Itakuwaje Lowassa akifukuzwa CCM, CHADEMA watampokea?

Itakuwaje Lowassa akifukuzwa CCM, CHADEMA watampokea?

Hakuna mtu anayeweza kusema lolote kwa EL, ccm yote ni mali yake na wengine wote ni watumwa wake tu, wewe hukumbuki walikuja na sera za kuvua gamba huoni EL anavyowavua magamba mawaziri? Kama kuna kidume ccm athubutu kumfukuza EL uanachama.
karibu tena kwa mjadala leo
 
Acha kupotosha umma, Lowasa sio waziri mkuu mstaafu, ni waziri aliyejihudhuru kwa matumizi mabaya ofisi ya umma, huyo ndiye mzee wa richmundi, kuhusu kwenda Chadema, unaota ndoto za alinacha, hiki ni chama cha watu makini.
tehe tehe tehe
 
Nilishawahi kusikia kuwa jeuri ya EL ni kwamba anawatishia eti wakimtema, ataenda upinzani. Tusije tukawa mbulula tukampokea CCM wakapata credit. Huyu jamaa nadhani ndio katuletea matatizo ya umeme kwa maslahi yake binafsi. Umeme unapanda mara dufu tunahoji tukiwa bar afu tunatulia (tuingie barabara kidogo-tuonyeshe anger). Wenzetu Kenya walipandishiwa bei ya chakula, wakaingia barabarani na mabango, tumekuwa wabinafsi sana.
Lowassa leo anazunguka nchi nzima na gia yake kubwa ni ruswa kwa watanzania maskini na bodaboda. Na matatizo mengi tunayoyapata, kielimu(shule za kata), kiuchumu (ki-umeme) yalikuja akiwa PM, leo aje upinzani tumpokee. Tutakuwa waroho wa madaraka.


hahahahahahah makubwa hayo! sijui mnajisikiaje hapa
 
Ngoja nifanye reference ya matukio ya nyuma ya uzi huu ili waje waone madudu yao ninapo waunga mkono:

EL ni kichwa na baba wa sisiemu hawezi fukuzwa kamwe [emoji23]

EL ni fisadi papa asiesafishika CDM aje kufanya nini? hatuna sabuni ya kumsafisha [emoji1]
 
Msimamo wangu haujawai kufa kuwa Lowassa ,Kikwete, Mkapa ni mafisadi papa wa nchi hii mpaka naenda kaburini ......

I will stand for that.......
 
Back
Top Bottom