Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Kwa kiwango kikubwa Israel yote inalishwa na shughuli za kilimo na ufugaji zinazofanyika kusini ya nchi hiyo na mpakani na Gaza ambazo asili ya ardhi hizo zenye rutuba zilitwaliwa na wayahudi waliovamia mpaka kufikia 1948. Na hata mashamba ya mitende ya kaskazini ya Israel yapo kwenye maeneo ya mabedui wa kiarabu waliozingirwa na uvamizi huo.
Kabla ya mwaka 1990 matajiri wa kiyahudi walitumia nguvu kazi kutoka Gaza kwa shughuli zote za mashambani. Pale wapalestina hao walipojuwa wanatumikishwa kwenye ardhi walizofukuzwa wazazi wao na kuanza mapambano ndipo Israel ilipoanza kuwawekea vikwazo na vizuizi vya ukaguzi na pia kuanza kufikiria kutafuta wafanyakazi kutoka mataifa mengine.
Kwa ujumla Israel inahitaji watu 300,000 kufanya kazi kwa gharama ndogo kwenye mashamba hayo.Zaidi ya nusu bado waliendelea kuwa ni wapalestina maskini kutoka Gaza ambao kila asubuhi huingia eneo hilo kwa vikwazo vingi na ukaguzi wa hali ya juu wakienda kujitafutia riziki zao.
Pamoja na wapalestina hao Israel imeweza kuwashawishi raia wengi kutoka nchi maskini kwenda nchini humo kufanya kazi za shambani kwa gharama za chini sana.Moja ya taifa lenye idadi kubwa ya wafanyakazi wa mashambani ni Thailand.
Wataiand pamoja na kukubali kufanya kazi kwa gharama ndogo lakini husaini mikataba ya muda mfupi inayowakataz kufanya mahusiano yoyote ya kimapenzi na wenyeji au kuanzisha familia nchini Israel.
Kutokana na kukua kwa uchumi wa viwanda wa Israel idadi kubwa ya raia wake wamekuwa wakiingia kufanya kazi za kiofisi na kupanua zaidi hitajio la wafanyakazi kutoka mataifa maskini.Hali hiyo imepelekea Israel kufikiria kupata raia wa mataifa mengine ya kiafrika kwa bei rahisi kwa kisingizio cha kwend kuchukua mafunzo ya kilimo.
Baada ya shambulio la kushtukiza la Hamas hapo oktoba 7 mwaka huu 2023 idadi kubwa ya wafanyakazi wa mashambani wa Thailand waliathiriwa kwa kuimizwa,wengine kufariki dunia na waliobaki hai kuamua kurudi kwao wakiazimia kutokurudi tena kwa shughuli za kilimo huko Israel.
Pengo la wafanyakazi hao lingezibwa na vibarua kutoka Gaza ambao wanapakana na maeneo hayo lakini Israel imeingiwa na hofu na watu hao wote na hivyo kuamua kuwarudisha makwao pamoja na vipigo na fedheha na bila ya hata kuwalipa ujira wao waliokwisha kuutumikia.
Hali hiyo imesababisha mashamba kutokupata huduma na hivyo mazao kuharibika na magugu kuota nafasi yake.Kwa vile mazao hayo hulisha karibu Israel yote kutokupata huduma kumepelekea kuzuka kwa hofu ya njaa nchini humo.
Mabanda ya mifugo ambayo ni moja ya nguzo za uchumi wa Israel yamebaki na ngombe wasiokuwa na watu wa kuwakatia majani na kuwalisha pamoja na kuwapa matunzo yake. Wale wachache waliobaki wamekuwa wakitoa maziwa mara mbili tu kwa siku badala ya mara tatu kabla ya oktoba saba.
Kwa kujua athari za kiuchumi za kukimbia na kufukuzwa kwa wafanyakazi wa bei rahisi,vikundi vya raia vimekuwa vikihamasishana kufanya kazi hizo bila mafanikio kwani wengi wao hawana nguvu na ari ya kufanya kazi hizo ngumu za mashambani.