Iran yajaribu kupitisha Uranium Tanzania!

Iran yajaribu kupitisha Uranium Tanzania!

VZCZCXRO1511
PP RUEHMR RUEHRN
DE RUEHDR #1593 2700838
ZNY CCCCC ZZH
P 270838Z SEP 06
FM AMEMBASSY DAR ES SALAAM
TO RUEHC/SECSTATE WASHDC PRIORITY 4811
INFO RUCNSAD/SOUTHERN AFRICAN DEVELOPMENT COMMUNITY PRIORITY
RUEHSW/AMEMBASSY BERN PRIORITY 0116
RUEHKI/AMEMBASSY KINSHASA PRIORITY 0214
RUEAIIA/CIA WASHINGTON DC PRIORITY C O N F I D E N T I A L DAR ES SALAAM 001593

SIPDIS

SIPDIS

AF/E FOR BYODER, AF/RSA FOR MBITTRICK
ALSO VCI FOR HHEINTZELMAN AND KWALKIN

EO 12958 DECL: 09/27/2016
TAGS PTER, PINR, IAEA, PGOV, CG, TZ
SUBJECT: URANIUM IN DAR COMMON KNOWLEDGE TO SHIPPING
COMPANIES, PER SWISS DIPLOMAT

REF: A. DAR ES SALAAM 01376 B. UNVIE VIENNA 00601 C. KINSHASA 01309

Classified By: Charge d’Affaires D. Purnell Delly for reasons 1.4(b),(d) and (e).

http://www.wikileaks.no/cable/2006/09/06DARESSALAAM1593.html#par1

1. (C) According to a senior Swiss diplomat, the shipment of uranium through Dar es Salaam is common knowledge to two Swiss shipping companies. Hans Peter Schoni, Counsellor at the Embassy of Switzerland in Tanzania, referred to the allegations of uranium from the Democratic Republic of Congo (DRC) passing through Zambia and Tanzania en route to Iran, but did not attribute to the shipping companies any opinion of the source or destination of the alleged uranium. Poloff pointed out that the reports were unsubstantiated, but Schoni repeated that transport of uranium is common knowledge to the two companies, though no one at either company would admit it in writing. XXXXXXXXXXXX are both based in Geneva and conduct verification and inspection work in Tanzania.

http://www.wikileaks.no/cable/2006/09/06DARESSALAAM1593.html#par2

2. (C) Mission has shared this information with all relevant agencies at post which were unable to substantiate this or any other such reports of uranium shipments. Nevertheless, given the potential significance of such allegations we believe it is important to report nonetheless. DELLY
 
*Yadai ndicho kitovu cha usafirishaiji Urenium kwenda Iran



BAADA ya tovuti inayovujisha siri nyeti kuhusu serikali mbalimbali duniani kudai kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inakwamishwa na Rais Jakaya Kikwete, imedai kufichua siri nyingine nzito inayodai kuwa Tanzania ni kitovu cha usafirishaji wa madini ya uranium kwenda Iran.

Kwa mujibu wa Wikileaks, Marekani inazishutumu nchi mbili katika ukanda wa Afrika Mashariki ambazo ni Kenya na Tanzania kwa kuwa kitovu cha usafirishaji kinyemela madini hayo hatari.

Mtandao wa Wikileaks ambao ulifichua siri mbalimbali za balozi za Marekani unaitaja Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kuwa chimbuko la madini hayo ambayo, baada ya kusafishwa, hutumika kutengeneza nguvu ya umeme au mabomu.

Mtandao huo unaodai kufichua siri nyeti za kibalozi kutoka mjini Kinshasa hadi Dar es Salaam unaeleza kuwa madini hayo ya uranium yanachimbwa na kampuni za kigeni katika Jimbo la Katanga kabla ya kampuni hizo kuyasafirisha kwenda Iran kupitia nchi za Tanzania na Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mwanadiplomasia wa Marekani aliyekuwa mjini Dar es Salaam Septemba 2006, Purnell Delly, anadaiwa kuripoti kwa wakuu wake mjini Washington, Marekani, akisema inafahamika wazi kuwa shehena za madini ya uranium imekuwa ikipita katika bandari ya Dar es Salaam zikiwa njiani kwenda Iran.

Taarifa hiyo inadai kuwa miwili baadaye Polisi wa Kenya waliamua kuingilia kati suala hilo kwa kile walichohisi kuwa ni Uganda kusafirisha madini hayo kutoka DRC.

Polisi hao walifanikiwa kukamata vifaa vyenye milipuko ya hali ya juu huku wakiwatia mbaroni wanaume wawili waliodai kununua vitu hivyo kutoka DRC kwa sh. milioni 3.9 za Kenya na kwamba walipanga kuviuza mjini Nairobi kwa sh. Milioni 100 za Kenya.

Mei mwaka huu, Polisi nchini Kenya walifanikiwa kukamata kilo 10 za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni madini ya uranium, hali ambayo ilizua taharuki kwa Jumuiya za Kimataifa kwamba Kenya ilikuwa ikitumika kama njia ya kusafirishia madini hayo kutoka DRC.

Wikileaks pia ulimnukuu Balozi wa Uswisi akidai kuwa Afrika Mashariki ndiyo njia kuu ya kusafisha madini hayo.“Kwa mujibu wa mwanadiplomasia mwandamizi wa Uswisi, usafirishaji wa uranium kupitia bandari ya Dar es Salaam unafahamika vyema baina ya kampuni mbili za meli kutoka Uswisi,” aliandika Delly.

“Hans Peter Schoni, ambaye Kansela wa Uswisi nchini Tanzania, alishazungumzia tuhuma za madini ya uranium kutoka DRC kupitishwa katika nchi za Zambia na Tanzania kwenda Iran, lakini hakupewa jibu lolote kutoka kwa kampuni husika ama mahali panapodaiwa kupelekwa madini hayo,” aliongeza mwanadipolimasia huyo.Alielezea kusikitishwa kwake pamoja na taasisi husika lakini haijawahi kuthibitishwa ama kukanushwa ripoti hizo kuhusu meli meli hizo za uranium.

“Haifahamiki wazi kama kampuni ya Malta Forest ama kampuni nyinginezo zilizopo katika Jimbo la Katanga zinahusika na usafirishaji wa uranium. Mazingira ya kuwapo kwa biashara hiyo yanaonekana lakini ushahidi wa uhakika ndio hauonekani,” aliripoti mwanadiplomasia wa Marekani mjini Kinshasa, Dpopovich Econoff.“Vilevile kuna faida kubwa kutokana na kiwango cha uranium kinachozalishwa na kampuni ya Malta Forest's Mines, hususani tangu bei ya madini hayo ilipopanda kutoka wastani wa bei ya dola 15 mwaka 2004 na kufikia wastani wa dola 135 kwa paundi mwaka 2007,” alifafanua.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo, madini hayo yanachimbwa kwa wingi na kampuni zinazomilikiwa na vigogo wa Serikali ya DRC na kusafirishwa nje ya nchi kwa njia za magendo na mitandao ya rushwa.

Alisema mfano kampuni ya Malta Forest inahusishwa na mshauri wa Rais Joseph Kabila huku kampuni za Uswizi na Finland zikijipatia faida kubwa kutokana na madini hayo katika Jimbo la Katanga.
 
Si tunataka kujiunga na OIC lazima tujibembeleze nao mweh
 
Unajua kwangu mimi hii sio habari mpya.Taarifa zilikuwepo zinazo mnyooshea kidole ZIZAMA TSOR kuwa anahusika na kazi hiyo. Mwenye akili na afahamu.Inasemekana huyu bwana ni sleper agent na yuko hapa kwa kazi nyeti
 
Tunadhania tumejificha kumbe watu wanatuchora tu. Hii wikileaks itaharibu mambo mengi sana. Wait and see!!
 
Haya sasa ualifu wa CCM peupeeeeeeeeeeeee........na bado tutasikia mengi zaidi!!!
 
Tulidhani wanamtandao wanafanya mambo yao hapa hapa hasa kwenye uchaguzi; sasa tufunguke macho huu ni global mtandao
 
Aibu imewakuta..hiyo ndio aina ya viongozi tulionao Tanzania!
 
haya sasa ualifu wa ccm peupeeeeeeeeeeeee........na bado tutasikia mengi zaidi!!!

bakii na sisiemu na sie tukafukue kule shinyanga jamani yapo uwanja mzima wa mpira na watu washaanza kupewa viamba swala si kelele kamata na we chako chapa lapa
 
Mwee, mwe mwe mwe!!!!!!!!!!!!! Tanzania tena, haki yanani twafwa!! Huu ni uozo wa Kikwete na srikali yake. Kuna siku !!
 
Haina neno hiyo kama wanalipa ushuru.....Sisi marekani siyo walinzi wetu wa kutuzuia kufanya biashara.
Sisi ni nchi huru na tuna uwezo wa kua rafiki na nchi yeyote duniani kwa maslahi ya nchi yetu.
 
Kwa hilo tusipokuwa makini utakuja sikia viongozi waandamizi wa ccm kutakiwa the haig kwa kosa la uhalifu wa kivita yaani kuwasaidia wairan. mkwere komaa na intelligence yako japo uisaidie wikileaks kupata info uepukane na balaa
 
Haina neno hiyo kama wanalipa ushuru.....Sisi marekani siyo walinzi wetu wa kutuzuia kufanya biashara.
Sisi ni nchi huru na tuna uwezo wa kua rafiki na nchi yeyote duniani kwa maslahi ya nchi yetu.
Nchi huru wakati mlo unatoka Marekani?Siku tukiacha kuomba omba ndio tutakua na nchi huru!Untill then....they own us!
 
Back
Top Bottom