1. Uwezo wote ni kutoshindwa kitu na unapimwa kwa mantiki. Ujuzi wote ni kutokosa kujua kitu na unapimwa kwa mantiki. Upendo wote ni kilele cha upendo na kipimo chake ni mantiki.
Nani kasema uwezo, ukanilifu na upendo ndio vitu vinavyohitaji (sic) kuumba ulimwengu mkamilifu?
2. Kilichokamikika hakihitaji kuumba, kuhitaji kuumba au kuhitaji kikote ni upungufu wa ukamilifu.
3. Kughairi ni kipanga kifanya kitu na baadaye kutengua usifanye. Mwenye kujua yote anayajua mambo yote mwanzo wake na mwisho wake, hivyo hawezi kughairi, mungu anayejua yote hawezi kughairi, mungu wenu inakiwaje aghairi mioango yake kama kweli anajua yote?
4. Kukasirika ni udhaifu wa kukosa kiweza kuhimili mhamaniko baada ya kugundua kukosa kupata unachotaka, mungu mwenye kujua yote, kuweza yote na upendo wote hawezi kukasirika kwa sababu hawezi kihamanika, hawezi kujua kipya cha kumkasirisha na hawezi kugundua kwani amejua yote, huyu mungu mnayesema anakasirika anakasirikaje?
5. Fallacy kubwa zaidi ni yako ya kusema fallacy by fiat bula kuitaja iko wapi na kivipi ni fallacy.
6. Wewe muamini mungu na roho unaniuliza mimi roho ni nini?
7. Ujuzi wa mungu wenu mnavyousema si utabiri wa hali ya hewa, au inataka kusema ujuzi wa mungu wenu ni wa kubahatisha kwamba anaweza kujua mvua itanyesha halafu isinyeshe? Ikiwa akijua itanuesha lazima itanyesha, tofauti ya ujuzi wake huo na kusababisha inyeshe ni nini? Hususan kwa sababu kila kitu kinaenda kwa command yake?
8. Ama mungu anajua yote na mwanadamu bana maamuzi, ama mwanadamu ana maamuzi na mungu hajui yote. You can't eat your cake and have it too.
9. Kama kajiweka wazi kabisa, mbona mimi sioni hivyo? Mbona ana contradictions kibao kama ya mungu mjua yote, muweza yote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu wenye mateso na mabaya? Hujajibu hili swali.
10. Hujajibu swali, umelikimbia tu.