IRINGA MJINI: Wafanyabiashara wagoma kufungua maduka na biashara zao kupinga uonevu wanaofanyiwa na Manispaa ya Iringa

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,027
5,258
Leo tarehe 15.06.2023 wafanyabiashara wa Iringa mjini wamegoma kufungua biashara zao baada ya askari wa manispaa ya Iringa jana kuvunja na kuharibu biashara zao kwa kuvunja vibaraza vya maduka. Jambo hilo limeharibu mali zao wafanyabiashara na pia kufungwa kwa biashara kumesababisha kukosekana kqa huduma kwa wananchi kwani maduka yote yamefungwa.

Wafanyabiashara wanalalamika kitendo cha kuzuiwa kuweka vitu (bidhaa) nje ya maduka yao wakilazimishwa na manispaa waweke bidhaa zao ndani ya maduka.

Wafanyabiashara hao wamekusanyika eneo la stendi kuu ya Iringa mjini wakitaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa ili awasikilize kero zao.

Baada ya kusubiri sana, saa 5:07 asubuhi ndio Mkuu wa Mkoa amewasili eneo hilo na wafanyabiashara wameanza kutoa kero zao.

Mkuu wa Mkoa anatishia kuondoka kurudi ofisini baada ya katibu wa wafanyabiashara kusema kuwa hawapo tayari kukubali wazo la kutoweka biashara nje ya maduka.

Updates:
Baada ya kusikiliza hoja za wafanyabiashara, Mkuu wa Mkoa ametoa amri ya kusitisha zoezi la ubomoaji wa vibaraza vya maduka mpaka pale manispaa watakapojadiliana na wafanyabiashara.

Pia Ameagiza walioharibiwa mali kufanyiwa uthamini wa mali zao na pia wafanyabiashara wamekubaliana na hoja hizo na wamekubali kufungua biashara zao.

Wafanyabiashara waliokuwa wamekamatwa jana na kushukiliwa polisi, wameachiwa.

Saa 5:51 asubuhi, maduka yameanza kufunguliwa ili wananchi wapate huduma
IMG_20230615_105958_1.jpg
IMG_20230615_105956_1.jpg
IMG_20230615_105948_1.jpg
IMG_20230615_105944_1.jpg
IMG_20230615_105938_1.jpg
 

Attachments

  • IMG_20230615_105934_1.jpg
    IMG_20230615_105934_1.jpg
    884.3 KB · Views: 2
  • IMG_20230615_101037.jpg
    IMG_20230615_101037.jpg
    940.8 KB · Views: 2
  • IMG_20230615_101040_1.jpg
    IMG_20230615_101040_1.jpg
    895.2 KB · Views: 2
  • IMG_2023-06-15-10-08-32-554.jpg
    IMG_2023-06-15-10-08-32-554.jpg
    1.4 MB · Views: 2
  • IMG_20230615_100731_1.jpg
    IMG_20230615_100731_1.jpg
    1.1 MB · Views: 2
  • IMG_20230615_100729.jpg
    IMG_20230615_100729.jpg
    1.2 MB · Views: 2
  • IMG_2023-06-15-10-06-59-592.jpg
    IMG_2023-06-15-10-06-59-592.jpg
    1.3 MB · Views: 2
Hii nchi ya ajabu sana badala wakomae na bandari kule ili izidi kuingiza pesa wao wanaibinafsisha na wanakomaa na wafanya biashara wasipange bidhaa zao nje.
 
Bila sababu yyte wameambiwa wasiweke bizaa nje? Tuanzie hapo kwanza
 
Baada ya kusikiliza hoja za wafanyabiashara, Mkuu wa Mkoa ametoa amri ya kusitisha zoezi la ubomoaji wa vibaraza vya maduka mpaka pale manispaa watakapojadiliana na wafanyabiashara.

Pia Ameagiza walioharibiwa mali kufanyiwa uthamini wa mali zao na pia wafanyabiashara wamekubaliana na hoja hizo na wamekubali kufungua biashara zao.

Wafanyabiashara waliokuwa wamekamatwa jana na kushukiliwa polisi, wameachiwa.

Saa 5:51 asubuhi, maduka yameanza kufunguliwa ili wananchi wapate huduma.
 
Back
Top Bottom