Hoja ipi ya msingi sijaijibu? Hebu niulize hapa kweupeeeee watu wanasoma.
Mimi hoja zangu za msingi ambazo hazijajibiwa hizi hapa.
1. Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu wenye kuwezekana mabaya na maovu wakati uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya na maovu hayawezekani alikuwa nao?
2. Kwa nini mungu mwenye ukamilifu wote aumbe chochote? Kutaka kuumba ni kukosa ukamilifu, utasemaje mungu mkamilifu kaona haja ya kuumba wakati haja ya kuumba ni kukosa ukamilifu?
3. Imekuwaje mungu mjuzi wa yote na muweza yote akapanga mambo halafu akaghairi? Alivyoanza kupanga si alijua yote, kaghairi vipi tena?
4. Imekuwaje mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote akakasirika? Kukasirika kunatokana na kujua kipya ambacho hukutegemea, huyu mungu mjuzi wa yote kipya kipi kitakachomtoa katika furaha na kumkasirisha?
5. Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo bila kujichanganya mwenyewe?
6. Unaweza kuthibitisha roho ipo na kuhakikisha kwamba si hadithi ya uongo tu?
7. Kama mungu anajua kila kitu na anapanga kila kitu, wanaosemwa kufanya dhambi na watahukumiwa siku ya hukumu kwa nini wanahukumiwa na wanaosemwa wamefanya mazuri wanapewa thawabu kwa nini wakati vyote vimepangwa na mungu?
8. Kama nipo njia panda, nataka kuamua kwamba nichukue njia ya kulia au ya kushoto, mungu anajua nitachukua njia gani? Kama anajua mimi nina maamuzi kweli? Kama hajui, mungu anajua yote kweli?
9. Kwa nini mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo wote hajiweki wazi watu wote tumjue bila utata?
10. Je, mungu anaweza kuumba jiwe zito kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Kama anaweza, basi kuna kitu hawezi, nacho ni kubeba hili jiwe, kama hawezi, basi kuna kitu hawezi, nacho ni kuumba hili jiwe. Either way mungu muweza yote hayupo. Unaweza kubisha?
Mimi nishaweka wazi hoja zangu ambazo hazijajibiwa. Zijibu. Weka zako.Nitazijibu, hata kama ni kwa kusema sijui tu.
sasa ili ujibiwe lazima tuweke frequency zetu sawa.
1.-uwezo wote ni kitu gani na unapimwaje
-ujuzi wote ni nini na kipimo chake nini
-upendo ni nini na kipimo.chake nini ?
-Je ? kwanini unafikiri uwezo,ukamilifu na upendo ndivyo vitu vinavyohitajika kuumba ulimwengu mkamilifu ?
jibu ili tuondoe FALLACY OF DEFINITIONS.
2.Kwanini haja ya kuumba iwe ndicho kipimo cha kukosa ukamilifu ?
3.nini maana ya kughairi na uhusiano wale na ujuzi wote ukoje ?
4.kukasirikia ndiyo nini na nini kipimo chake kadri ya Mungu anavyohusika ?
5.inawezekana kabisa kama tutaondoa FALLACY OF DEFINITION zinazoathiri uwezo wako wa kufikiri.
6.Ndiyo baada ya kuondoa FALLACY OF DEFINITION. Roho unayohoji uwepo wake ni nini ?
7.kuna husiano gani kati ya kujua kila kitu na kuenfluence uchaguzi wa binadam mwenye free will ?
tiondoe kwanza FALLACY OF DEFINITION ili utibiwe ipasavyo.
8.kujua na kumfanya mtu aamue ni vitu viwili tofauti...
lakini tuondoe kwanza msingi wa tatizo linalokukabili ndiyo tukufundishe...
9.Mungu kajiweka wazi kabisa kwa wenye nia ya kumjua rejea zipo.
labda Mungu ni.nini au ni nani ?
Tuondoe FALLACY OF DEFINITION.
10. Swali lako limejibiwa mara nyingi sana japo kulariri kunakufanya ushindwe kujitambua na kuona jibu.
kuunda jiwe kubwa na kuweza kulibeba ni sehemu ya mwenye uwezo wote.
lakini kuumba jiwe kubwa na kushindwa kulibeba ni hoja ya kichaa maana uwezo wote ni kinyume cha kukosa uwezo.
Safisha uwanja kwa kuondoa hizo FALLACIES then upelekwe jando.