Iran yazionya Marekani na Israel juu ya 'matokeo hasi makali' endapo jinai za kivita zitaendelea Gaza

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,646
3,936

Iran yazionya Marekani na Israel juu ya 'matokeo hasi makali' endapo jinai za kivita zitaendelea Gaza​

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amezionya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba zitakabiliwa na "matokeo hasi makali" iwapo zitashindwa kukomesha kikamilifu uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza uliofanywa wakati wa vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya eneo Palestina lililowekewa mzingiro.

Amir-Abdollahian ameyasema hayo katika mahojiano na chaneli ya televisheni wa Al Jazeera ya Qatar yaliyochapishwa leo Jumanne, huku kukiwa na mapatano ya muda ya usitishaji vita huko Gaza ya utawala wa Kizayuni na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameonya kwa kusema: "ni muhimu kwamba uchokozi na uhalifu [wa Israel] lazima ukomeshwe na usitishaji vita wa muda lazima uwe wa kudumu. Vinginevyo, eneo litashuhudia hali nyingine mpya".

Ameongezea kwa kusema: "utawala wa Kizayuni na Wamarekani itawapasa wakubali matokeo hasi makali ya kushindwa kukomesha uhalifu wa kivita".

Usitishaji vita wa siku nne katika Ukanda wa Gaza uliomalizika jana Jumatatu, umerefushwa kwa siku mbili zaidi na kupelekea kusimamishwa vita angamizi vilivyoanzishwa na utawala katili wa Israel dhidi ya eneo hilo la Palestina na kufanyika zoezi la kuachiwa huru Wapalestina waliokuwa wakiteseka na kuatilika ndani ya magereza ya Israel na mateka wanaoshikiliwa na harakati ya Hamas.

Uharibifu uliofanywa na Jeshi la Kizayuni Ukanda wa Gaza
Katika mahojiano hayo na Aljazeera, Amir-Abdollahian ameendelea kueleza kwamba, Israel inakaribisha kuendelea na kupanuka kwa vita endapo Marekani itaendelea kuunga mkono kikamilifu mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Ameongezea kwa kusema, Tehran imearifiwa kupitia duru za ubadilishanaji wa taarifa kwamba Ikulu ya White House hivi karibuni imegundua kwamba kuendelea kwao kuiunga mkono Israel si kwa manufaa yake.

Mwanadiplomasia mkuu wa Iran amebainisha kuwa, utawala ghasibu wa Israel umeshindwa kuiangamiza Hamas katika kipindi cha wiki sita zilizopita licha ya kupata msaada na uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na nchi washirika wa Washington.

Amir-Abdollahian amesisitiza kwa kusema: "Hamas ni uhakika uliojikita na kutoa mizizi ndani ya Palestina. Hamas ni sehemu ya Muqawama wa Wapalestina, na tunaamini kwamba mustakabali wa Gaza utaamuliwa na watu wa Palestina.

1701193752982.png
 
View attachment 2827979
Huu ushabiki unasuasua nini wakati watu na mali vinateketea.vita kaanzisaha Israel au Hamas aliyevamia na kuua na kuteka.
Ninachojua mimi Hamas wameshahundwa ,hadi ardhi imejaliwa na IDF bado unasema wameshindwa!
 
Putin alisema atakayeisaidia Ukraine atakiona cha moto. Sasa sijajua kwa nini aliamua kukaa kmya mpaka leo. Kusema ni rahisi ila vitendo ni vigumu kutekeleza.
Kuna siku, Hawa wanaotoa maonyo watashitukizwa na kitu kikali. Waendeleee na maonyo tuuu
 
Iran iko mbali! Inawadanganya Wapalestina ambao ni Wahanga wa Vita hivyo vinavyoendelea!
Kama Iran inajiamini si itume jeshi lake Israel ikampambane na IDF?
 
Kiburi cha Israel kinakwenda kupatiwa dawa ya kudumu muda si mrefu
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kutekeleza mauaji ya kimbari huko Gaza Palestina huku asasi zote muhimu za kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zikishindwa kusitisha unyama huo wa Israel.
 
Putin alisema atakayeisaidia Ukraine atakiona cha moto. Sasa sijajua kwa nini aliamua kukaa kmya mpaka leo. Kusema ni rahisi ila vitendo ni vigumu kutekeleza.
Hapo usichoelewa nini ipo wazi G7 wamekataa kuingia vitani ila wataisaidia Ukraine vifaa vya kivita na ipo mpk sahv Ukraine wanapigana wenyewe
 
Back
Top Bottom