Irish Times - Tanzania Inahatarisha Dunia

Irish Times - Tanzania Inahatarisha Dunia

Mkuu unajuaje hatujafa kwa maelfu wakati haturipoti wala kupima wagonjwa wa corona?Vifo vinavyotokea mtaani na kwa wakubwa vinaashiria idadi ya vifo ni kubwa.
Kwa kusema hivi inamaana kama hapo zamani watu walikuwa hawafi? Jiulize mwaka jana umehudhuria misiba mingapi na sababu zipi za hao watu kufa na mwaka huu pia umehudhuria misiba mingapi na sababu ni zipi za vifo hivyo.
 
Ni kweli maambukizi na vifo vinavyotokana na corona, kwa mataifa mengi vimepungua sana kutokana na hatua mbalimbali walizochukua. Mataifa kama US, UK, Israel wamefanikiwa sana kupunguza vifo, japo cumulative number ukiangalia utaona inazidi kupanda. Lakini vifo na maambukizi kwa siku vimepungua kwa kiwango kikubwa sana. Marekani vifo vinapungua kwa wastani wa 40% kwa wiki, UK wamepunguza wastani wa cases 28 kwa siku, Israel wamepunguza vifo kwa 94%. Haya Ni mafanikio makubwa sana.

Lakini kinachowasaidia sana ni ukusanyaji wa taarifa. Huu utaratibu wa kwetu wa kutoakupima na kutoa takwimu ni wa kijinga, kishamba na kimbumbumbu kabisa. Takwimu ni muhimu sana katika jambo lolote. Ndiyo zinakupa picha ya ukubwa wa tatizo, ndizo zinakuongoza kuona kama mbinu zako zinafanya kazi au hapana.

Kutokupima na kutokutoa takwimu, kwa kweli kunafanya elimu ya Rais Magufuli kutiliwa mashaka makubwa sana. Ni mwanasayansi gani hajui umuhimu wa utafiti na takwimu? Labda alisoma tu masomo ya sayansi lakini hajui sayansi.
Unasema vifo vimepungua kwa takwimu tunazoletewa na BBCSWAHILI na dadaako Zuhura Yunusi beberu wa kizanzibari.
Zinaaminika vipi hizo takwimu zao kama ni za kweli?
Hata marekani wanakaa wanajinadi kama democrasia ipo nchini mwao na haki za binaadamu lakini wamarekani wenyewe wakihojiwa wanakuambia hakuna haki za binaadamu kwa mtu mweusi toka enzi na enzi lakini wao kwenye takwimu za bbc na kwenye karatasi wanasema haki zipo.
 
Wazimu wa dini umetoka kwa mabeberu pia.

Na inaonekana ni hatari kuliko hata korona kwa sasa.

Muasisi wa taifa letu alisema maadui zetu wakubwa ni ujinga, maradhi na umasikini.

Hakukosea.

Ujinga ukiongezeka unachochea kuongezeka kwa maradhi na vyote viwili vinachochea kuongezeka kwa umasikini ambao nao unazaa ujinga zaidi ukiwamo huu wazimu wa kidini.

Mduara katili sana ambao watanzania tumeshindwa kuuvunja.
 
Kwa kusema hivi inamaana kama hapo zamani watu walikuwa hawafi? Jiulize mwaka jana umehudhuria misiba mingapi na sababu zipi za hao watu kufa na mwaka huu pia umehudhuria misiba mingapi na sababu ni zipi za vifo hivyo.
Sababu za misiba za kipindi hiki ni shida ya kushindwa kupumua aka corona tofauti na kipindi cha nyuma misiba ilikuwa very rarely na shida sio kupumua ni matatizo mengine kabisa malaria,moyo nakadhalika.Mbona hili lipo wazi mkuu.

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 
Kipindi cha nyuma si ndio mlikuwa mnasema watu wanakufa kimya kimya na kulikuwa na lawama kwa serikali kuliko sasa.
 
Mm ninachojiuliza kama chanjo ipo, na chanjo inazuia maambukizi, wakichanja watu wao si hawataambukizwa na sisi?

Ss tatizo linakuja wapi? Au wanatupenda sana hawataki tufe kwa kutochanjwa? Pamoja na umri kwenda ila sijaona bado mantic ya kulazimishana chanjo. Ntashukuru kama walioelewa watanipa elimu.
 
Back
Top Bottom