Hisbah, hufanya misako katika maeneo ya chakula na masoko wakati wa Ramadhani.

Wanaume 10 na mwanamke mmoja waliokamatwa, waliachiliwa huru baada ya kuapa kuwa hawatoacha kufunga bila sababu muhimu.

“Tulikamata watu 11 siku ya Jumanne, akiwemo mwanamke mmoja muuza karanga aliyeonekana akila na watu wakatujulisha,” amesema msemaji wa Hisbah Lawal Fagge, akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC.

“Wengine 10 ambao ni wanaume walikamatwa mjini karibu na masoko ambapo kuna shughuli nyingi.”

Ameongeza kusema msako utaendelea lakini amesema wasio Waislam hawahusiki na msako huo.
 
Huko Nigeria wanazingua kwani wengi wao wanashinda na njaa mchana wakidai wamefunga wakati matendo mengine ovu wakiendelea nayo.Kufunga kwao ni kwakuangaliana binadamu na binadamu lakini si kwa Mungu.Yaan unakuta mtu anaogopa asionekane na wenzake na siyo kumuhofia Mungu.
 
Polisi wa Kiislamu katika jimbo la kaskazini la Kano nchini Nigeria waliwakamata Waislamu 11 Jumanne ambao walionekana kula chakula wakati wa mwezi mtakatifu wa Ramadhani.

Kano ina idadi kubwa ya Waislamu, ambapo mfumo wa sheria ya Kiislamu - Sharia - unafanya kazi pamoja na sheria za kisekula.

Polisi wa Kiislamu, wanajulikana sana kama Hisbah, hufanya msako katika mikahawa na masoko kila mwaka wakati wa Ramadhani.

Wanaume kumi na mmoja na mwanamke mmoja walitolewa baada ya kuapa kwamba hawatakusudia kukosa kufunga tena.

"Tulikamata watu 11 Jumanne ikiwa ni pamoja na mwanamke aliyekuwa akiuza karanga ambaye alionekana akila kutoka kwa bidhaa zake na watu wengine wakatufahamisha," Msemaji wa Hisbah Lawal Fagge

"Wanaume wengine kumi walikamatwa katika mji huo hasa karibu na masoko ambapo kuna shughuli nyingi."

Aliongeza kuwa operesheni za ukaguzi zitaendelea lakini akasema kuwa wasio Waislamu walikuwa hawajumuiki.

BBC

=====================
The Islamic police in Nigeria's northern state of Kano arrested 11 Muslims on Tuesday who were seen eating food during the Ramadan fast.

Kano has a majority Muslim population, where an Islamic legal system - Sharia - operates alongside secular law.

The Islamic police, widely known as Hisbah, carry out searches of eateries and markets every year during Ramadan.

The 10 men and one woman were released after swearing an oath that they would not purposely miss a fast again.

"We got 11 persons on Tuesday including a lady selling groundnuts who was seen eating from her wares and some persons alerted us," Hisbah spokesman Lawal Fagge told the BBC.

"The other 10 were men and were arrested across the city especially close to markets where a lot of activities happen."

He added that the search operations would continue but said that non-Muslims were exempt.
 
Back
Top Bottom