Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,192
- 10,926
Matumaini ya kupatikana nafuu kwa wapalestina karibia milioni 2 na nusu wanaoangamia kwa vita na njaa yameanza kupatikana.
Katika mazungumzo ya kusitisha vita baina ya Israel na Hamas kila upande umelegeza masharti yake ili kufikiwa kwa lengo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zinazovuja kutoka kikao cha upatanishi huko Doha nchini Qattar,kimsingi Israel imekubali sharti la Hamas la kuachiwa wafungwa wa kipalestina baina ya 700 mpaka 800 kati ya maelfu walioko kwenye magereza ya Israel.
Sharti jengine muhimu la Hamas la kuruhusiwa kurudi watu kwenye maeneo yao hasa Gaza ya kaskazini nalo limekubaliwa.
Hata hivyo huenda Israel ikaunganisha na kikwazo cha umri na jinsia za hao watakaoruhusiwa kurudi maeneo kwa hofu ya kuruhusu wapiganaji watakaotia nguvu wenzao ambao bado Israel inaendelea kupambana nao.
Kwa upande wa Hamas nao wamelegeza sharti la kutaka Israel iondoshe majeshi yake yote kutoka Gaza.