Iringa: Wakala wa malipo anaswa akidaiwa kuiba TSh Bilioni 2.1, Polisi wafanikiwa kuokoa TSh Milioni 956

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan L. Bukumbi ametoa ripoti ya matukio kadhaa ikiwemo lililohusisha wizi wa zaidi ya Shilingi Bilioni mbili mkoani humo.

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linafanya Uchunguzi/Upelelezi dhidi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za kitanzania kiasi cha TSh 2,129,856,000= mali ya kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED ambapo wakala wa Selcom aitwaye TYSON KASISI wa mkoani Iringa kupitia huduma ya ‘Selcom Pay’ isivyo halali alihamisha fedha kwenda nambari mbalimbali za simu na kisha kuchukuliwa taslimu kupitia wakala wa huduma za kifedha za mitandao mbalimbali ya simu pamoja na akaunti za Benki.

Wizi wa fedha hizo ulifanyika kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa, Dar es Salaam na Morogoro kati ya tarehe 9 Novemba 2021 hadi 27 Novemba 2021 baada ya wakala huyo TYSON KASISI kufanikiwa kuchezea mfumo wa kieletroniki wa ‘Selcom Pay’ unaomilikiwa na Kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED.

Wakala huyo kwa njia ya udanganyifu alianza kujitumia fedha pamoja na kuwatumia watu wengine na kwa kushirikiana na genge lake la uhalifu walifanikiwa kuiba kiasi hicho cha TSh 2,129,856,000=.

Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata (Kuokoa) fedha taslimu kiasi cha TSh 956,974,000= kutoka kwa watuhumiwa na washiriki wa uhalifu huo ambao walipokea sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuzificha katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi na shambani.

Aidha, kiasi cha fedha za kitanzania TSh 121,215,783= zimezuiliwa katika moja ya benki za biashara mkoani Iringa ikiwa ni mazalia ya uhalifu.

Upelelezi uliofanyika mpaka sasa umebaini kuwa genge la uhalifu na wizi wa fedha za Selcom uliongozwa na watu watatu ambao ni TYSON KASISI, PATRICK CHALAMILA na EVARISTO CHALAMILA ambao wamebainika kuwa wanufaika wakuu wa uhalifu huo.

Halikadhalika, mali ambazo ni mazalia ya uhalifu zimekamatwa na kuhifadhiwa ikiwa ni magari manne (4) yenye thamani ya TSh 303,000,000= ambayo ni;

i. SCANIA yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 128, 000,000=.

ii. MITSUBISH FUSO usajili namba T 796 DXV yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 75,000,000=.

iii. TOYOTA HARRIER usajili namba T 719 DXX yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 72,000,000=.

iv. NISSAN JUKE usajili namba T 605 DXV yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 28,000,000=.

Pia imekamatwa gari Toyota IST yenye namba za usajili T 576 DRN mali ya PATRICK CHALAMILA lililotumika kufanikisha uhalifu kwa kusafirisha fedha za wizi kutoka Madibira Wilayani Mbarali na Ilula Wilayani Kilolo kwenda kuzificha Kilombero mkoani Morogoro.

Ushahidi uliokusanywa mpaka sasa umetosha kuwafikisha watuhumiwa kumi (10) Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwa makosa ya Kuongoza Genge la Uhalifu na Kujipatia Fedha kwa njia ya Udanganyifu.

Daaaaaaah wangetoboa tayariii
 
Sio kibongo bongo, technolojia ni finyu saana. Hapo wangekua smart wasingekamatwa hata mmoja, traces zote za ushahidi wanafuta, mkwanja wanaingiza kwenye bitcoin wallet, apo inakua imeishaa hakuna mbwa atakaeweza kujua.
Unafutaje trace na huna access na platform, vitu vingine tusiongee ili ujulikane unajua
 
Hili jeshi Bana, MADIBIRA kuna wakulima wa mpunga Kilombero hali kadhalika,
Jeshi haliwezi kujisafisha waje na haya mapichapicha, hata watumie mchanganyiko WA mafuta ya tas, diesel, mchanga, chlorine, maji ya betri ngumu Sana kulisafisha,

Hii ID ya kututangazia matukio mema mazuri ya jeshi siyo??
 
Uongo tu mnatengeneza drama zenu ili watu wasahau habari ya mtwara,mtu aibe hela yote hyo ashindwe kuitunza.
 
Harrier 72M
Hybrid hizi new modelView attachment 2117768View attachment 2117769
download%20(1).jpg
 
Hawa jamaa wameiba pesa, bila yakujipanga! Unaweza vipi kuiba pesa ndefu kama hii,na bado ukawa upo Tanzania unashangaa mataa??

Yaani nipige pesa kama hii,napotea kabisa Tanzania,narudi baada ya miaka kadhaaa
Mkuu usitukane wakunga uzazi ungalipo.

Huo mchakato wa kuikimbia nchi ndiyo mchakato wa kusweka ndani.

Mtu kafa, usije ukamcheka marehemu kwa uzembe ulosababisha madhila ya kifo chake, elewa kuwa zako hazijafika tu, nawe waweza ukaja kufa kizembe zaidi ya marehemu!

Vinginevyo, wahalifu wasingelikuwa wanabambwa.

Walivyo ndani sasa hivi, ndiyo njia "njema" za kufanya waepuka kukamatwa zinawajia vizuuuri vichwani mwao!

Mambo haya, wee acha tuu!
 
Mkuu usitukane wakunga uzazi ungalipo.

Huo mchakato wa kuikimbia nchi ndiyo mchakato wa kusweka ndani.

Mtu kafa, usije ukamcheka marehemu kwa uzembe ulosababisha madhila ya kifo chake, elewa kuwa zako hazijafika tu, nawe waweza ukaja kufa kizembe zaidi ya marehemu!

Vinginevyo, wahalifu wasingelikuwa wanabambwa.

Walivyo ndani sasa hivi, ndiyo njia "njema" za kufanya waepuka kukamatwa zinawajia vizuuuri vichwani mwao!

Mambo haya, wee acha tuu!
Linakuaga kama pepo hata muhusika mwenyewe ukifikiria huelewi
 
Die Rich or Keep Trying !!! (Unfortunately this one didn't work that way !!)
 
Back
Top Bottom