Is God fair ?

Is God fair ?

Total contradiction. Roho ndiye alitundikwa msalabani?

Aliyetundikwa ni mwili wa Yesu,Immanuel wa Nazareth,ila roho yake haikufa,na ndio maana alisema,mikononi mwako baba,naiweka roho yangu

Tena akamwambia yule mwizi aliyetubu kuwa,kwa hakika usiku wa leo tutakuwa wote peponi...need i say more Mr Kiranga?
 
Sasa ndiyo inahusiana vp mkuu?
Bado sijaona cha maana ktk hoja yako hebu weka sawa.

Kuhitaji kuumba kitu ni kukosa ukamilifu.

Unahitaji kujenga nyumba kwa sababu unaona kuna hitaji la makazi.

Unahitaji kupika chakula kwa sababu kuna njaa.

Unahitaji kufuma labda pengine uko bored, kuna kitu kina miss, unaumba kitu.

Huyu mungu mkamilifu imekuwaje mpaka akahitaji kuumba?

Alikuwa lonely akataka tumpe kampani?
 
Kukamilika hakumfungi mtu kufanya mambo mengine
Mungu aliamua kufanya uumbaji si kwa sababu hajakamilika,aliumba ili afurahie kazi ya mikono yake....!
 
Una tatizo la kutojibu hoja za msingi, badala yake unazikwepa kiujanja ujanja.

Tumekustukia.

Hoja ipi ya msingi sijaijibu? Hebu niulize hapa kweupeeeee watu wanasoma.

Mimi hoja zangu za msingi ambazo hazijajibiwa hizi hapa.

1. Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu wenye kuwezekana mabaya na maovu wakati uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya na maovu hayawezekani alikuwa nao?

2. Kwa nini mungu mwenye ukamilifu wote aumbe chochote? Kutaka kuumba ni kukosa ukamilifu, utasemaje mungu mkamilifu kaona haja ya kuumba wakati haja ya kuumba ni kukosa ukamilifu?

3. Imekuwaje mungu mjuzi wa yote na muweza yote akapanga mambo halafu akaghairi? Alivyoanza kupanga si alijua yote, kaghairi vipi tena?

4. Imekuwaje mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote akakasirika? Kukasirika kunatokana na kujua kipya ambacho hukutegemea, huyu mungu mjuzi wa yote kipya kipi kitakachomtoa katika furaha na kumkasirisha?

5. Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo bila kujichanganya mwenyewe?

6. Unaweza kuthibitisha roho ipo na kuhakikisha kwamba si hadithi ya uongo tu?

7. Kama mungu anajua kila kitu na anapanga kila kitu, wanaosemwa kufanya dhambi na watahukumiwa siku ya hukumu kwa nini wanahukumiwa na wanaosemwa wamefanya mazuri wanapewa thawabu kwa nini wakati vyote vimepangwa na mungu?

8. Kama nipo njia panda, nataka kuamua kwamba nichukue njia ya kulia au ya kushoto, mungu anajua nitachukua njia gani? Kama anajua mimi nina maamuzi kweli? Kama hajui, mungu anajua yote kweli?

9. Kwa nini mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo wote hajiweki wazi watu wote tumjue bila utata?

10. Je, mungu anaweza kuumba jiwe zito kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Kama anaweza, basi kuna kitu hawezi, nacho ni kubeba hili jiwe, kama hawezi, basi kuna kitu hawezi, nacho ni kuumba hili jiwe. Either way mungu muweza yote hayupo. Unaweza kubisha?

Mimi nishaweka wazi hoja zangu ambazo hazijajibiwa. Zijibu. Weka zako.Nitazijibu, hata kama ni kwa kusema sijui tu.
 
Kukamilika hakumfungi mtu kufanya mambo mengine
Mungu aliamua kufanya uumbaji si kwa sababu hajakamilika,aliumba ili afurahie kazi ya mikono yake....!

Aliumba ili afurahie kazi ya mikono yake?

Ina maana alipungukiwa furaha?

Hujajibu swali langu la awali.

Unamlaumu shetani.

Shetani alitokeatokeaje?
 
Aliyetundikwa ni mwili wa Yesu,Immanuel wa Nazareth,ila roho yake haikufa,na ndio maana alisema,mikononi mwako baba,naiweka roho yangu

Tena akamwambia yule mwizi aliyetubu kuwa,kwa hakika usiku wa leo tutakuwa wote peponi...need i say more Mr Kiranga?

First off, unamchanganya Ibambasi na Kiranga.

Unaweza kuthibitisha kwamba roho ipo na si hadithi ya uongo wa kizamani tu? Inapimwaje?

Hujajibu swali hili.
 
Last edited by a moderator:
sehemu yenye kunguni ina uzuri gani wa kuishi?

Hahaha, dunia ina ma tsunami yanaua mpaka vitoto vichanga, ma Ebola ma vita ya kila aina.

Halafu mtu anakwambia imeumbwa na mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
'
What a sick joke!
 
Hoja ipi ya msingi sijaijibu? Hebu niulize hapa kweupeeeee watu wanasoma.

Mimi hoja zangu za msingi ambazo hazijajibiwa hizi hapa.

1. Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu wenye kuwezekana mabaya na maovu wakati uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya na maovu hayawezekani alikuwa nao?

2. Kwa nini mungu mwenye ukamilifu wote aumbe chochote? Kutaka kuumba ni kukosa ukamilifu, utasemaje mungu mkamilifu kaona haja ya kuumba wakati haja ya kuumba ni kukosa ukamilifu?

3. Imekuwaje mungu mjuzi wa yote na muweza yote akapanga mambo halafu akaghairi? Alivyoanza kupanga si alijua yote, kaghairi vipi tena?

4. Imekuwaje mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote akakasirika? Kukasirika kunatokana na kujua kipya ambacho hukutegemea, huyu mungu mjuzi wa yote kipya kipi kitakachomtoa katika furaha na kumkasirisha?

5. Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo bila kujichanganya mwenyewe?

6. Unaweza kuthibitisha roho ipo na kuhakikisha kwamba si hadithi ya uongo tu?

7. Kama mungu anajua kila kitu na anapanga kila kitu, wanaosemwa kufanya dhambi na watahukumiwa siku ya hukumu kwa nini wanahukumiwa na wanaosemwa wamefanya mazuri wanapewa thawabu kwa nini wakati vyote vimepangwa na mungu?

8. Kama nipo njia panda, nataka kuamua kwamba nichukue njia ya kulia au ya kushoto, mungu anajua nitachukua njia gani? Kama anajua mimi nina maamuzi kweli? Kama hajui, mungu anajua yote kweli?

9. Kwa nini mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo wote hajiweki wazi watu wote tumjue bila utata?

10. Je, mungu anaweza kuumba jiwe zito kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Kama anaweza, basi kuna kitu hawezi, nacho ni kubeba hili jiwe, kama hawezi, basi kuna kitu hawezi, nacho ni kuumba hili jiwe. Either way mungu muweza yote hayupo. Unaweza kubisha?

Mimi nishaweka wazi hoja zangu ambazo hazijajibiwa. Zijibu. Weka zako.Nitazijibu, hata kama ni kwa kusema sijui tu.
Hoja zako hizi hujazileta leo, ni za siku nyiingi, na baadhi yake (kama sio zote) zimeshajibiwa saana hapa jamvini.

Tatizo majibu yakitolewa huyataki. Kana kwamba unayo majibu yako tayari. Kwa hivyo kudebate na wewe kunakuwa kugumu sana.
 
Umechemsha kwa namna mbili.

1. Umeshindwa kujibu hoja zangu au kutoa link wapi nimejibiwa.
2. umeshindwa hata kunipa hizo hoja zako unazosema sijazijibu, hata baada ya kukuomba unipe nizijibu.

Inaelekea uvivu wa kufikiri umekukaa kwenye damu na hata huoni haya kusema sijazijibu hoja zako, nikakuuliza zipi, halafu hata usiniambie ni zipi.

Ushakubali kwamba hoja zangu huwezi kuzijibu.

Hoja zako zipi sijazijibu?
 
Mungu mwenye uwezo wote, ukamilifu wote na ujuzi wote kwa nini ahitaji kuumba binadamu?

Kuhitaji kokote, pamoja na kuhitaji kuumba, si kupungua ukamilifu?

Mungu mkamilifu angejitosheleza mwenyewe.

Kwa nini kaumba binadamu?

Aaaaaah Kiranga, toka lini kinyago kikamhoji mmakonde jinsi alivyo kitengeneza. Kama huamini ukuu wa Mungu basi fuata wanasayansi zaidi (evolution), ila utakapo rudisha namba ndio utatambua, ila nasikitika utakua umechelewa.
 
Hujajibu swali uliloulizwa, na ulilojibu hujaulizwa.
 
Kiranga, waamini/waumini wa Mungu tutakuwa na amani moyoni siku tukikubali kuwa:

Mungu ana mipaka (limit) ambayo hawezi kuivuka (transcend)

i.e.

Kama Mungu ni Pendo (Love) basi hawezi kuwa (na) Chuki (Hate)

i.e.

Upendo wa Mungu ndiyo mpaka wake - hawezi kuuvuka mpaka huo.

i.e.

Jambo Mungu (Pendo) hawezi/haliwezi ni kutokuwa Mungu (Pendo)
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom